PENDEKEZO: CHADEMA iahirishe maandamano ya Machi 25

PENDEKEZO: CHADEMA iahirishe maandamano ya Machi 25

makesy

Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
75
Reaction score
32
Kwanza nawasalim
pili naomba kuwashauri kwakuwa polisi wamezuia maandamano yetu ya kesho kwa visingizio mbalimbali ikiwemo ya mchina kuja tanzania na ccm kufanya maandamano kesho hiyohiyo naomba nishauri yafuatayo kesho tuwaachie ccm waandamane na mchina aje tanzania sisi tupange maandamano yetu siku nyingine na nashauri yawe baada ya pasaka na iwe siku ya j mosi ili kupata wafuasi wa kutosha maana siku za kazi wengine tunafanya kazi serikalini tukiacha kazi tukaenda kuandamana tunaweza kupoteza kibarua pili tukilazimisha kufanya kesho wakati wameshakataza mwitikio utakuwamdogo na wao wakapata ya kusema. Naomba tutumie busara nawasilisha.
 
Alipoulizwa itakuwaje maana kutakuwa na
ugeni wa Rais wa China nchini, sababu
ambayo hata serikali imeitumia ili kuyazuia
maandamano hayo, Mbowe alijibu:
“Kilio chetu hakikuja na Rais wa China, kama Serikali ya CCM wanaona aibu
kumwajibisha waziri mmoja na naibu wake,
basi wasubiri aibu ya dunia kuona jinsi
Tanzania inavyoendeshwa kibabe, ikiwa
haina elimu bora.

“Tumetangaza maandamano wiki tatu
zilizopita, hatukuwa na taarifa na ujio wa
Rais wa China, lakini jinsi Mungu alivyo
upande wetu amemleta Rais wa China,
kweli Mungu ni mwema, hakuna tena nafasi
ya kusubiri kuficha ubovu katika sekta ya
elimu nchini, ndani ya siku ambayo
CHADEMA waliandaa maandamano ili dunia nzima isikie kilio cha Watanzania kuhusu elimu.

“Sababu kuwa CCM nao wameandaa
maandamano kupinga maandamano ya
CHADEMA hazina msingi ni kutowajibika
kwa Jeshi la Polisi. Hatukatazi maandamano, polisi wapange ratiba siku
tofauti, sisi tutaandamana kumpinga waziri
ili kama CCM wataandamana kumpongeza
waziri wao wapangiwe siku yao, ila sisi
tulitangaza mapema na barua tulipeleka
kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.”

Mkuu, hope umeelewa. Kutoshiriki maandamano haya ni ubinafsi kwa wadogo zetu, ndugu zetu na elimu ya tanzania kwa ujumla

Viva cdm,
Tulianza na Mungu, tutamaliza na Mungu
 
Naunga mkono hoja, ukiona hadi Idara ya Habari Maelezo inatumika ujue chu.pi zinawabana maCCM kwa kuogopa maandamano. Kwa kuwa Kikwete ni dikteta ambaye ameishaua watu wengi toka ameingia madarakani atawaamuru polisi wake waue watu wengine tena kesho.
 
ninakuelewa vizuri kamanda lakini kumbuka nia ya maandamano ni kuionyesha serikali kuwa tumechoka sasa kama wataandamana watu wachache kwa kuogopa tangazo la polisi ujue lengo letu litafeli na ccm itapata maneno ya kutukejeli tafakari kwa makini kuu
 
kwanini Kawambwa na Mulugo wasijiuzuru au walazimishwe kujiuzuru ili maandamano yasiwepo? 90% watoto kufeli kwanini?

Hawa 90% wataishia kutupora mali zetu, watakuwa majambazi, watakuwa wadokozi, watakuwa matapeli nk je tupo teyari kuona taifa la tanzania linageuka kuwa la kizazi cha majambazi, matapeli, wadokozi nk. maana kufeli kumeanza muda mrefu na matokeo yamendelea kuwa mabaya zaidi kila tunavyosonga mbele.

Lazima tuchukuwe hatua kuliepusha taifa na balaa inayokuja mbele yetu, hivo vigari vyenu,vikorora, suzuki, benz nk hamtaviendesha kwa amani na huko kwenye mahekalu yenu hamta lala salama maana ujambazi utakomaa na wataingia na mageti mazimamazima kuja kupora. Unadhani hii 90% itakubali kufa njaa na kutaabika wakati wachache wanashiba na kusaza ndani ya mageti?

Tunapashwa kuchukuwa hatua sasa ili tuitafute Tanzania yenye neema kwa wote kwa amani, haki na upendo kila mtu atafaidi jasho na mali yake bila kuvunjiwa mageti na kupolwa magari.
 
Kwanza nawasalim
pili naomba kuwashauri kwakuwa polisi wamezuia maandamano yetu ya kesho kwa visingizio mbalimbali ikiwemo ya mchina kuja tanzania na ccm kufanya maandamano kesho hiyohiyo naomba nishauri yafuatayo kesho tuwaachie ccm waandamane na mchina aje tanzania sisi tupange maandamano yetu siku nyingine na nashauri yawe baada ya pasaka na iwe siku ya j mosi ili kupata wafuasi wa kutosha maana siku za kazi wengine tunafanya kazi serikalini tukiacha kazi tukaenda kuandamana tunaweza kupoteza kibarua pili tukilazimisha kufanya kesho wakati wameshakataza mwitikio utakuwamdogo na wao wakapata ya kusema. Naomba tutumie busara nawasilisha.

wazo linazungumzika ila tujiulize yafuatayo؛
1. Cdm walipopanga tar.25 siku ya j3 kuna vigezo walizingatia
2.kati ya hizo sababu walizotoa polisi kuwa xi jinping na ccm kuandamana zina holdwater?
3.cdm wakibadili tarehe kwa kuzingatia ushauri wako kahali hii kandamizi watapewa kibali?
 
wazo linazungumzika ila tujiulize yafuatayo؛
1. Cdm walipopanga tar.25 siku ya j3 kuna vigezo walizingatia
2.kati ya hizo sababu walizotoa polisi kuwa xi jinping na ccm kuandamana zina holdwater?
3.cdm wakibadili tarehe kwa kuzingatia ushauri wako kahali hii kandamizi watapewa kibali?

bado sipingi hoja yako lakini waswahili wana sema njia ya mwongo ni fupi endapo tutaahirisha na tarehe nyingine polisi wakatoa tena visingizio hapo tutaamua la kufanya swala la siku ya j3 mimi nimeshauri ibadilishwe iwe jmosi kwa nia ya kupata wahudhuriaji wengi maana suku ya kazi ukiwa mfanyakazi wa serikali halafu waziri wa kazi akasikia ulitoroka kazini ukaenda kuandamana kuipinga seikali sijui kama utaendelea kuwa na kibarua likini kama waliopanga j3 walikuwa na sababu za msingi mimi sipingi ila na mmi ningependa nishiriki hayo maandamano mimi na familia yangu maana niwaathirika wa matokeo hayo mabaya ya mtihani.
 
Hivi kuna upotoshaji wa makusudi juu ya tarehe rasmi ya maandanano ya CHADEMA kutaka waziri wa elimu ajiuzulu?Maandamano ni leo au kesho?Nina wasisi kuna upotoshaji wa chini chini kwa lengo la kuhujumu maandamano haya.

Wahusika toeni taarifa ya kueleweka maana magazeti na mitandao yana taarifa tofauti tofauti.
 
Sikubaliani na wewe you're supposed 2 remember that "when i lost dis chance i will never get it again in ma life. Tambua kamanda aliye vitani aruhusu kurudi nyuma kwenye mapambano, pia usimpige nyani kwa mwangalia usoni.

Binafsi sitokuwa na msamaha pale nitakapoona makamanda wanarudi nyuma, kwani itanifanya nifirie mara mbili juu ya kuendele kuwamo kwenye kundi linalo jitanabaisha watetezi na wapiganaji wa haki ya mtanzania wakirudi nyuma.

Peopleeeeees..... CHADEMA 4malife. Pls cdm prove on me if am not wrong as what i belived
 
Hoja yako ni nzuri kaka. Ila lazima uelewe kuwa lengo la Serikali kuzuia maandamano si kwa sababu ya Ujio wa Rais wa China bali ni hofu na mfululizo wa ubabe na kutofuata sheria tu.

Rejea matukio ya kupinga maandamano ya chadema kwa kisingizio cha Sensa Iringa, Morogoro eti barabara ni ndogo, Maandamano na Mkutano wa JJ Mnyika eti kuna ukarabati wa barabara na Kiwanja cha Manzeshe ni parking ya magari. Arusha tunaambiwa eti CCM wamepanga maandamano siku hiyo. Rejea maandamano ya wanaharakati kupinga Dowans eti kuna tishio la Al-Shaabab hivyo hairihusiwi mikusanyiko na wakati kipindi hicho kulikuwa na mechi kubwa Uwanja wa Taifa na Mashabiki walihamasishwa kujitokeza kwa wingi.

Rejea Maandamano ya Madaktari ambapo Jeshi la polisi lilidai kuwa hayana tija kwa kuwa serikali imeunda kamati, pia kutakuwa na maandamano ya wananchi kupinga mgomo huo ambao nao watatumia njia hizohizo. Na kama Maandamano hayana tija kwa sababu ya Xi, mbona wananchi wamehamashishwa na wameandaliwa, tena wamepatiwa na bendera kumpokea Xi?.

NB: Lengo la Serikali ya Tanzania ni kupinga Maandamano ya Upinzani kwa sababu zozote zile, na kama tutasubiri kupata kibali za kuandamana kamwe hakitatokea.
 
"Some laws of state aimed at curbing crime are even more criminal" ni ukweli usiopingika wana jifanya wanasimamia sheria kumbe ndo wavunjifu wa sheria polisi wanaiba, ni majambawazi,wanaua raia,no one can stop us CDM! Peopleeeeee! power!
 
alipoulizwa itakuwaje maana kutakuwa na
ugeni wa rais wa china nchini, sababu
ambayo hata serikali imeitumia ili kuyazuia
maandamano hayo, mbowe alijibu:
"kilio chetu hakikuja na rais wa china, kama serikali ya ccm wanaona aibu
kumwajibisha waziri mmoja na naibu wake,
basi wasubiri aibu ya dunia kuona jinsi
tanzania inavyoendeshwa kibabe, ikiwa
haina elimu bora.

"tumetangaza maandamano wiki tatu
zilizopita, hatukuwa na taarifa na ujio wa
rais wa china, lakini jinsi mungu alivyo
upande wetu amemleta rais wa china,
kweli mungu ni mwema, hakuna tena nafasi
ya kusubiri kuficha ubovu katika sekta ya
elimu nchini, ndani ya siku ambayo
chadema waliandaa maandamano ili dunia nzima isikie kilio cha watanzania kuhusu elimu.

"sababu kuwa ccm nao wameandaa
maandamano kupinga maandamano ya
chadema hazina msingi ni kutowajibika
kwa jeshi la polisi. Hatukatazi maandamano, polisi wapange ratiba siku
tofauti, sisi tutaandamana kumpinga waziri
ili kama ccm wataandamana kumpongeza
waziri wao wapangiwe siku yao, ila sisi
tulitangaza mapema na barua tulipeleka
kwa mujibu wa sheria za nchi yetu."

mkuu, hope umeelewa. Kutoshiriki maandamano haya ni ubinafsi kwa wadogo zetu, ndugu zetu na elimu ya tanzania kwa ujumla

viva cdm,
tulianza na mungu, tutamaliza na mungu

naona sasa zamu ya mbowe kunyea debe imewadia. Chezea na polisi wewe. Ngoja aandamane hapo kesho aone nguvu ya vyombo vya dola
 
hoja yako ni nzuri kaka. Ila lazima uelewe kuwa lengo la serikali kuzuia maandamano si kwa sababu ya ujio wa rais wa china bali ni hofu na mfululizo wa ubabe na kutofuata sheria tu.

Rejea matukio ya kupinga maandamano ya chadema kwa kisingizio cha sensa iringa, morogoro eti barabara ni ndogo, maandamano na mkutano wa jj mnyika eti kuna ukarabati wa barabara na kiwanja cha manzeshe ni parking ya magari. Arusha tunaambiwa eti ccm wamepanga maandamano siku hiyo. Rejea maandamano ya wanaharakati kupinga dowans eti kuna tishio la al-shaabab hivyo hairihusiwi mikusanyiko na wakati kipindi hicho kulikuwa na mechi kubwa uwanja wa taifa na mashabiki walihamasishwa kujitokeza kwa wingi.

Rejea maandamano ya madaktari ambapo jeshi la polisi lilidai kuwa hayana tija kwa kuwa serikali imeunda kamati, pia kutakuwa na maandamano ya wananchi kupinga mgomo huo ambao nao watatumia njia hizohizo. Na kama maandamano hayana tija kwa sababu ya xi, mbona wananchi wamehamashishwa na wameandaliwa, tena wamepatiwa na bendera kumpokea xi?.

Nb: Lengo la serikali ya tanzania ni kupinga maandamano ya upinzani kwa sababu zozote zile, na kama tutasubiri kupata kibali za kuandamana kamwe hakitatokea.

kumbe yale maandamano ya madaktari yaliratibiwa na upinzani? Sasa nimeamini ile kauli ya slaa aliyosema kuwa watafanya kila jitihada ili nci isitawalike
 
naona sasa zamu ya mbowe kunyea debe imewadia. Chezea na polisi wewe. Ngoja aandamane hapo kesho aone nguvu ya vyombo vya dola

Kwa akili yako nguvu ya vyombo vya dola na nguvu ya umma ni ipi kubwa???TUMIA FIKRA SAHIHI.
 
mbona mengine walikua wanazungumza polisi ... hii imekaaje?
 
Sasa kama Maandamano ya CHADEMA yamepigwa marufuku kwa nini na hayo ya CCM yasipigwe marufuku?Yote si ni maandamano?Polisi watakuwa hawatendi haki.Kama kupiga mrufuku basi yote ya CCM na ya CHADEMA yote yawe marufuku sababu yote yatahatarisha uhai wa raia na mali zao.Polisi wawe-Fair
 
naona sasa zamu ya mbowe kunyea debe imewadia. Chezea na polisi wewe. Ngoja aandamane hapo kesho aone nguvu ya vyombo vya dola

NIngekuona wa maana kama ungepiga kelele mafisadi na wahujumu uchumi waende kunyea hilo debe.Vinginevyo rudi mtaani uone maisha ya kawaida ya vijana wenzako na uwe mzalendo.Uzalendo kwanza vyama baadaye.Elimu kwanza mengine baadaye
 
Back
Top Bottom