Pendaneni, acheni majungu na kufitiniana, chapeni kazi kwa bidii

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,285
7,854
Leo Mei mosi 2024, tunawatakia wafanyakazi wote wa Tanzania sikukuu njema.
Salam zetu kwao ni kwamba;

1. tunawaasa wawe na mahusiano mazuri kazini, wapendane, waache kuoneana wivu, waache kufitiniana/kuchongeana kwa maboss wao na kupigana majungu.

Majungu na fitina mahali pa kazi inapunguza ufanisi na tija.

Viongozi mlio teuliwa kuwasimamia walio chini yetu acheni kuendendeza majungu na fitina, unganisheni wafanyakazi wapendane.

Bango langu la leo kwa wafanyakazi ni;

WAFANYAKAZI ACHENI MAJUNGU NA FITINA MAHALI PA KAZI. PENDANENI.

Kazi iendelee.
 
Leo Mei mosi 2024, tunawatakia wafanyakazi wote wa Tanzania sikukuu njema.
Salam zetu kwao ni kwamba;

1. tunawaasa wawe na mahusiano mazuri kazini, wapendane, waache kuoneana wivu, waache kufitiniana/kuchongeana kwa maboss wao na kupigana majungu.

Majungu na fitina mahali pa kazi inapunguza ufanisi na tija.

Viongozi mlio teuliwa kuwasimamia walio vhini yetu acheni kuendendeza majungu na fitina, unganisheni wafanyakazi wapendane.

Kazi iendelee.
Ujumbe wako ni mzuri lakini kamwe haiwezekani kwa mtanzania.
 
Palipo na wafanyakazi wawili au zaidi majungu yapo kati kati yao
Hili ni tatizo kubwa sana sehemu za kazi.
Siku moja nimeenda ofisi moja kupata huduma nimekuta wafanyakazi wao kwa wao wanasemana vibaya tena mbele ya wateja bila kujali!!!!!
Hili lazima likemewe na viongozi.

Wafanyakazi wao kwa wao hawapendani, wanachuki na wivu!!!!
 
Ujumbe wako ni mzuri lakini kamwe haiwezekani kwa mtanzania.
Inawezekana endapo tu kiongozi anaye wasimamia walio chini yake hapendi majungu wala fitina.

Tatizo viongozi wengi waliopewa dhamana kuwasimamia wengine ndio vinara wa kuchochea majungu, kufitiniana na kuharibiana kazi.
 
Hili ni tatizo kubwa sana sehemu za kazi.
Siku moja nimeenda ofisi moja kupata huduma nimekuta wafanyakazi wao kwa wao wanasemana vibaya tena mbele ya wateja bila kujali!!!!!
Hili lazima likemewe na viongozi.

Wafanyakazi wao kwa wao hawapendani, wanachuki na wivu!!!!
Hao hao viongozi nao wakitulia majungu yanakuwepo. Tuseme labda kulinda heshima ya ofisi wasemane wakiwa free au wakiwa wenyewe bila wateja.
 
Fitna,majungu,chuki,wivu makazani kwa asilimia kubwa ndio imefanya hili taifa linazidi kuwa maskini.Hii ni kuanzia sekta binafsi hadi serikalini.
 
Fitna,majungu,chuki,wivu makazani kwa asilimia kubwa ndio imefanya hili taifa linazidi kuwa maskini.Hii ni kuanzia sekta binafsi hadi serikalini.
Hili ni tatizo ambalo limeota mizizi maofisini na haswa ofisi za Umma, majungu na fitina zimetawala mno!!! Mbaya zaidi viongozi wao pia wamo humohumo!!!

Tabia hizi lazima zikemewe na viongozi ili kuleta ufanisi na tija mahali pa kazi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom