wambura marwa
JF-Expert Member
- Mar 7, 2015
- 2,171
- 1,130
Kuna kitu kinafafahamika kama pembetatu ya upendo, mwanasaikolojia mmoja wa Kijerumani Robert sternberg, baada ya kutafakari sana, alibaini kwamba, kupenda au kupendana hakuwezi kuwa ngazi sawa.
Alibaini kwamba, kuna vipengele ambavyo kwa sifa zake vinaweza kuitwa kupenda, lakini vyenyewe kama vilivyo siyo kupenda. Alindelea kutafiti na kubaini kwamba, vipengele hivyo, vikiwa pamoja ndipo kupenda kunapokamilika. Lakini hata hivyo, anasema kwamba, ni wapenzi wachache sana wanaoweza kufikia hatua hiyo ya kutimiza vipengele vyote.
Mimi binafsi nakubaliana na mwanasaikolojia huyu, ingawa kuna mahali ambapo sikubaliani naye moja kwa moja, ambapo hata hivyo siyo mahali pengi sana. Anataja vipengele vikuu vitatu ambavyo anasema ndivyo vinavyoweza kwa pamoja kuunda upendo uliokamilika, usio na masharti. Anavitaja vipengele hivyo kuwa ni UKARIBU, MVUTO na KUJITOLEA.
Anasema mtaalamu huyu ambaye nadharia yake hii imekuwa msingi kwa wataalamu wengi wa saikolojia ambao wamejaribu kuelezea kupenda. Kwa kuchambua vipengele hivyo vitatu ameweza kupata aina saba za upendo. Mtaalamu huyu anasema kwamba, pale ambapo pana kipengele cha UKARIBU na MVUTO, aina ya upendo inayopatikana ni ile ya kimwili zaidi watu wawili wanaojiita wapenzi wanakuwa karibu na wana utana kimwili.
Hawa mara nyingi kama sio zote wamevutana zaidi kimwili. Ndiyo wale wapenzi ambao huwa tunawaona wakiwa wanafuatana kama kumbikumbi na nguvu yao iko kwenye kufanya tendo la ndoa na kufuatana kimwili. Linapotokea la kutokea kwa mmoja wao, mwingine hukimbia na kusimama mbali, hamjui tena mwenzake. Anapotokea kupata mwingine ambaye ni mzuri zaidi, humsahau huyu ambaye watu waliamini kwamba, hawezi kutengwa naye hata na kifo.
Aina ya pili ya upendo ni ile ambapo kuna kipengele kimoja tu kinachoushikilia, ambacho ni UKARIBU. Hapa ndipo pale ambapo watu wengine hubisha sana na kusema, hakuna mwanamke na mwanaume wanaoweza kuwa marafiki tu bila kushiriki mambo mengine. Hili linawezekana na hii ni aina ya urafiki ambao kipengele chake ni UKARIBU.
Watu wanakutana, wanazungumza, wanaenda mahali mbalimbali na kufanya shughuli mbalimbali. Urafiki huu hauna mashiko hata hivyo, kwa sababu ukaribu huo ukiondolewa na urafiki nao hakuna. Ni sawa na wanafunzi ambao hupendana sana, wakiwa shuleni na baada ya pale upendo hakuna.
Aina nyingine ya upendo ni ambayo imeshikiliwa na MVUTO na KUJITOLEA. Huu ni upendo wa hatari sana ambapo unakuta kijana anakutana na mshichana leo kwenye muziki kesho wametangaza uchumba na keshokutwa wameshaoana.
Kinachowaongoza hapa ni tamaa ya mwili, kumpenda mtu kwa sura na umbile tu na kuamua kuwa na mtu huyo au kujitolea. Kwa sababu, hapa hakuna ukaribu, hakuna kujuana, kabla ya uamuzi kufanywa, upendo huu huwa haudumu.
Aina nyingine ya upendo ni ile yenye kipengele cha MVUTO tu. Mtu anampenda fulani kwa sababu tu amemuvutia kimwili, kisura au kwa sifa za nje ambazo mara nyingi hupelekea watu kuingia kwenye mapenzi ya mwili. Uhusiano unaoshikiliwa na kipengele hiki, hutokea ukazaa upendo kamili badaye, kama wahusika watamudu kupata vipengele vingine viwili, yaani kujitolea na ukaribu.
Watu wengi huanza na aina hii ya uhusiano unamwona mwanamke au mwanaume roho inadunda kwa sababu amekuvutia kwa umbile au sura. Halafu unaingia kwenye uhusiano naye. Kama nilivyosema, inawezekana vipengele vingine vikaongezwa au hata kimoja. Inaposhindikana na kuishia hicho cha MVUTO, uhusiano huo huwa wa mashaka makubwa.Ndiyo unakuta wivu hauishi kinachoangaliwa ni ngono zaidi kuliko kitu kingine.