katika kuhangaikia uzima, Ndungu yangu mmoja amejikuta akielekezwa kwa Mganga wa jadi. amerejea ananieleza kuwa Mganga yupo Makini anatumia mizimu, kuna bibi na babu wanaongea kupitia kibuyu na pembe la ng'ombe. nimetafakari sana hii kitu, hivi Jamani haya mambo hapo kweli??..naona kama kuna utapeli..ila sijajua teknolojia gani inatumika hapo.
==============
update
imenilazimu kufuatilia kwa kina suala hili na tayari Mganga husika nishamtia mkononi. Ni Miongoni mwa matapeli nguli hapa mjini. Hakuna lolote ni udanganyifu tu. Naweka picha yake hapa ili mchukue tahadhali kubwa, kuna chain ya matapeli. Msishawishike na vibao vya matangazo ya waganga wa jadi mkiviona barabarani.