G-Mdadisi
Senior Member
- Feb 15, 2018
- 157
- 99
Mbunge wa Jimbo la Konde, Mohammed Said Issa 'Kiboribo' amesema ulaji wa samaki aina ya KASA ni jambo la kawaida kwa jamii ya visiwani licha ya samaki huyo kusababisha athari kwa walaji.
Ametoa kauli hiyo mapema leo November 28, alipofika Hospital ya Wilaya Micheweni kwaajili ya kuwafariji waathirika waliolazwa katika hospitali hiyo baada ya kula samaki huyo anaedaiwa kuwa na sumu katika Shehia ya Msuka wilayani hapo na kupelekea vifo.
Amesema licha ya samaki huyo kusababisha madhara kwa wananchi hasa vifo lakini ameipongeza serikali kwa kufanikiwa kulishughulikia bila taharuki zaidi kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma.
VIDEO:
Mapema leo mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib amesema mpaka kufikia leo asubuhi vifo vimefikia 6 huku jumla ya waliofikishwa hospitalini hapo wakiwa ni wananchi 63 kwaajili ya kutanyiwa uchunguzi ili sumu hiyo isiendelee kuwaathiri.