Pemba - Je mtawaunga mkono kuikoromea CCM na Njama Zake ?

Haya mambo yanashangaza kabisa. Hivi kweli kama Seif ana wafuasi wa kutosha Pemba, Kwa nini anafanya fujo, haachi zoezi hilo likaendelea kama lilivyopangwa? Na jee ana hofu gani wakti Pemba ndiyo ngome yake? mwaka huu tutajua la kweli!!

Jawabu lako analo kikwete,alipokuja znz alisema atayalinda mapinduzi kwa njia yoyote na gharama yoyote na atakaechezea atakiona.
 
Bila ya MUUNGANO, Zanzibar ni NCHI? Au Jamhuri ya Pemba( na Rais wao wa maisha Maalim Seif) na SMZ ya Waunguja?
 
Kama unafuatilia uandikishaji wapiga kura kule Pemba utaona kile marehemu Mwalimu Nyerere alichosema kwamba kitu kinachowaunganisha Wazanzibari ni Muungano. Nje ya Muungano kuna wao Waunguja sisi Wapemba. Wao CCM sisi CUF. Na kwenye suala la kupatikana mafuta kule Permba wanasema sisi Wazanzibari wao Watanganyika. Mafuta yetu hatuyataki kwenye muungano. Lakini mzigo mzito wa kulipa kodi ya kuendesha serikali ya Muungano unabebeshwa Mtanganyika/Mnyamwezi.

Taratibu unapomtaja Mwalimu Nyerere, Ukiangalia kwa undani wanaowapiga na kuwaua WaPemba kama ngedere ni majeshi na mapolisi kutoka bara kati yao Wazanzibari ni wachache sana.

Nembo inayotumika katika utekelezaji wa kulinda wizi wa CCM ni ya Jeshi la polisi na usalama wa Taifa.

Sasa la kujifunza kutoka katika unyama huu ni kuwa haya mambo yanayofanyiwa WaPemba ni ya nini ,au tuseme yamesababishwa na nini ?

Je hizo sababu zinaweza kupatikana sehemu yeyote ile hapa Tanzania au tuseme Tanganyika ?

Sasa ikiwa sababu hizo zitapatikana kwa wingi upande wa Tanganyika ,Je CCM watashindwa kutumia na kufanya kile wanachofanya Pemba ?

Mchezo huu unaofanywa na CCM ni mikakati ya kupata ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao ,je huko Tanganyika hakuna wapinzani wa kuitikisa CCM kama wananchi wa Pemba ?

Je tuamini kuwa vyama vya upinzani kwa upande wa Tanganyika vyote vipo na kuilinda CCM kwa kuwadanganya wananchi wake kiasi ya kwamba hawawezi kujumuika katika kupinga wanayofanyiwa WaPemba ?

Yaliyofanywa Mbeya katika uchaguzi mdogo hayana tofauti na yaliyofanywa Zanzibar katika uchaguzi mkuu uliopita ,sasa fahamuni kwamba kinachofanywa Pemba kitafanywa na huko Tanganyika vilevile ,hivyo basi kama haya yanayofanywa leo hayakupigiwa makelele na kukomeshwa ,mnafikiri mtaweza kuyazuia yakianza kuelekezwa na huko ?

Kusema kweli WaPemba wanajitahidi sana sana katika kupinga na kujaribu kuzizuia hila za CCM kwa kila kitu chao zikiwemo roho zao pia ,yaani wapo tayari kufa lakini wasidhulumiwe katika haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Kuna hatari huko Tanganyika wakasema kuwa nyote si raia na muonyeshe stakabadhi za kulipia kodi au ushahidi kama mliwahi kuomba uraia.
Je mnao ushahidi kama nyinyi ni WaTanzania ?
 
Back
Top Bottom