Pemba - Je mtawaunga mkono kuikoromea CCM na Njama Zake ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pemba - Je mtawaunga mkono kuikoromea CCM na Njama Zake ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Sep 13, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Pemba kwachafuka
  • Askari wapigwa mawe, Maalim Seif atuhumiwa


  na Mwandishi Wetu, Pemba
  HALI ya amani kisiwani Pemba si shwari, baada ya jana kuibuka vurugu kubwa zilizosababisha nyumba ya sheha kuchomwa moto, polisi kurushiwa mawe na watu saba kukamatwa, kwa madai ya kuwazuia watu kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

  Vurugu hizo zimetokea baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuanza zoezi hilo ililolisimamisha mwezi uliopita kutokana na kuwapo kwa vurugu zilizosababishwa na baadhi ya watu wanaodai mizengwe kutawala katika uandikishaji wa watu kwenye daftari hilo.

  Mamia ya watu walijitokeza katika vituo vya uandikishaji wapiga kura, lakini hawakusogea kwa makarani kuandikishwa, huku wengine wakipambana na polisi kwa matusi na kurushiana mawe walipotakiwa waondoke vituoni kama hawakuwa tayari kujiandikisha.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Yahya Rashid Hemed, alilazimika kufika katika kituo cha Kiuyu, Minungwini na askari wa ziada wapatao 20 wenye silaha na mabomu ya machozi kuungana na askari wapatao 50 wa polisi, KMKM, Magereza na Usalama wa Taifa, ambao walionekana kushindwa kuidhibiti hali.

  Polisi walipojaribu kutumia nguvu na kutisha watu kwa mtutu wa bunduki, ndipo wananchi walipoanza kurusha mawe, ambapo Kamanda Yahya, alilazimika kufanya kazi ya ziada kutuliza jazba za wananchi.

  Vurugu hizo kwa kiasi kikubwa zimetokana na baadhi ya wananchi kudai kuwa wengi wao hawana vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi, ambavyo ndivyo vinavyotumika kama kigezo cha kuandikishwa.

  Hali ya vurugu ilianza kujitokeza katika vituo vya uandikishaji vya Kambini na Minungwini katika Jimbo la Ole, ambapo wanachama wa CCM walipokuwa wakijaribu kwenda katika vituo vya kuandikishwa, makundi ya watu yaliyokuwa karibu na vituo yalionekana kupinga na kusababisha zoezi hilo kutokwenda vizuri.

  Askari polisi na wa Kikosi cha Kujenga Uchumi (JKU) walionekana kuimarisha ulinzi katika kituo cha uandikishaji Kambini, lakini ulinzi huo haukusaidia kitu, baada ya wananchi wenye jazba kuzuia kazi hiyo ya uandikishaji.

  Kutokana na hali kuwa tete, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi, alifika katika eneo hilo na kuwataka wananchi kuacha jazba ili watoe nafasi kwa wananchi wenye sifa kujitokeza kuandikishwa.

  Akizungumza katika eneo hilo, Dadi aliwataka wananchi hao kuacha kuchukua sheria mikononi na kuwasihi wasio na vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi kufuatilia katika maeneo husika.

  Kabla ya kuanza kwa vurugu hizo, usiku wa kuamkia jana nyumba ya Sheha wa Kangagani, Faki Omar Yusuf, imechomwa moto na watu wasiojulikana, huku yeye na familia yake wakinusurika baada ya kuwahi kutoka nje.

  Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman, aliyekuwapo katika kituo cha Minungwini, alisema vurugu hizo na watu kugoma zinatokana na uhamasishaji uliofanywa na viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), hasa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

  Alisema Maalim Seif anajua hawezi kushinda katika uchaguzi mkuu ujao na ule wa serikali za mitaa, kwa kuwa hana wafuasi wa kutosha visiwani Pemba, ndiyo maana amefanya mipango ya kuchafua zoezi la uandikishaji wapiga kura.

  Katika vurugu hizo, Ali Makame, Makame Mcha, Ame Mtwana Juma, Ali Jafar Haji na Suluhu Ame, walikamatwa na askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) katika vituo vya uandikishaji vya Fukuchani na Nungwi shuleni.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mselem Masoud Mtuliya, alisema tatizo lililojitokeza linaonekana kukosekana elimu ya kutosha ya uraia kwa wananchi.

  Alisema kwamba watu wengi walikuwa hawalifahamu zoezi hilo, kwa vile wengi waliojitokeza ni waliotaka kubadilisha vitambulisho vya kura, wakati walitakiwa ambao wametimiza umri wa kuandikishwa wa miaka 18.

  Mzee Saleh Mohamed Salim (58) wa Kityu alisema mwaka huu Wapemba wameamua kukataa kutii amri zinazowakandamiza na kuwadhalilisha na wanataka ulimwengu utambue kuwa na wao ni watu wenye kuthamini utu wao na haki zao.

  Siti Ali Hamad (83) , alisema wamekusudia kukomesha wizi wa kura, hila na mizengwe inayofanywa na serikali inayoongozwa na CCM kila unapofika wakati wa uchaguzi, hivyo safari hii wameamua kudai haki ya kupiga kura kwa gharama yoyote ile.

  “Mwaka 2001 tulizika watoto wetu walioandamana kudai haki, sasa tupo tayari kujitolea roho zetu ili wajukuu wetu wapate haki, lakini si kukubali kuendelea kuburutwa,” alisema Siti.

  Said Mbaruk, alisema yeye ni mtetezi wa haki za vijana, anasikitishwa kuona askari walijazwa vituoni kwa lengo la kuwatisha raia ili wasiweze kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishwaji.

  “Nilikuwa ninapigania haki na nitaendelea kuwapo hapa kusisitiza vijana wapiganie haki mpaka zijulikane mbichi na mbivu, tumetishwa sana, tumepigwa sana na hakuna kinachotutisha katika kudai haki zetu, hatuui, tunachotaka ni kupewa haki ya kupiga kura,” alisema Said.

  Ole Saleh Mohammed Salim (58), alipinga kauli iliyotolewa na Mkurugenzi wa Vitambulisho, Mohammed Juma Ame, kuwa wametoa vitambulisho 155,561 kisiwani Pemba.

  “Labda vitambulisho hivyo vimegawiwa Giningi (makao makuu ya wanga vibwengo). Sisi hatuna na hawataki kutupa, lakini tutaendelea kuvidai, kwa vile ni haki yetu. Tunachotaka ni kupiga kura,” alisema Salim.

  Naye Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Bimani, alisema sakata hilo la wananchi kukosa vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi ni mpango maalumu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na CCM, wenye nia ya kuwanyima haki ya kikatiba wananchi ili kuwezesha CCM kushinda kwa ujanja ujanja.

  Hivi karibuni Jumuiya ya Ulaya (EU), Marekani, Canada na Japan zilitoa tahadhari kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika zoezi la uandishaji wa watu katika daftari la kudumu la wapiga kura.

  Tahadhari hiyo ilipingwa vikali na Umoja
   
 2. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Abaa swala lako halitopata jibu na thread yako itasomwa lakini hakuna atayewaunga mkono Wapemba la muhimu wapemba walioko kule wameshalijua hilo na hawamtegemei mtu wanachosema ni kuwa uchaguzi ujao kama watapigwa na wao wanaingia majumbani. Kwa hivyo humu lete mada ambazo zinapendwa na wengi lakini sio za kuuliza kama wapemba wataungwa mkono kwani hilo ni nadra katika forum yetu hii wao na Maalim Seif kila wakati wanaonekana ni wakorofi tu.
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huko Pemba kuna mambo! Na hii staili mpya ya kutegesheana mizinga ya nyuki imekaaje?

   
 4. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mizinga ya nyuki tukiizoea tutaleta mizinga ya nyukl.a!!!!:mad:
   
 5. C

  Calipso JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sijui wewe unatoka burundi,yaani si mtanzania? WaTz wenzako wanateswa na kunyimwa haki yao wewe unafurahia... Omba yasije kukufika..
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mola inusuru Pemba.
   
 7. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haya mambo yanashangaza kabisa. Hivi kweli kama Seif ana wafuasi wa kutosha Pemba, Kwa nini anafanya fujo, haachi zoezi hilo likaendelea kama lilivyopangwa? Na jee ana hofu gani wakti Pemba ndiyo ngome yake? mwaka huu tutajua la kweli!!
   
 8. C

  Calipso JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu tmechanga pesa mimi na wewe lkn zako nyingi kuliko zangu,imefika siku tumesema tugawane,mimi nakwambia zangu ndio pesa nyingi... UTAKUBALI?
  Sasa hiyo ndio inafanyika Pemba,CCM wanajua Pemba hawapati kabisa,la kufanya ni kuwakatalia wapemba wasiandikishwe ili wao waandikishe watu wao, Nani atakubali? La kushangaza unaambiwa watu waliokuwa washaandikishwa ni laki moja na hamsini na kidogo,wametokea wapi wakati wapemba wenyewe mpaka hivi sasa hawajaandikishwa,yaani Daftari limeshiba hata chakula bado...
   
 9. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli!!!!

  Sasa nani anasema ukweli? Jambo moja liko bayana HIYO PEMBA NI YENU. MNAO WAJIBU WA KUHIFADHI AMANI. KWA STAHILI HII HAMFIKI. HAPA AWE CUF, CCM, AU NANI NI BORA MUIANGALIE PEMBA YENU IWE YA AMANI MAMBO MENGINE YATAFUATA.
   
 10. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sifurahii lakini ukweli unabaki kuwa pale pale kuwa hakuna atayewaunga mkono Wapemba na mateso ya CCM kwa kuitumia SMZ na ushahidi wa hayo angalia michango ilotolewa yote kama kuna hata mmoja unao oonyesha kinyume na niliyoyasema.
   
 11. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kuna mambo mengi yanashangaza hususan katika serekali ya zanzibar juzi hizi Rais kikwete alisema kuwa mafuta yalipokuwa hayajapatikana yalikuwa yapamoja sasa yameshakuwepo si yamungano tena inawashanga hata hao inaowaweka madarakani serekali lakini hawa jamaa wa Tanganyika na wapongeza kwa elimu yao na akili zao zinavyofanya kazi kwani hivi sasa inawaridhia tu SMZ huki ikijuwa baada ya mika michache jeuri yao itamalizika na wanachokitaka kama alivyosema waziri mkuu punda anatamani siku moja kuwe na nchi moja tu naserekali yake moja,serelkali ya SMZ ya hivi sasa ni sawa na mtu aliyewekewa lifu sapoti mashine .
   
  Last edited: Sep 15, 2009
 12. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu unajuwa kwanini hakuna anaewaunga mkono kutokana na mateso ya CCM ?hii inatokana na sumu ya CCM ilivyokuwa kali kw hapa kwetu zanzibar tunaita kilizoni hiyo ukinywa ndio safari tu hakuna msalie mtume ,kunawakati wa uchaguzi mwaka 05 Jumaduni alikuwa katika mkoa mmoja kule bara akawambia wananchi wa sehemu ile kuwa CCM ni kama Ulevi (pombe)ukinywa katika chomo chochotekile hata katika jani na mgomba basi utalewa tu (utapombeka)na ndio yanayowakuta wengi humu ndani ya jamii forum .
   
 13. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mungu Saidia mambo ya Pemba yaishe kwa Amani!! Maana naona watu wote wameamua kuona na kuacha mambo yaende kama yalivyo
   
 14. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  where democracy can not be done, revolution is the best way.
   
 15. w

  wasp JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama unafuatilia uandikishaji wapiga kura kule Pemba utaona kile marehemu Mwalimu Nyerere alichosema kwamba kitu kinachowaunganisha Wazanzibari ni Muungano. Nje ya Muungano kuna wao Waunguja sisi Wapemba. Wao CCM sisi CUF. Na kwenye suala la kupatikana mafuta kule Permba wanasema sisi Wazanzibari wao Watanganyika. Mafuta yetu hatuyataki kwenye muungano. Lakini mzigo mzito wa kulipa kodi ya kuendesha serikali ya Muungano unabebeshwa Mtanganyika/Mnyamwezi.
   
 16. w

  wasp JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM inataka kuifanya Pemba kuwa Daafur ya Tanzania. Unaweza kumchukua mbuzi kwa kamba mpaka mtoni. Lakini huwezi kumlazimisha anywe maji. I guess Zanzibar is slowly turning into a failed government over Pemba island.
   
 17. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pakacha, SMZ imeharibu mambo yenyewe kila mwaka inakuja na mbinu mpya za kuiba uchaguzi, marahii suala la vitambulsho limewageukia wenyewe wache wauwe waone watakapoishia. Poleni Pakacha maana mwisho wa utawala wa kibabe ni fedheha ndo historia ya ulimwengu ilivyo.
   
 18. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mafuta yetu hatuyataki kwenye muungano. Lakini mzigo mzito wa kulipa kodi ya kuendesha serikali ya Muungano unabebeshwa Mtanganyika/Mnyamwezi.[/QUOTE]

  Tuseme hizi ndio sababu za kutowaunga mkono?
   
 19. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Sasa wamekuja na style mpya ya Upupu, hivi kweli watu wamekosa agenda ya kisiasa hadi kuanzisha hivi vijifurugu mtoto?

  Upupu wahamisha kituo cha uandikishaji
  Na Mwinyi Sadallah
  18th September 2009

  Kituo cha uandikishaji Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, kimelazimika kuhamishwa baada ya watu wasiofahamika kumwaga upupu katika chumba cha uandikishaji na kuwaathiri maafisa wa kituo hicho.
  Kitendo hicho kilijulikana muda mfupi baada ya makarani wa uandikishaji kufika katika eneo hilo juzi na kuanza kujitayarisha na kazi ya kuandikisha wananchi waliokuwa wamejitokeza.
  Baada ya kubainika kuwa chumba hicho kimemwagiwa upupu, maafisa wa uandikishaji waliamua kuhamisha kituo hicho na kuhamishia chumba kingine cha jengo la shule hiyo.
  Msimamizi wa kituo cha uandikishaji cha Nungwi, Jabir Haji, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema jengo hilo lilibainika kuwa limemwagiwa upupu m baada ya makarani kufika na kujiandaa kuanza kazi. Tukio hilo ni la pili kutokea tangu kuanza tena zoezi la uandikishaji Septemba 12, baada ya watu wasiofahamika wiki iliyopita kumwaga upupu katika kituo cha uandikishaji cha Kigunda.
  Aidha, matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza katika vituo vya uandikishaji kisiwani Pemba, ikiwemo kutegwa mizinga ya nyuki, pamoja na kafara za kuchinja kuku na kutelekezwa katika vituo kwa malengo ya kuwadhuru makarani wa uandikishaji.


  CHANZO: NIPASHE
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kikwete upo wapi kushughulikia mtafaruku huu.
   
Loading...