Pele amshauri Neymar kuhamia Real Madrid!

Achraf Hakimi

JF-Expert Member
Mar 3, 2010
875
1,779
Staa wa zamani wa Brazil, Pele amemwambia mchezaji wa Santos (Neymar) kuwa kuhamia kwake Real Madrid kutakuwa na manufaa kwa mchezaji huyo
127253_news.jpg



"Kwenda pale Real Madrid si kuhusu pesa, ila rais wa klabu ya Santos anatakiwa kukubali kumuuza Neymar, hataki kumuuza Neymar mpaka mashindano ya kombe la dunia 2014 yamalizike, ila namshauri Neymar ahamie Madrid" Pele aliwaambia waandishi wa habari.

Neymar mwenye umri wa miaka 19, ni mmojawapo ya wachezaji mashuhuri wanaotamba duniani kwa sasa na ana nguvu kubwa ya kuhamia Madrid katika kipindi hiki cha usajili.

Msimu ulipita ilibakia kidogo tu kwa mchezaji huyu kuhamia Chelsea, ila aliamua kubakia Santos, na Pele anasema kuwa mchezaji huyu alifanya jambo sahihi kwa kutohamia ligi kuu ya England. "Neymar yupo kwenye hali nzuri ya kucheza ligi kuu ya Spain (La Liga) kutokana na uwezo wake na aina ya uchezaji wake uwanjani" Pele alisema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom