Pd Karugendo: Kwanini waliitaka sauti yangu?

Hivi jamani naomba mnisaidie, haya maneno kama shenzi, pumbavu, mjinga, baradhuri na mengineyo mfano wa hayo hua hayana mahala stahili pa kutumika?

Kama hakuna kwa nini bado yanaitwa eti maneno sanifu na bado yamo kwenye kamusi?

Kama papo mahala sahihi mbona yakitumika watu wanakuja juu sana?

Mtazamo wangu
Tufute maneno yote ambayo wataalam wanadai hutakiwi kuyatamka eti kisa ni makali na badala yake tuunde tamathali za semi nyingi ili kuepusha vigugumizi.
 

Ndiyo Karugedo ni vizuri kumtetea jirani yetu wa Ibwera Bukoba.Wasilete zao bana hawa C.M
 
hata yesu ilipobidi aliwafundisha watu kwa kuwaita enyi kizazi cha uzinzi mbona mna mioyo migumu?? sioni kosa la padri kuwaita wapumbavu jina hilo
 
Upumbavu na ujinga hauishii kwa hao vijana tuu,unakwenda mbali zaidi. Hebu fikirieni kiongozi wa hadhi ya kitaifa katika chama tena chama kinachotawala ana andamana na vijana wa aina hiyo katika ziara zake mikoani kwa gharama za chama ili tuu hao vijana wamsaidie kueneza uzandiki na upuuzi kwa jamii iliyojichokea kwa matatizo, na inahitaji zaidi kusikia mbinu za kuondokana na umasikini wao zaidi ya propaganda za kipuuzi zisizo tija.
Kiongozi/ viongozi wa aina hiyo huu ujumbe wa Karugendo unawahusa kwa kiasi kikubwa zaidi.
 
Ila? We unadhani kwanini hajapeleka sauti huko kwa wanafunzi wa Uandishi feki?Nadhani hajaruhusu kupeleka sauti kwa sababu ya kutokua na uhakika na hao vijana kutoka st.augustine!
 
Punguza jaziba padri hata kama hukutaja majina lakini sio vizuri kusema vijana wapumbavu tafadhari tumia lugha mbadala kufikisha ujumbe.

unatatizo gani wewe?padri katoa hoja wewe unashambulia mtu?kwani mpumbavu ni tusi?hata kama kakulenga usingeonesha kukerwa kako kwa kumshambulia mtu na ndiyo mana ametumia hilo neno..sasa ebu sema ukweli kama wewe si mpumbavu?ni mpumbavu tu..coz umeacha ukweli unakimbilia upumbavu huku ukiujua uhalisia..ni mpumbavu tu wewe.
 
Vijana hawa wameamua kuwasaliti na kuwauza wazazi wao,kaka,dada na binamu zao ..hakika Mungu anajua cha kuwalipa.
 
Natumaini kuwa Pasco naye ataisoma makala hii. Yeye alitaka kutuaminisha, kwa kusisitiza kila anapopata nafasi, kuwa ile tape ya Lwakatare ni "authentic," kama anavyosema mwenyewe
.
Mkuu Jasusi, nimeisoma makala na kuielewa!, japo siijua profesional rasmi ya Padri Privatus Karugendo, ila ni mimi ndie niliyeisimami makala fulani kwenye Gazeti la Mtanzania, kutoka kwa Askofu aliyemfuta sacrament ya upadirisho huyu Padri Karugendo kutoka na kwenda kinyume cha mafundisho ya Ukatoliki kwa maneno na matendo, ndio maana mmemshuhudia anavyitushuhudia humu kuwa watu fulani, hawawezi kupanga kufanya jambo fulani!.

Nasema salini na kuomba watu wasiconfess, vinginevyo watu kama kina Karugendo, watatafuta pa kutokea!.
Kuna watu wanaabudu watu, na nikasema hata shetani mwanzo alikuwa malaika!, na kuna watu mpaka kesho, wanamtumikia shetani disguised as God, wakijua wanamtumikia Mungu!, kumbe wanamtumikia Shetani, bila wao kujijua!. Kuna watu hawana moral authority kuzungumzia baadhi ya issues za morality za wenzao!.

With 15 years kwenye AV Production, naweza kabisa kutumika kama "amicus curiae" kwenye determination ya authenticity ya ile video kuwa "bonafide genuine!". Ila genuinity yake sio determinant ya "admissibility as evidence" before the court of law!.

Ila pia la rushwa kwenye media, nimeisha lizungumza sana hapa!-Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa ...

Pasco.
 
hata siku hizi Yuda iskarioti bado wako wanatanga tanga duniani kwa gharama ya 50,000 tshs wanakuuza jumla jumla
 
I can see the correlation kati yake na Dr. Slaa. WANAWAKE NA MATATIZO YA NDOA. Haishangazi kuona anamtetea sana.

Halafu huyu jamaa katika mada zake nyingi, yeye sana sana hugusia wanawake au ngono. Ninafikiri ana kaugonjwa fulani. Siyo ajabu hata Upadri ulinyea njia kwa sababu ya mada za ngono.

Hawa ndiyo dizaini ya tunaosikia wanawambia waumini wao kuwa, kutokuwa na mahusiano na Israel ni laana kwa Tanzania.

Hata ICC kuna Mapadre wanaokabiliwa na mashitaka. Kanisa pia lina mapadre walioacha njia na kufanya vitendo vya kishetani (Kulawiti).

Point yangu ni kwamba, siyo kila wanaoitwa Mapadre ni Mapadre katika macho ya Mungu. Shetani anakuja na sura nyingi.

I'm sorry kwa watu waliokuwa wanakwenda kutubu mbele yake. Moja ya article zake kipande chake hiki hapa chini,
 
Kweli jamiiforums imeingiliwa siku hizi. Wewe ferre au ---- hivi hata kusoma hujui? Mimi nimesema kwa mtazamo wangu na kwa nafasi ya padri katika jamii sijamshambulia mtu. Na najua wewe ukiitwa mpumbavu na mtu lazima utachukia. Hivyo ndio pumbavu ni tusi kama hutaki ni msimamo wako lakini siku nyingine usilushe ngumi ukiitwa hivyo. Na suala la kuguswa mimi kama kijana ni kweli limenigusa maana naamini kusikia matamshi mbadala kutoka kwa mapadri wa kanisa nalo sali kila jumapili sio kuita watu wapumbavu. Wakati tunafundiswa na hao mapadri kuepukana na chuki kwa watu wote.
 
Punguza jaziba padri hata kama hukutaja majina lakini sio vizuri kusema vijana wapumbavu tafadhari tumia lugha mbadala kufikisha ujumbe.
'Vijana wapumbavu'? Hiyo phrase sijaiona kwenye hii makala ya Padri. Nimesoma neno baada ya neno na kurudia mara kadhaa bado sijaliona. Nakaamua kutumia MS word kulitafuta neno wapumbavu kwenye makala hii lakn hata hivo sikulipata. Ninachoweza kusema hilo neno umelizua mwenyewe, nakujitukana au kuwatukana mwenyewe hao vijana aliwamaanisha Padri kuwa ni WAPUMBAVU. Nami nakuunga mkono kuwa hao vijana ni wapumbavu.
 
Makala nzuri, sijui mtu kama Mwigulu anasomaga vitu kama hivi.

Mwigulu Machemba asome makala makini namna hii!!! Huo muda atautoa wapi!? Yeye ni never miss magazeti ya udaku ya shigongo ya Ijumaa, n.k.
 
.
With 15 years kwenye AV Production, naweza kabisa kutumika kama "amicus curiae" kwenye determination ya authenticity ya ile video kuwa "bonafide genuine!".
Pasco.
AV production, 15 yrs ago, enzi za analogia, mambo digitali siku hizi bana!.
 
Well said, Pd. Karugendo. Taifa limekosa mwelekeo tena kipindi cha miaka 8 sasa. Awamu ya nne imekuwa ya kipuuzi, dhaifu na upeo mdogo sana kifikra, kidira na hata kiuongozi. Awamu hii imetufikisha hapa tulipo! Tanzania ya kichekesho! Tanzania inayowaza nani achinje ng'ombe! Tanzania inayopewa meli ya kisasa ya uvuvi na mahakama baada ya kuitaifisha kutokana na uvuvi haramu lakini inaiacha meli hiyo izame! Taifa lenye naibu waziri wa elimu mwenye elimu tata! Taifa ........... (jaza mwenyewe upuuzi mwingi tunaoushuhudia). Je tutafika?
 
Ni kweli mkuu katumia neno ushenzi. Kwangu mimi na wewe tukisema ni washenzi au wapumbavu haitakua na nguvu kama akisema padri. Na ukitaka kujua kakosea angalia hata suala la udini. Ilibidi aimbe samahani na kutaja sababu sio ahanze kuongelea mazao Kalima mkiristo basi waislam wasile. Haikua na haja ya yote hayo. Anyway ushenzi ni tusi sio vizuri kutumiwa na kiongozi wa dini ndo msimamo wangu
 
AV production, 15 yrs ago, enzi za analogia, mambo digitali siku hizi bana!.
Mkuu Isotope, ni kweli, enzi hizo, tulikuwa na Analogue! lakini mimi Pasco wa jf, nimeingia rasmi TV Newsroom, 1995 nikiwa na Digital Camera yangu sony (personal) na ipo mpaka leo as achieve!. Wakati huo TV zetu zote analogue, nilikuwa nikitumia DV yangu na kuhamisha picha kurudi Aanalogue kwa AV cable!.

Inawezekana mimi ndie VJ (Video Journalst) wa kwanza Tanzania, na kutokana na uwezo wa kupiga picha na kuandika habari, nimekula trips kibao, ikiwemo 4 trips kuripoti UN GA from New York!.

Mwaka fulani nilikamatwa Zanzibar na DV Camera yangu ikazuiliwa na polisi pale Mwembe Madema, ikapelekwa TV wakatoe mkanda kuungalia, by that time, natumia Mini DV ya HD ina save kwenye hard Disc, TVZ hawana hili wala lile, nikafuatwa polisi, nikawatolee mkanda wao wameshindwa!, nilipofika nikasema hii camera haitumii mkanda, na sio video bali ni ya still photo. Nika swich upande wa memory card, nikawaonyesha picha za still, wakajiridhisha kuwa sikupiga picha, nikasindikizwa under escort mpaka bandarini na kutimuliwa!, kufika Dar, kwenye news ya Saa 1:00 usiku, DTV ikaibuka na breaking news ya machafuko ya Zanzibar with video footage!. Hata ile seke seke ya Mwembe Chai, aliyei breaki ni mimi na zile picha nilipiga mimi!. Kitendo cha kumaliza JKT nikaunganisha na JWTZ na ndipo nikaingia Nwesroom kilinifanya niwe kama mjeshi fulani!.

DV kwa TV za Tanzania imeletwa na TBC, enzi hizo TVT, na kwa sasa technology imehamia HD, sisi Tanzania bado tuko kwenye DV, ile mimi kupitia Studio yangu ya PPR, siku nyingi nimeisha hamia kwenye HD nikitumia XD Card camera za Sony, ila bado nalazimika ku export kwa DV kwa sababu mitambo ya TBC ikiplay HD, picha inaonekana kama ina over exposure!.

Ile video ni "bonafide genuine!" kama kuna mengine na tuyasubirie!.

Pasco.
 

Kama "pumbavu" ni tusi basi ni tusi kwa mtu yeyote yule atakayetamka, iwe padri au teja, ukisema eti Padri kwa nafasi yake "hakupaswa" utakuwa unakosea, YESU mwenyewe alimuita Herode "mbweha" baada ya kuzidisha upumbavu ndo sembuse Padri,Kuwa kiongozi unapaswa kusema ukweli ikiwapo kuwaita wapumbavu WAPUMBAVU na sio kumridhisha kila mtu kwa maneno matamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…