Nataraji mko poa waungwana..
Ki ukweli mimi ni mmoja kati ya watu ambao nikitokewa na kitu kizuri ama kibaya maishani huwa kwanza natafakari kujua ni malipo ya kitu gani nilichokifanya siku za nyuma.
Na pia km watu wengi walivyo wepesi kukumbuka mambo mema waliyoyafanya na kusema "Mungu amewalipia ila ni wachache wanaokumbuka mabaya waliyofanya na kusema "Mungu amewalipa"
Ki ukweli hata post nyingi za malalmiko ya kupatwa ns mambo mabaya zinazojazwa humu ndani ni malipo ya mambo mabaya ambayo watu waliyafanya huko zamani..na naamini ni fair km tungeheshimu "payback" na kuwa wawazi zaidi na labda pia kuandika na vitu vibaya tulivyovifanya huko nyuma na malipo yake yaliyotupata..
Ahsanteni sana wana M.M.U