Paulo Makonda acha tamaa ya uongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Paulo Makonda acha tamaa ya uongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkatangara, Sep 30, 2012.

 1. m

  mkatangara Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijafurahishwa na taarifa ya huyu mtu anayeitwa Paulo Makonda kukasimisha nafasi yake kwa makamu mwenyekiti tahlso bwn. Abubakar Mohamed toka Zanzibar huku yeye akijikita na siasa za kuwania kiti cha umakamu uenyekiti UVCCM Taifa, na kwamba eti akishinda nafasi yake hiyo ya huko UVCCM ndio ataachia ngazi nafasi yake hiyo na kwamba akishindwa atarudi kuendelea na nafasi yake.

  Mi nadhani kama katiba ya tahiliso haijatoa maelezo ya situation kama hii ilivyo nadhani ingekuwa busara kama Paulo Makonda aiachie hiyo nafasi ya uenyekiti wa tahiliso na uchaguzi ufanyike nafasi hiyo ijazwe na yeye kama amechagua kufanya siasa auende huko kwenye siasa zake za UVCCM akishinda ni kheri yake akishindwa asirudi tena tahiliso.
   
 2. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  kofia mbili ndio sera ya magamba.
   
 3. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Anachezea karata zake vizuri. Unataka akose kotekote??
   
 4. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  kofia mbili ndio sera ya magamba. Na ninyi wasomi wa kisasa sijui ni haya mafuta ya siku hizi ndio yamepunguza uwezo wenu wa kufikiri au sijui ni njaa? ilikuwaje mkachagua kiongozi ambae hajiamini kama huyu? ona sasa hajiamini hata nafasi anayogombea kama tashinda au la, ndio maana anashindwa kujiuzuru.
   
 5. P

  Pilitoni JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 1,001
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Paul makonda ni jembe na hilo liko wazi
   
 6. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hizi ndio siasa uchwara za c c m
  by rostam
   
 7. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  angekuwa jembe asingefanya anayofanya, labda ni jembe kwako, angekuwa jembe angekuwa na uhakika wa ushindi na angeachia cheo hicho cha uenyekiti wa tahliso, tahliso hakuna kitu tena umebaki kuwa umoja mwingine wa uvccm, viongozi wa ukweli walikuwa wakina silinde, wawa stephene na machibya kwani ndio waliogundua mbinu hizi za ccm za kuongezea tahliso kuwa tawi lao na wakaamua kuitoa udsm katika umoja huo, nikiwakumbuka viongozi hawa huwa napata ujasiri sana wakufanya maamuzi magumu kwani bila wao tusingejua mbinu hizi za ccm kuiingilia tahliso kuanzia ule mwaka wa 2008 mpaka leo
   
 8. m

  mkatangara Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa kuhusiana na kitendo cha huyu mwenyekiti wa tahiliso kukaimisha nafasi yake kwa muda na kisha kwenda kugombea umakamu mwenyekiti uvccm taifa sijaikubali kabisa kwa sababu inaonyesha huyu jamaa yupo kimkakati kufanikisha kujilisha na si kuwakilisha.
  Sikubaliani na kitendo chake cha kukaimisha nafasi yake kwa muda na kwenda kugombea uvccm na kwamba eti akishinda huko ndio aachie madaraka yake rasmi na akishindwa eti arudi tena tahiliso,kwa mtazamo wangu hii ni dharau kwa tahiliso.
  Sijaisoma katiba ya tahiliso lakini naamini kabisa suala hili halipo kwenye katiba ila basi huyu paul makonda kwa mtazamo wangu angekubalika zaidi kama angeamua kuachia ngazi nafasi yake ya uenyekiti tahiliso na kujikita kwenye kuwania hiyo nafasi ya umakamu mwenyekiti uvccm na asingeweka masharti kwamba eti akishindwa huko uvccm atarudi tahiliso akishinda ndio aachie ngazi tahiliso. Naamini kabisa kuna watu wengi wanaweza kuongoza tahiliso vizuri hakuna haja ya nafasi ya ungozi wa juu kuksimiwa kwasababu ya kumruhusu yeye kwenda kugombea uvccm ingekuwa bora aachie ngazi kabisa hata akishindwa asirudi tena tahiliso, asijifanye mtaka yote
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  inaelekea hukumsikiliza au kama ulimsikiliza hukumwelewa au unapotosha makusudi kwa maslahi yako na wanaokutuma.makonda alijiuzulu na kumwachia majukumu yote makam wake.acha upofu wa kufikiri,.wengi tuliiona hiyo taarifa akiongea kwenye vyombo vya habari
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  makonda ni kiboko ya mafisadi ndio mana mnamsakama.poleni sana
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  inaelekea we ndio beno wewe.baada ya kubanwa kisawa sawa na wanamabadiliko ya kweli wasiofikiri kwa kutumia matumbo unatafuta huruma ya wana jf.
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  BENO Malisa acha kutapatapa,lazima ung'oke UVCCM kwa aibu.kijana umeaminika ukaanza kufikiri kutumia tumbo.
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  .TAARIFA KWA UMMA


  1.0 UTANGULIZI.
  Ndugu zangu wanahabari na wadau wote, napenda kuwakaribisha katika mkutano wetu wa leo tarehe 28 septemba, 2012 ambao unalenga kuwashukuru kwa dhati ya moyo wangu wajumbe wote wa vikao vya Chama Cha Mapi...nduzi chini ya busara na hekima za Mwenyekiti-CCM Taifa MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE (Rais) vilivyomalizika hivi karibuni mjini Dodoma na hatimaye kupitisha majina mbalimbali ya wagombea nikiwemo mimi PAUL MAKONDA kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa.


  2.0 SHUKURANI.
  Napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ,vikao vyote vya CCM kupitia kwa umakini majina yote ya wagombea na kupitisha jina langu mimi PAUL MAKONDA kugombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM-Taifa kwa kuniona ninafaa kukitumikia na kukiongoza Chama kupitia UVCCM katika nafasi hiyo.Nitatumia uzoefu wangu wote,ushauri wenye tija na misingi iliyowekwa na Chama katika kuiongoza UVCCM kwa `kushirikiana na viongozi wote wa jumuiya zote na ngazi zote za CCM wakati nitakapopata nafasi kuwa Makamu Mwenyekiti –UVCCM Taifa.


  Pia napenda kuwashukuru kwa dhati viongozi wote wa Vyuo Vikuu/Taasisi za elimu ya juu nchini kwa kuniamini na kunichagua kuwa Mwenyekiti wa "TAHLISO" mnamo 27 Septemba, 2011 mpaka hivi leo ambapo tangaza rasmi kukasimisha nafasi yangu ya Mwenyekiti kwa Makamu Mwenyekiti wa "TAHLISO" Taifa Ndugu AHMED ABUBAKARY MOHAMED kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi hiki.Nawashukuru viongozi wote
  ,Wizara,Wakurugenzi na Viongozi wote na wadau wa elimu ya juu nchini kwa ushirikiani mkubwa walionipa kipindi chote cha uongozi wangu wa "TAHLISO"
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  3.0 DHAMIRA.
  Nimewiwa kufanya hivyo ili kutenganisha kofia mbili za uongozi kwa wakati mmoja "TAHLISO na siasa za vyama (UVCCM) nakuzuia mgongano maslahi ya kisiasa dhidi TAHLISO kwani TAHLISO ni Umoja wa Serikali za Wanafunzi Tanzania ulio huru usioingiliwa au jihusisha na chama chochote cha siasa nchini.Hivyo kujenga imani,mshikamano,utulivu na amani kwa wadau wote kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana katika kipindi chote.


  Pia itanisaidia kufanya kushiriki kuijenga UVCCM kwa ustadi mkubwa
  pindi nitakapopata nafasi katika mchakato wa uchaguzi kwa kutumia
  kofia moja tu.

  4.0 HITIMISHO.
  Nawashukuru tena kwa dhati wote mlio hudhuria mkutano huu na kuwaomba tushirikiane kwa pamoja kuijenga nchi na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.

  "MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA."

  PAUL MAKONDASee More-
   
 15. m

  mkatangara Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasema tena huyu jamaa afai kuwa kiongozi kwa sababu kwanza anajionyesha hajiamini kama nafasi anayokwenda kugombea atashinda na pili inaonekana anatamaa sana ya uongozi, kwanini akaimishe nafasi ya Uenyekiti Tahiliso na kwenda kugombea nafasi ya umakamu mwenyekiti UVCCM.

  kwa masharti ya kwamba akishindwa arudi kuendelea na uenyekiti wake tahiliso na akishinda ndio Ajiuzuru. Huo ndio ukweli wenyew msituletee taarifa yake aliyoitoka kwenye vyombo vya habari kama utetezi kwamba kajiuzuru, hata taarifa yenyewe inasema anakaimisha kwa wakati huu.

  Aache kigeugeu na tamaa za madaraka, tamaa zilimuua fisi. Anataka kutufanya watu sio waelewa sio.
  Na kwa taarifa aliyenisema mimi ni Beno Malisa umekosea sana kunifananisha na huyo mpumbavu na stupidy person ungejua navyo muhate huyo jamaa usingenifananisha nae.
  Mimi ni mkatangara natokea kijiji cha katangara , mashati.
   
 16. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Unajua maana ya jembe lakini? Kwahiyo ili afanye kazi lazima atiwe mpini sio? Unamsifia au unamnanga?
   
 17. P

  Pilitoni JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 1,001
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Masaburi aliona mbali sana! Naogopa ban ila narudia tena; makonda ni jembe na hilo liko wazi na halina ubishi.
   
 18. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Makonda ni mmoja wa waanzilishi wa CCJ hana uhakika wa kushinda hiyo nafasi.
   
 19. Shindu Namwaka

  Shindu Namwaka JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2017
  Joined: Sep 22, 2014
  Messages: 4,690
  Likes Received: 2,832
  Trophy Points: 280
  Ndivyo Walivyo
   
 20. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2017
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  wale wale
   
Loading...