VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kujiamini sana kuna madhara makubwa. Kuamini kuwa umemshika na kumdhibiti Mkuu wako kuna pigo kuu. Rais hutumbua watu na kauli zao kutokana na kumchokoza. Kumchokoza huwaponza. Lilipotolewa tamko la kuwahamisha wamachinga kule Mwanza, Rais alichokozeka. Akaitengua kauli.
Waziri Mwakyembe alipotamka kuhusu vyeti vya ndoa, Rais alichokozeka na kauli yake ikatenguliwa. Mama Kilango aliposema 'uongo' kuhusu watumishi feki akatenguliwa. Ukimya wake ukamrejesha Bungeni. Wapo wengine wengi waliomchokoza Rais na wametumbuliwa.
Bwana Makonda wa Dar, umetoa kauli ya kwamba kila mwananchi wa Dar awe na kitambulisho ima cha ajira au cha ujasiriamali. Unajua kuwa kwa wengine, choka mbaya kutokana na Maisha kutofautiana, hawakijui hata kitambulisho wala kujua maana yake? Umekuwa ukifanya na kusema mambo mbalimbali ya kichokozi kwa Rais. Umekuwa ukichuniwa.
Unadhani na kuamini kuwa huwezi kumchokoza Rais Magufuli? Eti, kila mtu awe na kitambulisho. Hii ni kauli iliyosheheni dharau, kejeli na majivuno kwa wengine. Hii ni kauli ya kutojali wanaokuzunguka na kuamini kuwa ulichonacho wote wanacho. Chunga sna Makonda. Kalaghabaho!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa kuhudumia mashamba yangu)