Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,321
- 72,749
Habari za magazetini asubuhi hii zinasema Mkuu wa mkoa wa Dar Bw Makonda ametoa siku tisini viwanda vinavyotengeneza mifuko ya plastik kuacha uzalishaji kudhibiti uchafu Dar es salaam. Hili ni jambo zuri lakini haliko kwenye hadhi ya kimkoa bali ya kitaifa kwani viwanda vilivyoko Dar sii kwa ajili ya jiji hilo pekee bali nchi nzima.
Mamlaka ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastic hayawezi kuwa ya Dar es salaam pekee bali yanapaswa kuwa kwa nchi nzima, na kwa hivyo hata kama Makonda anasifiwa na Rais lakini hawezi kuwa na mamlaka ya kuagiza jambo linalohusu mikoa mingine. Hili jambo lingeshughulikiwa na watu wa NEMC au wizara ya Viwanda na Biashara kwa kuweka sera ya nchi nzima juu ya matumizi ya mifuko ya plastic kama ilivyo Rwanda na kwingineko.
Paulo Makonda unapaswa kufanya kazi kwa kuangalia mipaka yake na sio kutafuta sifa kila jambo uonekane umeanzisha wazo jipya, utaleta migongano isiyo na sababu na jifunze uendeshaji wa shughuli za serikali maana hizo sio za chama.