GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,418
- 120,737
Mosi nianze tu kwa kusema kuwa nilikuwa miongoni na bado ni miongoni wa Watu ambao nimependa sana uteuzi wako kwa hiyo nafasi ya Ukuu wa Mkoa hasa kutokana na utendaji wako ulipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwani ulionyesha kuwa ni tumaini jipya kwa Vijana katika nyanja nzima ya Uongozi.
Mheshimiwa naomba tu utanivumilia kwa haya nitakayoenda kusema hapa kwani naamini ukiyachukulia kwa uzito wake mkubwa naweza nikawa nimekusaidia kama si kukuongezea kitu katika Uongozi wako ila ukiyachukulia kwa hisia hasi utaniona Mimi ni adui yako na bahati mbaya mno nimeumbwa kusema ukweli na kuwa muwazi bila uwoga.
Mheshimiwa Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam itoshe tu kusema kuwa tokea upate hiyo nafasi ya Uongozi binafsi sijaona bado lolote ulilolibadilisha zaidi tu ya kuona kipaumbele haya yafuatayo:
Labda nikusaidie tu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwani yawezekana ukawa umesahau kuwa huu Mkoa wa " Changanyikeni Brains " nikimaanisha wa Dar es Salaam umeshawahi kuwa na Wakuu wa Mikoa ambao walikuwa wakali wewe cha mtoto lakini wameondoka na kuuacha Mkoa wa " Changanyikeni Brains " ukiwa vile vile.
Nadhani ungetumia muda wako mwingi kufanya utafiti wa jinsi gani unaweza kuuongoza vizuri huu Mkoa wa " Changanyikeni Brains " ungefanikiwa mno na sana ila bahati mbaya ninavyokuona na Wewe unataka kupita kule kule walikopita watangulizi wako na niseme sidhani kama utafanikiwa kama ambavyo umefanikiwa kuombewa sana hadharani na Viongozi wa dini kila uchao.
Kuna kauli ambazo umezitoa jana hasa za kuhusiana na Mashoga na Wavuta Sigara pamoja na Shisha. Binafsi nimeyapokea haya matamko yako kwa Wasiwasi fulani hivi hasa nikijua ugumu uliopo na ambao pengine utaupata juu yake.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa hivi kama tu yale mambo niliyoyaorodhesha katika aya yangu ya nne ( 4 ) hapo juu ambayo ndiyo ya msingi bado mpaka sasa umeshindwa kuyatekeleza haya magumu kabisa ya Mashoga na Wavutaji " fegi " na hadi " sigara bwege " utayaweza kweli?
Nimalizie tu kwa kusema kuwa jitahidi sana uwe na Vipaumbele vyako vikuu kadhaa katika Uongozi wako na pia ukijipa time frame ya utekelezaji wake badala ya kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja kwani kwa Watu waliobobea katika Management na Administration wanaweza wakakushangaa. Kiongozi makini huwa na Vipaumbele vichache na ambavyo huwa na uhakika navyo kuwa ataviweza na siyo kama hivi ufanyavyo Wewe na ndiyo maana hapo juu nimekuambia kuwa punguza drama na acha siasa.
Nikutakie tu usomaji mwema wa huu UZI wangu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa " Changanyikeni Brains " na yapokee tu haya katika dhana nzima kimtazamo na yafanyie kazi kwani kwa umri ulionao nina uhakika unaweza ukabadilika na hatimaye kuja kuwa Kiongozi mmoja wa mfano kwa sisi Vijana wenzio na labda nikutoe tu hofu kwa kusema kuwa so far unaenda vizuri kiasi ila nikuombe tu punguza " mashauzi ".
Uwe na Jumapili njema na naomba kuwasilisha.

- Kupenda publicity.
- Kufanya drama zisizo na mpango.
- Kutoa kauli bila ya kuzipima kwanza.
- Kupiga " mikwara " ya kitoto na isiyo na tija.