Paul Makonda punguza siasa na drama badala yake fanya Kazi...

Matamko yasiyofanyiwa utafiti wa aina yoyote yanazidi kuturudisha miaka mingi nyuma. Wanachojua wao ni kuwa wanatawala kwa kutumia Polisi, sasa sijui wanategemea watasafisha jiji kwa kutumia jeshi la Polisi? Usafi anaojua Polisi ni usafi wa zile Uniforms tu, nenda kakague usafi wa kuanzia pale anapoishi, ofisini na penginepo ndiyo utagundua Polisi wetu hawajui uchafu ni nini, sasa sijui watatumikaje kuhakikishaje Mkoa unakuwa msafi wakati hawajui tofauti ya hali hizo mbili!
Makonda ni Time buyer tu, na katika hilo ameweza sana kumkamata mkuu. Mpaka sasa sijui ameweza kufanikisha lipi kati ya yote.
Tusifanye masikhara na uongozi wa wa kijamii, hii tabia ya 'tuwape muda' ndiyo imesababisha miaka hamsini tuendelee kuchechemea tu, kila anayekuja tumpe muda, akipewa muda, mwaka umeisha tunaingia mwaka mwingine, tukikosoa tunaambiwa jamani mbona mwaka ndiyo umeanza hebu tumpe muda, mwaka wa pili unaisha, tunaingia mwaka wa tatu tukijaribu kukosoa au kuchangia tofauti tunaambiwa haraka ya nini wakati bado anaendelea kupambana, tusubiri akimaliza ndiyo tuone kama amweza au hajaweza. Akimaliza muda wake na akiwa amefeli na yeye ataungana na wakosoaji kulalamika eti mfumo umemkwamisha, tena atalalamika kwa sauti utadhani wakosoaji hawakuwahi kuonya hali hiyo ambayo wao waliikumbatia na kuitete kwa nguvu zote za kijeshi.
Miaka hamsini mingine itatukuta hapahapa...
Umesema kweli mwanangu
 
Kuna kitu Makonda na hata Magufuli naona hawakielewi kabisa
Mtu pekee Tanzania ambae alikuwa akitoa tamko linakua sheria hapo hapo alikuwa Mwalim Nyerere
baada ya hapo katiba ikarekebishwa

kuanzia sasa tamko lolote la kiongozi yeyote linapaswa kuendana na sheria zilizopo
kama hakuna sheria ya ku support hilo tamko basi hilo tamko halina maana yoyote

Sasa unasema eti marufuku kumfollow gay kwenye Instagram....unabaki unajiuliza
je mkuu wa mkoa anazijua hata sheria?
je huyo mtu ukimkamata utamshitaki kwa sheria zipi?
na akisema mimi siishi Dar nimekuja tu?
Mkuu umeua!!!
 
Wanabodi mtakumbuka maneno ya Baba Nanii
"Walianza kumsema Mak ni kasema atabaki hahapa
Walianza kumsema Kasesera DC wa Iringa nikasema atabaki palepale"
Anataka mumseme vibaya Mukulu wa Mukulu ambakize hapahapa
Mind gamesmanship
 
Sasa hapa panazungumziwa mashoga wa kiume au wakike?maana kuna mashoga yaani marafilki wa kike
 
HUU UZI NAOMBENI "MODERATOR'S" MUUUPIGE BAN TU; Una mwelekeo Wa kutetea Mashoga na uhalifu, Mkuu Wa mkoa Anajitahid kupambana Kwa hali na Mali lakini watu kama hawa wanaturudisha nyuma; huu Uzi naomba "mod's" muufute. Zoezi la kutokomeza ukahaba, ushoga na uchafu ni endelevu haliwezi kuisha Kwa siku mbili tu...mkiuacha huu Uzi uendelee kuwepo ni kuwa katisha tamaa viongozi! Ukuu Wa mkoa ni taasisi kubwa sana ina mambo mengi ya kufanya, mengine sisi kama wananchi husika tunatakiwa kumuunga mkono.

well said!
 
HUU UZI NAOMBENI "MODERATOR'S" MUUUPIGE BAN TU; Una mwelekeo Wa kutetea Mashoga na uhalifu, Mkuu Wa mkoa Anajitahid kupambana Kwa hali na Mali lakini watu kama hawa wanaturudisha nyuma; huu Uzi naomba "mod's" muufute. Zoezi la kutokomeza ukahaba, ushoga na uchafu ni endelevu haliwezi kuisha Kwa siku mbili tu...mkiuacha huu Uzi uendelee kuwepo ni kuwa katisha tamaa viongozi! Ukuu Wa mkoa ni taasisi kubwa sana ina mambo mengi ya kufanya, mengine sisi kama wananchi husika tunatakiwa kumuunga mkono.

Nikianzisha huwa linakuwa na usijaribu kushindana na zawadi niliyopewa na Mwenyezi Mungu hivyo sidhani kama ombi lako hata limeangaliwa achilia mbali kufanyiwa Kazi. Wewe katika UZI wangu umeona USHOGA tu ila maudhui mengine ya maana kuzidi hata huo USHOGA hujayaona? Nimekudharau kuliko hata ninavyomdharau Ng'ombe pori.
 
Kama kweli una nia njema na hao viongozi basi ilipaswa usifie uzi huu. Kuna tofauti kati ya upendo wa dhati na kuwa mamluki. Upendo wa dhati ni ule wa kuwa tayari kurekebisha yule umpendae kwa nia njema hata kama itamkera, umamluki ni ile hali ya kuwa tayari kumsupport umpendae hata kama unakereka ama anapotoka. Hapa unataka kuleta umamluki.
GENTAMYCINE hajasema lolote baya, alichofanya ni kumkosoa kwa kumjenga (Constructive criticism) sasa ndugu unapotaka ban na kufutwa kwa uzi kisa tu ukweli umesemwa tutafika kweli?

Msamehe Mkuu huyo kwani hajui alitendalo. Mbona katika ule UZI wangu niliomsifu sana Makonda kuteuliwa kuwa RC hakujitokeza hivi kunishukuru? Leo kimemuwasha nini? Huyo ana lake jambo ila bahati mbaya sana kakutana na GENTAMYCINE hivyo ataishia tu kuisoma namba. Nikianzisha linakuwa, linakubalika na linapendwa vile vile na kama tatizo lake ni NYOTA akatafute zinaposafishwa nae awe " juu ".
 
Hujaelew haluna anayetete mashoga na hakuna anayependa ushoga.. Sisi tunachomaanisha ni kuwa rc kaacha mambo ya muhimu kama usafi na mambo mengine anakomaa na kazi ambayo hataiweza... Anajipotezea muda tu

Akhsante Mkuu. Mfundisheni kujenga hoja na kufikiri vizuri huyo POPOMA na aache kukurupuka kwa chuki zake binafsi.
 
Kweli Mungu wetu ni Mungu wa maajabu. Leo Mkuu Gentamycine kwa mara ya kwanza tangu nimfahamu kaongea neno la maana lenye kueleweka na watu wenye akili timamu...naomba uwe mwanzo.

Leo umeonesha uzalendo kwa Mkoa wetu kwa kuziba pengo badala ya kuliita mwanya. Ushauri uliompa ndugu yetu, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ni ushauri mujarab. Yale uliyomuainishia kwenye aya ya 4, yanatosha kuyafanyia kazi kwa sasa. Mimi niongeze tu ushauri kwake: WEKA SANDUKU SEHEMU TUKUSAIDIE KURIPOTI MATUKIO YA BAA ZINAZOPIGA KELELE USIKU KUCHA MITAANI, na hata kupokea maoni mengine kuhusu uchafuzi wa hali ya hewa unaofanywa na bodaboda kwa kupiga kelele kwa kuzibua exhaust pipes za pikipiki na redio.

Safi sana GENTAMYCINE

Akhsante Mkuu na nimezipokea kwa mikono miwili.
 
Mosi nianze tu kwa kusema kuwa nilikuwa miongoni na bado ni miongoni wa Watu ambao nimependa sana uteuzi wako kwa hiyo nafasi ya Ukuu wa Mkoa hasa kutokana na utendaji wako ulipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwani ulionyesha kuwa ni tumaini jipya kwa Vijana katika nyanja nzima ya Uongozi.

Mheshimiwa naomba tu utanivumilia kwa haya nitakayoenda kusema hapa kwani naamini ukiyachukulia kwa uzito wake mkubwa naweza nikawa nimekusaidia kama si kukuongezea kitu katika Uongozi wako ila ukiyachukulia kwa hisia hasi utaniona Mimi ni adui yako na bahati mbaya mno nimeumbwa kusema ukweli na kuwa muwazi bila uwoga.

Mheshimiwa Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam itoshe tu kusema kuwa tokea upate hiyo nafasi ya Uongozi binafsi sijaona bado lolote ulilolibadilisha zaidi tu ya kuona kipaumbele haya yafuatayo:

  1. Kupenda publicity.
  2. Kufanya drama zisizo na mpango.
  3. Kutoa kauli bila ya kuzipima kwanza.
  4. Kupiga " mikwara " ya kitoto na isiyo na tija.
Mheshimiwa Paul Makonda nakumbuka huko nyuma uliwahi kutoa matamko kuwa hutaki kuona uchafu wowote jijini Dar je huo uchafu umeisha? Mheshimiwa Paul Makonda uliwahi kusema hutaki kuona Makahaba wakijiuza hapa jijini Dar je wameondoka? Mheshimiwa Paul Makonda uliwahi kusema hutaki Gereji bubu jijini Dar je zimeisha? Mheshimiwa Paul Makonda ni miezi michache tu ulisema kuwa Halmashauri zote za Dar zihakikishe barabara zote zipo katika hali nzuri je una uhakika hilo agizo lako limefanikiwa?,Mheshimiwa Paul Makonda ulisema kuwa hutaki kuona Kumbi za Starehe na Nyumba za Ibada zinapiga Mziki hadi usiku kucha na wa makelele je hilo umefanikiwa?

Labda nikusaidie tu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwani yawezekana ukawa umesahau kuwa huu Mkoa wa " Changanyikeni Brains " nikimaanisha wa Dar es Salaam umeshawahi kuwa na Wakuu wa Mikoa ambao walikuwa wakali wewe cha mtoto lakini wameondoka na kuuacha Mkoa wa " Changanyikeni Brains " ukiwa vile vile.

Nadhani ungetumia muda wako mwingi kufanya utafiti wa jinsi gani unaweza kuuongoza vizuri huu Mkoa wa " Changanyikeni Brains " ungefanikiwa mno na sana ila bahati mbaya ninavyokuona na Wewe unataka kupita kule kule walikopita watangulizi wako na niseme sidhani kama utafanikiwa kama ambavyo umefanikiwa kuombewa sana hadharani na Viongozi wa dini kila uchao.

Kuna kauli ambazo umezitoa jana hasa za kuhusiana na Mashoga na Wavuta Sigara pamoja na Shisha. Binafsi nimeyapokea haya matamko yako kwa Wasiwasi fulani hivi hasa nikijua ugumu uliopo na ambao pengine utaupata juu yake.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa hivi kama tu yale mambo niliyoyaorodhesha katika aya yangu ya nne ( 4 ) hapo juu ambayo ndiyo ya msingi bado mpaka sasa umeshindwa kuyatekeleza haya magumu kabisa ya Mashoga na Wavutaji " fegi " na hadi " sigara bwege " utayaweza kweli?

Nimalizie tu kwa kusema kuwa jitahidi sana uwe na Vipaumbele vyako vikuu kadhaa katika Uongozi wako na pia ukijipa time frame ya utekelezaji wake badala ya kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja kwani kwa Watu waliobobea katika Management na Administration wanaweza wakakushangaa. Kiongozi makini huwa na Vipaumbele vichache na ambavyo huwa na uhakika navyo kuwa ataviweza na siyo kama hivi ufanyavyo Wewe na ndiyo maana hapo juu nimekuambia kuwa punguza drama na acha siasa.

Nikutakie tu usomaji mwema wa huu UZI wangu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa " Changanyikeni Brains " na yapokee tu haya katika dhana nzima kimtazamo na yafanyie kazi kwani kwa umri ulionao nina uhakika unaweza ukabadilika na hatimaye kuja kuwa Kiongozi mmoja wa mfano kwa sisi Vijana wenzio na labda nikutoe tu hofu kwa kusema kuwa so far unaenda vizuri kiasi ila nikuombe tu punguza " mashauzi ".

Uwe na Jumapili njema na naomba kuwasilisha.

Kama ni dawa hii yako ni ya ukweli! Asipopona basi itabidi atafutwe mtaalam wa miti shamba.
 
Akhsante Mkuu. Mfundisheni kujenga hoja na kufikiri vizuri huyo POPOMA na aache kukurupuka kwa chuki zake binafsi.
Tatizo lililopo kuna kundi la watu wanatamani nchi hii iendeshwe kidikteta mfalme akiwa uchi wote mseme mfame amependeza, hili jambo haliwezekani.

Wanatuharibia nchi ni kikundi cha wavivu wachache ambao hat wawe wamesoma kiasi gani hawataki kujituma wanategemea waishi migongoni mwa wanasiasa na kutegemea teuzi.

Makonda ni mpenda sifa tu lakini akae akiwa Dar ndio Tanzania, watu wanaitumia hata ikulu kutapelia na kuna mapolisi wazito ngazi ya makamishna wanatapeliwa na watoto wadogo tu kwa uroho wa kuwa IGP.

Ila tatizo lingine inaonekana watu wa aina ya Makonda ndio chaguo la Magufuli, maana alivyomsifu na kasesera nimepata jibu.
 
Hakuna mahali aliniacha hoi kama aliposikia magufuli kakamata sukari,eti na yeye akaenda kukamata mifuko 160!eti mtu kaficha sukari!
 
tamko lolote la kiongozi yeyote linapaswa kuendana na sheria zilizopo
kama hakuna sheria ya ku support hilo tamko basi hilo tamko halina maana yoyote

Makonda anatakiwa apelekewe paragraph hii moja tu kama semina elekezi kwake

Hivi mimi sielewi, waliwaza nini kumreplace mzee Said Sadiq na huyu jamaa??
 
Back
Top Bottom