Paul Chizzi amuumbua Mwakyembe

shule zingine bomu kabisa. labda ni english unreachable. kununua nguo zote ndiyo hiyo dola 18000. weye mwenzetu ati wadhani uniform moja dola 18000?

Hapa hatupo kushinda elimu wewe dada na labda kama hujatembelea JF siku kadhaa zilizopita, huwezi kunielewa. Nukuu kidogo kutoka gazeti la tanzania daima la tarehe 8 inaweza kukusaidia pamoja na hiyo elimu ambayo si ya shule za kata kama yangu.

''Waziri huyo aligusia pia hatua ya baadhi ya maafisa kwenda nchini China na kukaa huko takriban siku 45 kwa ajili ya kusimamia sare za wafanyakazi, jambo ambalo alidai ni ufujaji wa fedha za umma kwa kugharamia sare moja dola 49,900.''

Nilimjibu mleta mada nikitumia nukuu hiyo na si vinginevyo.
 
kwani hizo dola 18,000 ni kidogo? wakati shirika halina hata ndege moja? Tusiwaonee haya wahalifu kama hawa ni hatari kwa nchi yetu

Umeona ehe chizzi acha kulalamika,jezi moja ya mfanyakazi ni sh. 3m?? Nayo ni kubwa mno jezi za china haizidi laki mbili kwa moja.
 

Usitutoe kwenye mada hatujathibitisha wizi wa chizi au mwakyembe kinachozungumzwa ni kukanushwa kwa kauli ya mwakyembe na chizi. Mwanzo kabisa wa sakata wengine tulisema kuwa ya mwakyembe hayana mantiki matokeo yake chizi amekanusha tusubiri mwendelezo. Ila ni kweli mawaziri wa serikali ya ccm ina maamuzi ya kukurupuka.
 
Kama kweli bwana Chizi anadhani Dr. Harrison amekosea au alidanganywa then sioni sababu yeye akae kubwabwaja kila siku kwenye vyombo vya habari. Uchunguzi utafanyika, nadhani atapata nafasi ya kujieleza then ukweli utajulikana.

Uwe mkweli mwakyembe kakurupuka, chizi anatufahamisha upande mwingine wa shilingi.
 


Chizi anafahamu sana anachokifanya, ameharibu akubali, aondoke akapumzike.Mwakyembe amezungumzia gharama ya uniforms ni $49,900, tena amesama wazi. lakini chizi kwa usanii wake na huyo mwandishi wanazungumzia bei ya uniform ni $18,000. bei na gharama ni vitu viwili tofauti, sasa sitegemei CEO apindishe tafsiri kati ya bei na gharama.
hao precision air walinunua uniform kwa bei kati ya $ 200 na $ 600 kwa kila mmoja. ATCL hata kama wangenunua kwa bai kama ya precision air, gharama ya ATCL kwa uniform zao bado ni juu , kwani wao (ATCL) walituma wafanyakazi wao kwenda kununua na walitumia siku 45 huko, so maisha yao huko yanaingia ktk gharama ya uniform.je precision air nao walituma watu china kwa siku 45?, kama wangefanya hivyo, si precision air ingeshakufa?. chizi ni mtu mzima ameharibu akubali. baadhi ya waandishi wetu nao ni waandishi uchwara, wana ripoti bila kuchunguza na kutafsiri wanacho ripoti
 
Wakuu, nimejaribu kuyasoma maelezo ya Bw. Chizi, japo lugha iliyotumika inanipa shida sana kuna kitu nimeshindwa kuelewa. Hususan anaposema "the matter is that the amount of money used to purchase the uniforms in China late last year was $18,000 only out of the stated amount, as the remaining amount was spent on the purchase of other materials,” stated Chizi.

Tatizo langu lipo katika hiyo rangi nyekundu, what on earth are these other materials which are not related to the uniforms? and why can't he mention them to justify his cleansing?
Naishia hapo misamiati imeniishia.
 
Sijasoma yote nitasoma baadaye lakini huu ni wizi na uhuni. Amekansha nini sasa hapo kihusu uniform? Anasema hela zingine zilitumika kununua other materials; yapi? Uhuni tu. Hivi angekuwa mbunifu si angewapa wanamitimdo wetu washone nguo zinazofanana fanana na Tanzania badala ya kukimbilia China. Ati CEO hivyo ana mandate; mandate y wizi?
 
Ana ushahidi kweli kwamba kwa kuagiza Uchina ameokoa milioni 40 za Kitanzania? Mbona hiyo difference ni kubwa mno. Uwizi tu kila mahala
 


Other materials ndio wizi wenyewe huo. Labda nguo za ndani!
 
kwani hizo dola 18,000 ni kidogo? wakati shirika halina hata ndege moja? Tusiwaonee haya wahalifu kama hawa ni hatari kwa nchi yetu

upo sahihi mkuu. Dola 18000 kwa peace 15 za uniform si sawa. Tena huy u kajikaanga mwenyewe achukuliwe hatua mara moja.
 

Lini tena aliongea zaidi ya hiyo jana na ndio leo tunaujua ukweli wa upande wapili, naona harufu ya Fidia kwa wale directors wengine 4.
 
Haijalishi maelezo mengi yanayoweza kutolewa ili kutafuta huruma ya Watanzania. Ukweli ni kuwa sio yeye tu inapaswa shirika zima hao wafanyakazi waondoke wote (imekuwa kama cancer) kwa miaka yote tunachosikia ni kuanguka kwa ndege na kukodisha kusiko mafanikio. Nasema haijalishi ikiwa waziri amekurupuka, wakati fulani tunahitaji watu wakusafisha na kisha mambo mengine baadae. Hivi sasa ATCL inatia aibu kuwa ndio mbeba bendera yetu.

$18,000 tu ndio zimetumika ????, je hizo za watu kukaa siku 45. Ikiwa unaweza nunua kila kitu kwa mtandao kwanini wakakae huko, je wao walikuwa wanazishona. Hii ni kansa, mtiririko wa wezi kupeana dili. Nashauri wafanyakazi wote hadi wafagizi, Waondolewe. Kisha tuanze moja.

Tumechoka kuibiwa kodi zetu!!!...
 
Si ajabu anaitwa chizi....utatumiaje dola 18,000 kushona nguo ambazo zaweza shonwa kwa batiki za hapa hapa na hata Millioni 2 isifike.....

nakuunga mkono ndugu yangu. Tatizo watz hatutaki kukubali kama twaweza kupendeza kwa kuvaa hata hizo batiki ambazo wahudumu wangependeza na kuonyesha utaifa wetu. Kuna wabunifu wengi tu wa kibongo kama kina Manju, naamini wasingeshindwa kubuni vazi la wahudumu wa ndege, naamini wangependeza sana na shirika kutumia gharama nafuu.
 
Nawewe kama kidhungu hujui si uulize? hizo 18000 ni kwa ajili ya nguo za wahudumu wa ndani ya ndege, mapokezi na marubani. Seti moja yaani viatu, soksi, sketi, chapi(not sure), blause, skafu, nk ni kati ya dola 200 mpaka 600. Na sio pea moja. Sasa rudi uchangie uzi.
 
Chizzi naona anamatatizo ya kisaikolojia kwa sasa hivi kweli anaona kama watanzania hatuna elimu ya kujua huu ni uhuni na huu si uhuni haingii akilini kusema shirt moja ilinunuliwa kwa usd 18000 kweli hata aibu hauna unaongea mbele ya medium bila kuongopa sikutegemea kama ukochizi kama jina lako lilivyo. tuondolee ujinga wako kama unaona nchi haina watu wenye elimu kakae hata na mkeo unaweza pata raha nje yakutuongezea hasira na machungu ya mali zetu mnazofaidi kikundi kidogo kama wewe.
 

Kaijage amehongwa senene kuhalalisha wizi umetukosa shule wote tumekwenda ila wewe ni msema chochote hata kama ni uwongo la kuvunda halina ubani kazi kutetea majizi tu shame on you
 
Huyu Chizi sasa naona kweli ameingiwa Uchizi.. Yaani ukimsoma tu unaelewa ana matatizo makubwa sana. Kifupi kama kweli wamenunua suti hizo kwa gharama ya Usd 18,000 na kuliepusha shirika gharama ya Usd 40,000 ina maana local supplier walitaka Usd 49,000 kwa suti 15?.. yaani kila suti moja karibu Usd 3,000!.

Hii inaingia akilini kweli jamani mimi naomba hizo tender walizoleta hao jamaa wanaotaka zaidi ya Usd 3,000 kwa suti, halafu kama kweli wamenunua direct China ndio anajifunga kabisaa maana China suti ya wahudumu na hata Ma pilot unaweza kupata kwa Usd 100 hadi 300 inategemea na grade..Hapo China ndio rahisi sana kupiga bao na kwa sababu najua hili nina hakika anayekwenda kununua China ana room ya kucheza na hesabu kwa sababu bei zao huwezi kuzipata sehemu yoyote duniani by far..
 
Angesema nini jana pale cdm square! Anajaribu kukisafisha chama ambacho kilisha oza kabisa cha kutupa.

Anajidahi kuwasafisha alaf wana mpoison.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…