Patrobas Katambi: Vyama vya upinzani ni mali ya mwenyekiti, wanachama wanaobaki wananufaika na mfumo uliopo

si alishawahi ongea na vyombo vya habari alivyoingia ccm ndio akaja na msemo wa karai, sasa karudi tena
 
Hivi kuna chama kinachomilikiwa na Mwenyekiti zaidi ya CCM?
Gazeti la Rai wakati wa enzi zake liliwahi kuandika makala mfululizo kuonyesha "umungu mtu wa Mwenyekiti wa CCM". Kimsingi kama wenyeviti wa vyama vingine nao wanamiliki vyama vyao, basi tabia hiyo wameiiga kutoka CCM. Dhana ya Mwenyekiti kumiliki chombo anachoongoza imeasisiwa na CCM na sasa imesambaa kote. Tujikumbushe:
-Bunge la Katiba tuliona vituko
-Bunge la sasa tunaona Spika/Mwenyekiti alivyo na madaraka kuliko bunge lenyewe
-Ukienda kwenye kamati za bunge, wenyeviti ni miungu watu
-Ukienda kwenye halmashauri - mameya na wenyeviti wana madaraka kuliko "mungu"

Katambi aseme wazi: Nguvu ya mwenyekiti wa sasa wa CCM ndiyo imempeleka CCM kutoka Chadema. na alipojaribu kukaidi maelekezo aliyopewa kwa kung'ang'ania apewe fedha kubwa, anajua mwenyewe kilichompata. Hawezi hata kumhadithia baba yake wala mkewe akiwa naye! Akibishi iko siku hayo mambo yatawekwa hadharani akose pa kupita.
 
Katambi ni bora ungeenda kwenye msiba wa mzee Kingunge ungepata promo kuliko kwa waandishi wa habari wa tbc na uhuru ambao gazeti na tv zao hazina wasomaji wala wasikilizaji tena!
Huu ushamba wako utakunyima fursa za uteuzi kwani huko ulikokimbilia wanakusoma na kukuona kilaza tu kwa maana ya kuwa siku ndoto yako isipotimizwa kwa hisani kwani huna jipya basi watakosa imani nawe na utawakimbia na kuwasema vibaya!
Ccm sio wajinga kama ulivyopima na wanachambua vigezo pia. Chunga sana hii staili yako ya kuvitaka usivyovimenyekea kwani hakuna uongozi wa zawadi tena siku hizi!
Waonaje ukihamia tlp ambayo ina nafasi za kitaifa zilizo wazi?
Umekosa sifa za kuwa roll model wa uvccm na vijana kwa ujumla! Hivi ni kweli ulitekwa kipindi cha uchaguzi au bei ilikuwa ndogo?
 
Huyu anatangaza live.
Maoni yenu.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA ambaye hivi karibuni alikihama chama hicho na kuhamia CCM Patrobas Katambi amejitokeza kwa mara ya kwanza na kueleza udhaifu mkubwa wa kiuongozi uliopo ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Patrobas amesema, vyama vingi vya siasa vya upinzani vimekuwa mali ya wenyeviti wa vyama hivyo na kueleza kuwa haviwezi kusonga mbele kutokana na mwenendo wa vyama hivyo.

Katambi amesema kuwa vyama vya siasa vya upinzani, vimekuwa vikifuja fedha za ruzuku na mara zote vimekuwa vikipata hati chafu katika matumizi yao ya ruzuku na fedha nyingine za chama.

Mwanasiasa huyo machachari amesema, alimua kutoka-CHADEMA kutokana na kupotea kwa ajenda na hoja za msingi na kusema kuwa wote waliobakia katika vyama vya upinzani wananufaika na mfumo uliopo.

Wewe kijana umenishangaza! Mbona sasa anaonyesha mapenzi makubwa kwa CHADEMA kuliko huko ulikokimbilia? Ongelea huko uliko.
 
Nani anajali kuhusu kuhama kwake? Ilipunguza nini Chadema na kuongeza nini CCM zaid ya kuichosha CCM kuyafikiria haya mazezeta wayape majukumu gani?
Halafu hili toto halijui kuwa halina athar hata huko CCM kama lilivyokuwa mzigo Chadema.
 
Huyu anatangaza live.
Maoni yenu.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA ambaye hivi karibuni alikihama chama hicho na kuhamia CCM Patrobas Katambi amejitokeza kwa mara ya kwanza na kueleza udhaifu mkubwa wa kiuongozi uliopo ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Patrobas amesema, vyama vingi vya siasa vya upinzani vimekuwa mali ya wenyeviti wa vyama hivyo na kueleza kuwa haviwezi kusonga mbele kutokana na mwenendo wa vyama hivyo.

Katambi amesema kuwa vyama vya siasa vya upinzani, vimekuwa vikifuja fedha za ruzuku na mara zote vimekuwa vikipata hati chafu katika matumizi yao ya ruzuku na fedha nyingine za chama.

Mwanasiasa huyo machachari amesema, alimua kutoka-CHADEMA kutokana na kupotea kwa ajenda na hoja za msingi na kusema kuwa wote waliobakia katika vyama vya upinzani wananufaika na mfumo uliopo.

Kwa maelezo ya Patrobas asinge stahili kubaki CHADEMA, amefilisika, hana hoja.
 
UVCCM MNA VITUKO. HATA MSIBA PIA MNATAKA KUUFUNIKA KWA KICK ZENU ZA KIJINGA. HUU HAMTAWEZA NI WA MTU MKUBWA NA MMOJA WA WAASISI WA TAIFA LETU.
 
Hahahahaha lol!! Lazima atokwe povu zito ili kuhakikisha analipwa alichoahidiwa. Anasahau kwamba wahuni wa MACCM ni majambazi ya kutupa ndiyo yameisha mtia ndani.

Anajiondoa mara ngapi??
Ha ha ha ha dogo kaondoka akaona amelipwa milioni 5 badala ya 30 walizomuahidi kupitia Juliana Shonza kaanza kutapatapa.

Sasa kapotea kwenye "Media",naona kaamua kutafuta tukio ili arudi tena midomoni mwa watu.Amekosea sana timing,leo ni kifo cha Mzee Ngombale na kesho ndio kitapamba kurasa za mbele
 
Back
Top Bottom