Wasalam , wana jamvi nakumbuka wakati tunatoa maneno yetu wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 nilionya na kuwaambia vyama pinzani haswa Chadema kwa kumpokea MHE Lowassa ndani ya chama chao ndio mwanzo wa kufa upinzani hilo linaenda kutimia hata kabla ya kuingia duru la pili la uchaguzi ndani ya nchi hii ya Tanzania mwaka 2020, kwa kuona wimbi la watu maarufu na vijana wenye elimu wakiondoka kurudi chama tawala cha Ccm, Patrobas Katambi ni kijana ambae amenistua sana leo achilia mbali Masha, Kitila Mkumbo, Albert Msando pamoja na Mwigamba.
Ukimchukua Patrobas unaweza kumlinganisha na kijana Humphrey polepole ambae amekuzwa katika misingi imara ya chama na kukomaa hadi kufika mahali alipo, kwa maaana nyingine chama cha mapinduzi kiliitambua hazina iliyomo ndani ya polepole na kuilea na kumfikisha mapaka alipo, maana yake hawakuupuza uwezo alionao polepole, nitaeleleza kwa kifupi kwanini nimeguswa na kuhama kwa huyu kijana haswa kwa kuzichambua kauli zake mwenyewe kwa kuzinukuuu alipokuwa anajieleza katika mkutano wa chama cha mapinduzi.
"Wapinzani wengi wanahubiri mabadiliko ila kiuhalisia wao wanaishi maisha ya kishetani wakati raia wanaumia" mwisho wa kunukuuu, nimepata wakati mgumu kuifanyia kazi kauli, je wapinzani ni wap? na Raia ni wapi? na maisha ya kishetani ni yapi? wakati Mhe Rais John Magufuli anapewa nguvu na mamlaka ya kupeperusha bendera ya chama wakatia wa kampeni za Urais alisema waziwazi bila ya kupepesa macho kuwa atapambana na rushwa na mafisadi haijalishi walikuwa wapi na katika chama kipi, na kweli Mhe Rais ametekeleza maneno yake kwa matendo bila ya kusitasita na wengine kuwakemea hadharani bila ya aibu ndani ya chama chake hata nje ya chama chake, Kama ni kweli Bwana Patrobas umeguswa na nguvu chanya ambayo Mhe Rais ameionesha karibu sana kwa mapambano sababu haya mapambano si ya mda mfupi kama wengi wadhaniavyo, uliposema raia wanaumia je uliimaanisha wanachama wanyonge waliopo chadema au ulimaaanisha raia wote ndani ya nchi hiii? jibu unalo wewe kama ni ndani ya chama cha chadema hilo ni halisi na huwezi kulificha ni chama ambacho kimebeba ukanda na uabinafsi, bila ya kuwa wa kanda Fulani huwezi kufaidi matunda ya chama ukiwemo mgawanyo wa uongozi na mapato ya chama, ingawa we ulikuwa mwenyekiti wa Bavicha hapo ndio nafika Napata shaka au kuongeza Imani na wewe yawezekana unaishi unayoyahubiri
"Kwa upinzani kijana ni karai katika ujenzi wa ghorofa" hii ni kauli yako nyingine ambayo pia imenigusa mtima wangu, kama ulitumia nguvu zako nyingi kuitumikia chadema na mwenyekiti wako uliyemkimbia Bw. Mbowe , na malipo yake hayalingani na kile ulichokuwa unapigania kila siku, hiyo ni hakika kabisa kwa kijana mwenye akili timamu, yaani hauna matatizo ya akili lazima ujitazame na ujiulize thamani yako iko wapi ? kama kijana, na hii ni kwa vijana wote wa kitanzania, kama upo mahali na unatoa mchango Mkubwa ambao unaleta matokeo chanya mahali ulipo, lakini wenye kuyapata matokeo yale hawauthamini mchango wako, ni budi ujiulize thamani yako pale iko wapi?
"Leo hii upinzani umegubikwa na umimi, ubinafsi na makundi" Siamini kama hili ndio umeliona leo Ndugu yangu Patrobas, utawala wowote kuanzia ngazi ya familia ukikosa utawala wenye misimamo na busara , tatizo hili utokea , vivyo hivyo katika vyama vyote vya siasa haijalishi ni chama tawala au cha upinzani, vivyohivyo katika uongozi wa nchi, mimi binafsi nakushauri kama ulikuwa umeshathiirika na tatizo kama hilo, jitibu haraka na uliache huko ulipotoka kama unaona huwezi kujitibu tafuta matabibu, utajitengenezea heshima na baadae kuja kuwa Kiongozi mzuri, namshukuru sana Mhe rais John Magufuli kwa kuonesha njia vijana sasa wameanza kuuona ukweli unaogusa nafsi zao.
"Kama nitaitwa msaliti basi nasaliti ubinafsi, kwa watu binafsi, kwa maslahi ya taifa"Dah kauli nzito sana hiii kwa kijana kama wewe kuitoa, hakika umegundua ubinfsi uliopo chadema, kuanzia Kiongozi wenu Mkuu na wengineo ndani ya chama , kama ni kweli umeamua kuusaliti ubinafsi, anza kuusaliti ambao upo ndani ya moyo wako, na hili pia nawaambia vijana wote wa Kitanzania ukitaka kufika mbali katika nchi hiii kamwe ubinafsi na umimi usibebe moyo wako, Karibu sana Patrobas ndani ya chama chenye mwelekeo, kaa ukielewa mapambano yanaendelea.
Hongera Rais wangu Magufuli, usivunjike moyo , wameanza kukubali unachokipigania, aluta continua....................................