Patrice Motsepe: Senegali wana haki ya kukata Rufaa

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
354
Reaction score
1,042
Patrice.jpg

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ametetea uadilifu na Uhuru wa Taasisi hiyo kufuatia wito wa Serikali ya Senegal kutaka uchunguzi wa kimataifa juu ya tuhuma za rushwa.

Akizungumza kupitia video iliyochapishwa kwenye tovuti ya CAF, Motsepe amefafanua kuwa kulikuwa na maamuzi tofauti kati ya Bodi ya Nidhamu na Bodi ya Rufaa, akisema Senegal ina haki ya kukata rufaa zaidi na CAF itaheshimu uamuzi wowote utakaotolewa na chombo cha juu zaidi.

Aidha, Motsepe ameongeza kuwa Wajumbe wa Bodi hizo huchaguliwa kutoka kwa mapendekezo ya Nchi Wanachama 54 wa CAF, na kwamba wanajumuisha Wataalamu wenye heshima kubwa wakiwemo Majaji na Wanasheria waliobobea Barani Afrika, ambao kwa mujibu wa rekodi zao zinaonyesha uadilifu na weledi katika maamuzi yao.

Kauli hii ya Motsepe inakuja baada ya CAF kuinyang’anya Senegal Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (AFCON) waliokuwa wameutwaa Mwezi Januari, ambapo Bodi ya Rufaa ya CAF ilibatilisha ushindi wa Senegal wa bao 1-0 dhidi ya Morocco na kuipa Morocco ushindi wa mezani wa mabao 3-0, huku Bodi hiyo ikieleza kuwa Senegal walikiuka kanuni kwa kuondoka Uwanjani wakati wa Mchezo wa Fainali.

Pia soma:
-Senegal imeapa kukata rufaa ya uamuzi wa CAF kuwapoka ubingwa wa AFCON 2025
- Senegal wapokwa ubingwa wa AFCON 2025 na CAF, apewa Morocco
 
Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ametetea uadilifu na Uhuru wa Taasisi hiyo kufuatia wito wa Serikali ya Senegal kutaka uchunguzi wa kimataifa juu ya tuhuma za rushwa.

Akizungumza kupitia video iliyochapishwa kwenye tovuti ya CAF, Motsepe amefafanua kuwa kulikuwa na maamuzi tofauti kati ya Bodi ya Nidhamu na Bodi ya Rufaa, akisema Senegal ina haki ya kukata rufaa zaidi na CAF itaheshimu uamuzi wowote utakaotolewa na chombo cha juu zaidi.

Aidha, Motsepe ameongeza kuwa Wajumbe wa Bodi hizo huchaguliwa kutoka kwa mapendekezo ya Nchi Wanachama 54 wa CAF, na kwamba wanajumuisha Wataalamu wenye heshima kubwa wakiwemo Majaji na Wanasheria waliobobea Barani Afrika, ambao kwa mujibu wa rekodi zao zinaonyesha uadilifu na weledi katika maamuzi yao.

Kauli hii ya Motsepe inakuja baada ya CAF kuinyang’anya Senegal Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (AFCON) waliokuwa wameutwaa Mwezi Januari, ambapo Bodi ya Rufaa ya CAF ilibatilisha ushindi wa Senegal wa bao 1-0 dhidi ya Morocco na kuipa Morocco ushindi wa mezani wa mabao 3-0, huku Bodi hiyo ikieleza kuwa Senegal walikiuka kanuni kwa kuondoka Uwanjani wakati wa Mchezo wa Fainali.
Wa Africa inabidi tutowe siasa na rushwa kwenye mchezo wa mpira otherwise tutauharibu kabisa.
 
Back
Top Bottom