Pato la Taifa lapanda kwa asilimia 7

Pato la Taifa lapanda kwa asilimia 7

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema pato la taifa limekuwa kwa asilimia 7 kwa mwaka 2019 sawa na ilivyokuwa kwa mwaka 2018.

Dkt. Mpango ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na kueleza sekta ambazo zinaongoza kwa ukuaji nchini.

Amezitaja sekta zilizoongoza katika ukuaji ni pamoja na uchimbaji wa madini na mawe kwa asilimia 17.7, ujenzi kwa asilimia 14.1, sanaa na burudani asilimia 11.2, usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 8.7.

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai aliikataa hotuba ya bajeti ya fedha na mipango ya kambi ya upinzani kutokana na Waziri Kivuli Mh. Halima Mdee kutokuwepo bungeni wakati baadhi ya wabunge waliokuwa wamejiweka karantini wamerejea bungeni.
 
Da!Sasa Kama ni sawa na mwaka 2019 imekuaaje?Au ulianguka mwaka gani na kwa asilimia ngapi?

Kuwa mboch sio jibu
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema pato la taifa limekuwa kwa asilimia 7 kwa mwaka 2019 sawa na ilivyokuwa kwa mwaka 2018.

Dkt. Mpango ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na kueleza sekta ambazo zinaongoza kwa ukuaji nchini.

Amezitaja sekta zilizoongoza katika ukuaji ni pamoja na uchimbaji wa madini na mawe kwa asilimia 17.7, ujenzi kwa asilimia 14.1, sanaa na burudani asilimia 11.2, usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 8.7.

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai aliikataa hotuba ya bajeti ya fedha na mipango ya kambi ya upinzani kutokana na Waziri Kivuli Mh. Halima Mdee kutokuwepo bungeni wakati baadhi ya wabunge waliokuwa wamejiweka karantini wamerejea bungeni.
Hongera kwa serikali,ingawa pongezi zisifike mpaka IMF wathibitishe kwanza maana zama za mapishi hizi.
 
Pato la Taifa linalokua kila mwaka kwenye makaratasi lina tija gani kwa wananchi wa kawaida? Wafanyakazi hali mbaya, wafanyabiashara kila siku wanalalamikia mazingira magumu ya kufanya biashara!

Wakulima zaidi ya 75% mpaka leo, miaka 59 tangu tupate Uhuru wanategemea jembe la mkono! Halafu eti pato la Taifa linakua kwa 7%! Labda kama linakua kwa hao Wakoloni wetu Weusi wa Ccm.
 
Back
Top Bottom