Patashika vita Rais Magufuli, IMF na mafisadi nguli

Patashika vita Rais Magufuli, IMF na mafisadi nguli

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
TUNAWEZA kuifananisha hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli [JPM], ya kufungua rasmi Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma, 20 Novemba mwaka huu na ?Sindano ya moto? kwa nchi iliyo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi chini ya uangalizi maalum [ICU].

Hotuba hiyo inaweza kufananishwa tu na hotuba iliyowahi kutolewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1978, alipoutimua nchini ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa [IMF], kwa kujaribu kushinikiza sera zake za kiuaji kwa uchumi wa nchi yetu.

Na baada ya ujumbe huo kuondoka puta nchini bila kutazama nyuma, Mwalimu alimgeukia aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa wakati huo, Edwin Mtei, na ambaye ndiye aliyepigia debe sera za IMF kuingizwa nchini dhidi ya sera za ?utu? za Mwalimu akamwambia, ?hutufai? na kumtaka kuachia ngazi mara moja.

Haraka haraka IMF wakamchukua Mtei na kumfanya mmoja wa Wakurugenzi wa taasisi dada na IMF chini ya Mashirika ya ukoloni-mamboleo ya ?Bretton Woods? ? Benki ya Dunia [WB], kumtumia kama kipago cha kuiandama Tanzania ili kuhakikisha inalipa kwa ?dhambi? ya kumfukuza zimwi mla watu nchini.

Ilikuwa vita kati ya Goliati [wa Kibiblia] mbabe wa vita [IMF/WB], pandikizi lenye silaha kali za mauaji, uonevu, dhuluma na madhara mengine kwa wanyonge, na kijana Daudi mshindi [Nyerere], kwa kumuua mtesi huyo kwa silaha duni [dhamira na dhamiri safi, utetezi na harakati dhidi ya ukandamizaji] kombeo, aina fulani ya manati makubwa.

Kama isingekuwa vita dhidi ya uvamiziwa nduli Idi Amini wa Uganda kwa nchi yetu mwaka huo, iliyoparanganyisha uchumi na mipango yetu ya maendeleo; ushindi wa Mwalimu dhidi ya IMF, ilikuwa kinga tosha katika kukuza kwa uchumi wetu kuliko ilivyo sasa, ikilinganishwa na nchi nyingi za dunia ya tatu.

Tunaiita hotuba ya Rais ?sindano ya moto? kwa sababu nchi zote za dunia ya tatu, ikiwamo Tanzania, zinaangamia kiuchumi na kijamii kwa kubugia bila udadisi, sera za IMF na WB na kujikuta katika kibano kutoweza kujinasua au kuleta mabadiliko kwa mema kwa watu wao. Aliyosema Rais Magufuli yanaweza kuwa sehemu ya dawa kwauchumi ulioparanganyika. Rais Magufuli kama Nyerere?

Tangu kung?atuka madarakani kwa Mwalimu Oktoba 1985, IMF na WB yametumia nguvu za ziada kutukejeli kwamba, tulifanya makosa kumsikiliza Mwalimu, na kwamba eti tulipoteza nafasi nzuri ya kuingia ?peponi? mapema; wakati ukweli ni kwamba hivi leo tu masikini zaidi na tegemezi wa misaada kutoka Ulaya, katikati ya utajiri mkubwa wa nchi; kuliko ilivyokuwa enzi za Serikali ya awamu ya kwanza.

Na hii hali ya ?amani na utulivu? tunayojivunia lakini iliyomo hatarini kutoweka kutokana na kuzuka ubaguzi wa kitabaka chini ya sera za IMF/WB, ilitokana na sera za ?utii? za Serikali ya awamu ya kwanza.

Umasikini nchini sasa ni janga kwa zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania. Na ingawa inadaiwa kitakwimu kwamba uchumi wa nchi unakua kwa asilimia saba, takwimu hizo hazishabihiani na hali halisi ya umasikini wa kurindima miongoni mwa watu.

Kumekuwa na heka heka za hapa na pale za ?shughuli za kiuchumi?, maghorofa marefu yakiibuka mijini kama uyoga kutoa picha bandia ya maendeleo na kukua kwa uchumi; lakini kiuhalisia watu wameendelea kuwa masikini kuliko mwanzo na kusababisha mihemko ya kisiasa na kiuchumi kutishia amani nchini.

Ufa kati ya ?walio nacho? [matajiri] na ?wasio nacho? [masikini] unakua kwa kasi ya kutisha na kujengeka matabaka hasama kwa misingi ya ?wao? [matajiri] na ?sisi? [masikini] na hivyo kutishia hali ya amani na utulivu nchini.

Hilo ni dhahiri, kwani jamii yenye umasikini wa kurindima kwa upande mmoja na utajiri kuwa mikononi mwa wachache kwa upande mwingine, haiwezi kujijengea misingi bora ya utajiri wa Taifa; wala haiwezi kuwa ya kidemokrasia.

Na hili alilibaini mapema Mwalimu Nyerere, akaamua kutibu ugonjwa kwa kuanzisha Azimio la Arusha na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea mwaka 1967; na sasa Rais Magufuli amelibaini pia si kwa kuchelewa sana, baada ya Watanzania kuonja adha ya ubepari unaoibuka kwa miaka 30, kuanzia na Serikali ya awamu ya pili ya ?ruksa? kwa kila kitu, mwaka 1985.

Chini ya sera za IMF na WB za kurekebisha uchumi [SAPs], tulidanganywa tukakubali kubinafsisha njia kuu za uchumi na miundo mbinu tuliyojenga kwa misuli yetu, eti kwa kufanya hivyo ufanisi na tija vinge ongezeka. Pamoja na mbwembwe za kuazima juu ya ufanisi chini ya programu ya ?Matokeo makubwa Sasa? [BRN], matokeo hayomakubwa yamekuwa ni umasikini wa kutisha, wizi, rushwa na ufisadi mkubwa kwa kila sekta.

Tena, Serikali ikaagizwa kujitoa katika kupanga uchumi na maendeleo ya nchi kwa kuachia nguvu ya soko ifanye kazi, na kazi pekee ya Serikali ibakie ya kusimamia na kulinda ?amani na utulivu? kama sehemu ya programu ya kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kutoka nje.

Kwa ujinga wetu tulikubali kuwasikiliza; tukabinafsisha kila kitu kwa wageni, viwanda vyetu wakavichukua na kuvitelekeza na vingine kuviua ili kutujengea utegemezi wa bidhaa zao kutoka nje kwa bei kubwa licha ya kuua ajira. Ubia na Wazawa tukaupiga teke kwa kejeli kwamba uwezo wao unaishia kwenye viwanda vya juisi na peremende tu.

Hao ?wawekezaji? tuliowatengenezea ?mazingira mazuri, amani na utulivu?, wamegeuka waporaji wa rasilimali zetu chini ya usimamizi na ridhaa yetu: angalia kashfa zinazofukarisha nchi kama zile za EPA, IPTL, Escrow, Meremeta, Deep Green, ?uwekezaji? wenye kunyonya nchi na kupandikizwa kwa utamaduni wa kutothamini utu na uzalendo miongoni mwa viongozi.

Chini ya utamaduni huu mpya, unaosimamiwa na kuratibiwa kwa mbali [teleguided] na ubepari pamoja na ubeberu wa kimataifa kwa nguvu ya mitaji, lengo kuu ni kuua uzalendo, utamaduni, maadili ya t aifa na uwajibikaji ili nchi igeuzwe ?shamba la bibi?, kwa kila ?fisadi? kupora kadri ya ukali wa kucha na wa meno yake.

Ni kwa sababu hii hatukushangaa mwaka jana, pale Bunge Maalum la Katiba [BMK], liliponyofoa na kuandika upya ibara za Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuhusu Maadili ya Uongozi na Utumishi wa Umma yenye kubana Viongozi, kinyume na yaliyopendekezwa na Tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba kutokana na maoni ya wananchi. Hii ni ishara tosha ya uozo uliotanda katika taasisi zetu likiwamo Bunge, ambamo viongozi wake wangependelea kuona ufisadi na kutowajibika kwa viongozi ukiendelea.

Tena tukadanganywa na hatimaye kushinikizwa kupunguza thamani ya fedha yetu kwa kuiita bila haya ?madafu?, kwa madai ya kuhamasisha kuongeza mauzo nchi za nje wakati hatukuwa, na hadi sasa hatuna cha kuuza kutokana na viwanda kuuawa na ?wawekezaji? tuliowakabidhi chini ya sera za ubinafsishaji usiojali.

Kisha tukaamrishwa na kukubali kuondoa ruzuku katika bidhaa muhimu kwa mlaji, elimu na tiba ili masikini wabebe msalaba wao mzito kuelekea golgota kwa sera za kuchangia gharama [cost sharing].

Tena, Serikali ikaagizwana kukubali kupunguza watumishi kwa matarajio kwamba sekta binafsi ingemeza jeshi lote la wasio na ajira, wakati kiuhalisia imekuwa kinyume chake na hivyo kutengeneza bomu la vijana wasio na kazi linaloweza kulipuka wakati wowote.

Yako wapi, na yamefanya kazi gani yale ?mabilioni ya Kikwete? tuliyoambiwa yangezalisha ajira kwa vijana?
Zimetafunwa na mafisadi tukiangalia kwa macho yetu; mzee wa watu [Rais Kikwete] ameondoka kimya kimya bila kutoa neno kwa nchi iliyolemewa na mzigo wa ufisadi!

Ukiondoa Serikali ya awamu ya kwanzaya Mwalimu Nyerere, Serikali za awamu tatu za mwisho zilichukulia kimbumbumbu sera za IMF na WB kama msahafu wa maendeleo ya uchumi kwa maangamizi yetu. Na hapa ndipo walipotufikisha, wakisema ?ndiyo? kwa kila shinikizo, wakimtetemekea kwa hofu ?kaka mkubwa? na Serikali za ubeberu na ubepari wa kimataifa.

Hali tuliyomo inatisha

Hali tuliyomo ni ya kutisha; kinachotakiwa hasa si mabadiliko, bali mtizamo mpya unaotutaka tubadili mwelekeo kutoka mwelekeo wa sasa wa ubinafsi kwa mdundo wa uchumi wa kifo, kuelekea uchumi wa kitaifa. Na juu ya yote, mabadiliko katika muundo wa uzalishaji mali.

Hili litahitaji mabadiliko kutoka mkakati wa maendeleo wa sasa unaotafuta ?ukombozi? kutoka nje [outward ? motivated] kwenda mkakati wenye ukombozi wa kweli kutoka ndani [inward motivated], na kwa msingi unaotambua kuwa, sababu za nje ni sharti tu la mabadiliko, wakati sababu za ndani ndizo msingi halisi wa mabadiliko; kwamba, malengo yetu ya ndani kwa ajili watu wetu ndiyo yatufanye tuongoze mabadiliko badala ya malengo ya [watu wa] nje kwa ajili ya maslahi ya nje yatufanye tuhangaikie mabadiliko kwa shinikizo [la IMF na WB] kutoka nje.

Baadhi ya mambo yaliyotufikisha katika hali hii ni pamoja na kutegemea kupita kiasi nchi zilizoendelea kwa maendeleo yetu.

Umahiri wa kutembeza bakuli la ?omba omba? kwa maendeleo umeua ubunifu na kuuza uhuru pia.

Ni aibu ilioje tuliyoshuhudia miaka ya karibuni, kwa nchi na kwa kiongozi wa nchi muumini wa safari za nje asiyejitambua, kudai bila aibu eti kwamba, safari hizo zisingekuwepo Watanzania wengi wangekufa kwa njaa?? Hii inaonesha jinsi baadhi ya Viongozi wanavyothamini utumwa na kujipendekeza kwa kaka mkubwa? kwa kuweka rehani uhuru wa nchi yetu.

Ikumbukwe kuwa, wakati tukitembeza bakuli nchi za nje, ?wawekezaji? wanapora rasilimali zaidi ya asilimia 4000 ya kiduchu wanachotufadhili. Je, shilingi bilioni 356.324, kwa mfano, zilizotumika kwa safari za nje kwa miaka miwili pekee [2013/2014 na 2014/2015] zisingetosha kununua chakula, ila kwa njia ya utalii wa matanuzi kama haya?.

Nchi yetu haihitaji kina ?James Mancham? wala ?Mobutu Sese Seko?, viongozi kwa njia ya matanuzi katikati ya umasikini wa kurindima miongoni mwa wananchi.

Mengine ni kutumia vibaya muda wetu kuzalisha bila umuhimu, bidhaa kwa ajili ya soko la nje, badala ya kuzalisha bidhaa zenye kukidhi kwanza mahitaji yetu ya msingi, kama vile chakula, makazi na mavazi. Aidha, ukopaji usio na tija na madeni ya mikopo yenye kuambatana na rushwa na riba kubwa, nalo ni tatizo linalokamua uchumi wetu.

Kukosekanakwa Sera makini juu ya nishati [umeme], kumetufanya tutegemee vyanzo kutoka nje kwa gharama kubwa na kwa kukomba akiba yetu ya fedha za kigeni. Baya zaidi ni rushwa na ufisadi mkubwa ulioghubika sekta hii, kuanzia na kashfa ya IPTL/TANESCO iliyolikamua taifa mabilioni ya fedha kwa miaka 20 mfululizo tangu mwaka 1994; kashfa ya Akaunti ya Escrow/Serikali/IPTL na hujuma kwa miundombinu ya vyanzo vya umeme nchini ili kuruhusu wawekezaji matapeli watambe, kumeathiri uzalishaji na kukua kwa uchumi.

Nchi yetu ingekuwa imeingia kwenye uchumi wa gesi tangu mwaka 1998, kama isingebanwa kwa nguvu turufu na IPTL kuruhusu Shirika hilo liendelee kutesa uchumi wetu bila mshindani.

JPM aondoe aibu, ashupalie kashfa hii sugu.Kwa upande mwingine, ubinafsishaji usiojali wa viwanda na njia muhimu za uzalishaji mali umeongeza utegemezi na uchumi wetu kusinyaa.

Kufikia hapo tujiulize: Tutaendelea hivi na kwa kuvumilia hali hii hadi lini? Wachumi wetu walikuwa wapi siku zote kuibua mambo haya kwa maendeleo ya nchi hadi wakurupushwe na Rais kwa ?kuitikia? na kudakiza ilivyo sasa?.

Magufuli Mkemia au Mchumi?

Sindano ya moto? ya Rais Magufuli, ambayo haikutarajiwa kutoka kwa msomi wa fani ya kemia kama yeye bali kwa mchumi mbobevu, imezua tahayari kwa wahafidhina wa sera za IMF na WB zenye kuzaa rushwa na ufisadi nchini. Kwa kifupi, Rais ameapa kuona na kuhakikisha kwamba madini na rasilimali zetu zinatumika kwa manufaa ya taifa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo, tofauti na ilivyo sasa ambapo kikundi kidogo cha wateule wachache na maswahiba wao wa nje, ndio wanaonufaika chini ya Sera mbovu na Mikataba ya uwekezaji yenye kufilisi nchi.

Tungekuwa na demokrasia ya kweli yenye kuruhusu sauti ya wananchi kuhoji na kusikika [social democracy], Marais waliotangulia [ukiacha Mwalimu Nyerere pekee], wangekuwa wamewekwa kando zamani kabla ya muda wao kwa kusaliti Katiba ya nchi inayotaka Serikali madarakani [ibara ya 9] kuhakikisha, ?kwamba, utajiri wa taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine?.

Tena kwamba, ?matumizi ya utajiri wa taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi [sio maendeleo ya vitu au ya watu wachache] na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umasikini, ujinga na maradhi?; na pia ?kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi?.

Utekelezaji wa matakwa haya ya Katiba umekuwa ni kinyume chake; jamii ya Kitanzania sasa ni mparanganyiko kati ya umma masikini wa kutupwa na matajiri wa kupindukia kwa kupora utajiri wa taifa.

Ni kwa nini Serikali za awamu tatu za mwisho zimekiuka bila hofu matakwa ya Katiba ya nchi, ni swali lisilo na jibu; lakini tunashindwa kujizuia kuamini kwamba ni kutokana na demokrasia duni, ubabe na mitizamo finyu ya viongozi mateka/mamluki wasiokuwa na chembe ya huruma wala uchungu kwa taifa na watu wake.

Tunajua, nia njema ya JPM kwa Watanzania itapata vihunzi ndani ya mfumo wa Chama na Serikali uliozoea vya kunyonga. Lakini chonde chonde kwa mafisadi ndani ya mfumo; kwamba kama hili litatokea, JPM atabakia shujaa nje ya mfumo, na mawe yatapiga kelele kudakia wimbo wake. Kindumbwe ndumbwe kitakachofuatia kwa umma uliochoka kwa ?mambo yale yale? na unaotaka mabadiliko, hakitabiriki.

Kuhusu viwanda vya umma vilivyobinafsishwa kisha kutelekezwa au kuuawa makusudi, Rais ameagiza vianze kazi mara moja ama vitatwaliwa na Serikali kwa kuzingatia sheria. Rais ameelekeza pia viwanda vitumie malighafi inayotoka ndani ya nchi, hususani toka sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, madini na rasilimali zingine ili kuzalisha bidhaa zinazotumiwa na watu wengi humu nchini ? nguo, viatu, na mafuta ya kupikia kabla ya kufikiria soko la nje.

Amesema, na kwa usahihi kabisa; kwamba lengo liwe ni kuimarisha mfumo wa uzalishaji ndani ya nchi uliofungamana na kushikamana [forward backward linkage] kwa manufaa ya uchumi wa nchi na ustawi wa jamii, mfumo unaopigwa vita na IMF, WB na mawakala wao nchini ili kutufanya tuendelee kuwa wahitaji na wategemezi daima.

Sindano ya Rais JPM inaibua vita ile ile kati ya Goliati mbabe na kijana Daudi.Tofauti pekee ni kuongezeka kwa adui mpya upande wa mbabe rushwa, wizi, ufisadi uliokithiri na ombwe la uongozi bora. Ameandaa vipi, au tumuandalieje kombeo kuweza kumbwaga mbabe ili wanyonge wapumue?


Itaendelea.

Raia Mwema
 
Wanajamvi
ninauza line za tigopesa na mpesa kwa yeyote anaehitaji
fanya kuni PM
tuongee biashara.
 
Pamoja na yote, IMF walikulazimisha pia:-

Kushamirisha rushwa, kuimarisha na kulinda mfumo fisadi?

Kuendesha serikali isiyokuwa na uwajibikaji wala kujali ustawi wa taifa na wananchi wake?

Kushindwa kusimamia sekta binafsi ili kuhakikisha inatekeleza malengo ya taifa kwa viwango vinavyotakiwa?

Kuua viwanda na kushindwa kuwa na nishati ya uhakika kwa uzalishaji?

Kuua elimu na kuanza kushusha viwango vya kila kitu kwa sababu tu watoto wa watawala mbumbumbu hawaelewi darasani ili nao wafaulu, na kutaa kuonyesha ufaulu umepanda bila kujali lwanafaulu kitu gani na kina tija gani katika maisha yao na taifa kwa ujumla?

Uvunjaji wa katiba na mauaji ya kisiasa?

Kuua democrasia na kuchakachua maamuzi ya Wananchi haasa nyenye maslahi ya taifa wa maslahi ya watawala na familia zao?

Matumizi mabovu ya raslimali za taifa zikiwemo mali asili, raslimali watu, fedha na maamuzi mabovu?

Kuweka viongozi wasio kuwa na uwezo wala sifa ili mradi tu wana nasaba ya aina moja ama nyingine na watawala?

Huduma mbovu za jamii na kuboresha ujinga na umaskini kama mtaji wa kutawala milele?

Kabla hamjanyoosha vidole kwa uadilifu na nia ovu za IMF, ni vizuri mkaanza kwanza ku question uadilifu na nia ovu ya ccm kwa taifa.

Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo uone kibanzi katika jicho la jirani yako.

Ccm ndiy mauti ya taifa hili.
 
hahahahahahahahahaha. this is great thinkers forum. nafurahi kuwa humu daima kwani kama una msongo wa mawazo,njoo jf ni tiba tosha.
 
Watu tupo gizani, umeme ni janga LA kitaifa, kila siku afadhali ya Jana halafu unatuletea mambo ya IMF.
 
Mchambuzi ameandika vema. Hata hivyo alitakiwa aelezee jinsi gani Mkapa amejutia uamuzi wa kukumbatia hizo bank. Maana tumesikia kauli zake mwaka jana akiwaasa viongozi wa Afrika kuacha kukumbatia mashirika hayo na utegemezi kutoka nje
 
Profesa Chachage aliwaita makuhadi. Kwanza mimi nawachukia wazungu na kila ninapomwona huwa natamani nimpige risasi. Mwalimu Nyerere alitwambia tufundishe waafrika katika mitaala yao inayojibu matatizo yao lakini leo nenda vyuoni, ni upuuzi mtupu. Mitaala yote tumeletewa eti twende sawa, sisi twende sawa na wazungu? yaani watu waliowahi kuwa na viwanda miaka zaidi za 400 leo twende nao sawa? na masoko na bei za mazao yetu twende nao sawa? angalia GATT inavyogeuka mnyoo wa kunyonya damu zetu. Tulishaambiwa na Mwalimu Nyerere kwamba huko nje hayuko Mjomba wala shangazi wa kuja kutusaidia matatizo yetu Afrika, hawa wazungu woooote wanaojifanya kutusaidia, they never mean it ..they are simply suckers and killers
 
IMF, WB na wazungu sio adui wa Watanzania, adui wa watanzania ni CCM, vitalu vyote vya mafuta na gesi, migodi mikubwa ccm wamewapa wazungu na viongozi wa ccm wanasema watz wanaweza kukamua matunda tu, wizi ,ufisadi na upendeleo kwa famili za viongozi ndivyo vinavyosababisha umasikini kwa watanzania kwani pesa wanazoiba manaweka ulaya na wananchi wanazilipa kwa kodi na wazungu wanazidisha tena kwa njia ya mikopo,umekua mzunguko viongozi wanautumia kuwanyonya watz, adui wa watz ni ccm, ukweli hatutaki kuusema, unafiki na ujinga wa watz ndio unawagharimu. Dawa namba moja ni kuikataa ccm kwanza ili Watanzania wamiliki mali zao wenyewe.
 
Pamoja na yote, IMF walikulazimisha pia:-

Kushamirisha rushwa, kuimarisha na kulinda mfumo fisadi?

Kuendesha serikali isiyokuwa na uwajibikaji wala kujali ustawi wa taifa na wananchi wake?

Kushindwa kusimamia sekta binafsi ili kuhakikisha inatekeleza malengo ya taifa kwa viwango vinavyotakiwa?

Kuua viwanda na kushindwa kuwa na nishati ya uhakika kwa uzalishaji?

Kuua elimu na kuanza kushusha viwango vya kila kitu kwa sababu tu watoto wa watawala mbumbumbu hawaelewi darasani ili nao wafaulu, na kutaa kuonyesha ufaulu umepanda bila kujali lwanafaulu kitu gani na kina tija gani katika maisha yao na taifa kwa ujumla?

Uvunjaji wa katiba na mauaji ya kisiasa?

Kuua democrasia na kuchakachua maamuzi ya Wananchi haasa nyenye maslahi ya taifa wa maslahi ya watawala na familia zao?

Matumizi mabovu ya raslimali za taifa zikiwemo mali asili, raslimali watu, fedha na maamuzi mabovu?

Kuweka viongozi wasio kuwa na uwezo wala sifa ili mradi tu wana nasaba ya aina moja ama nyingine na watawala?

Huduma mbovu za jamii na kuboresha ujinga na umaskini kama mtaji wa kutawala milele?

Kabla hamjanyoosha vidole kwa uadilifu na nia ovu za IMF, ni vizuri mkaanza kwanza ku question uadilifu na nia ovu ya ccm kwa taifa.

Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo uone kibanzi katika jicho la jirani yako.

Ccm ndiy mauti ya taifa hili.
Salute umenisemea uzoefu wangu wa miaka 70
 
IMF, WB na wazungu sio adui wa Watanzania, adui wa watanzania ni CCM, vitalu vyote vya mafuta na gesi, migodi mikubwa ccm wamewapa wazungu na viongozi wa ccm wanasema watz wanaweza kukamua matunda tu, wizi ,ufisadi na upendeleo kwa famili za viongozi ndivyo vinavyosababisha umasikini kwa watanzania kwani pesa wanazoiba manaweka ulaya na wananchi wanazilipa kwa kodi na wazungu wanazidisha tena kwa njia ya mikopo,umekua mzunguko viongozi wanautumia kuwanyonya watz, adui wa watz ni ccm, ukweli hatutaki kuusema, unafiki na ujinga wa watz ndio unawagharimu. Dawa namba moja ni kuikataa ccm kwanza ili Watanzania wamiliki mali zao wenyewe.

Nakupongeza wangu ccm ndio waliotufikisha hapa mijizi ccm mafisadi ccm metapeli ccm
 
Kama elimu yakoni ya darasa la saba utazielewa vipi sera za IMF/WB zilizotungwa na maprofesa wa uchumi???
 
Back
Top Bottom