Pata bitcoin kwa njia ya uchimbaji

Pata bitcoin kwa njia ya uchimbaji

Heshima kwenu wote wakubwa kwa wadogo! Natumai mnaendelea vyema!

Walau kwa DONDOO za hapa na pale kwa wale ambao wangependa kujua zaidi ningependa kuwashirikisha kile ambacho nimejifunza kuhusiana na Bitcoin.

Kwa uzoefu mdogo niliupata toka nimeanza kufuatilia na kupata bitcoins, zipo njia mbili za kupata bitcoins.

Njia ya kwanza ni TRADING yaani kuuza na kununua Biticoin.

Bitcoin ni aina ya sarafu kama ilivyo shilingi au dola,tofuauti yake ni kua yenyewe ni sarafu ya mtandaoni.Hivyo kama jinsi mtu anaponunua Dola kwa Shilingi kwa kutegemea exchange rate ya siku, ndivyo jinsi Bitcoin invyonunuliwa na kuuzwa kwa kutegemea exchange rate ya siku hio.

Faida kubwa ktk trading yaani kuuza na kununua Bitcoin hupatikana pale ambapo mtu ananunua bitcoin msimu ambao bei yake ni rahisi na kuiuza msimu ambapo bei yake inakua imeongezeka.

Njia ya Pili ya kupata bitcoin ni kwa operesheni iliopewa jina la Mining "Uchimbaji".

Hapa Bitcoin inachukuliwa kama jiwe la thamani mfano wa almasi au dhahabu ambazo hupatikana kwa njia ya kuchimba, tafauti ya uchimbaji wa bitcoin ni kua zoezi hili la uchimbaji linafanyika kwa kutatua milinganyo migumu ya mahesabu mtandaoni kwa kutumia computer.

Katika zoezi hili nguvu ya utatuzi wa milinganyo hii ambayo hutegemea na kupimwa na kasi ya computer husika(speed :the Number of bits of information/data that can be processed in a unit second) ndio msingi mkubwa wa uchimbaji, ndio maana computer za kawaida pekee hazitoshi kufanya zoezi hili kwa mafanikio yoyote ya kuridhisha.

Hii imepelekea wataalamu kuunda hardware ambazo ni maalum kwa ajili ya zoezi hili la uchimbaji, kwa maneno mengine hardwere zanye uwezo wa kuchakata Terahashes (T#=10^9) wakati mwingine Petahashes (P#=10^12) za data katika sekunde moja. Hardware hizi zinaitwa "Miners" hapo nadhani kwa kiswahili tutaziita chimbio au labda chimbaji...we amua!

Sababu nyingine kwa nini zoezi hili linafananishwa na uchimbaji wa madini, ni kwa sababu ya kuwepo kwa hifadhi yenye kikomo (limited reserve) ya bitcoin.

Mpaka sasa hifadhi ya bitcoin ulimwenguni mwote ni Milioni 21 tu.Kuwepo kwa hifadhi hii yenye kikomo ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa zianazo sababisha ongezeko la kasi la thamani ya Bitcoin.Chukulia kwa mfano hifadhi ya dhahabu au mafuta ulimwenguni inakaribia kuisha, kupungua wa kiwango cha dhahabu au mafuta kwa wakati wowote ule kutasababisha ongezeko kubwa la bei ya dhahabu au mafuta kwa wakati huo, vivyo hivyo kupungua kwa hifadhi ya Bitcoin.

Jambo jingine, zoezi zima la uchimbaji linahitaji na litumia nishati ya kutosha kabisa ya umeme jambo linalofanya computer za kawaida kua na ufanisi usiotosheleza katika zoezi hili la uchimbaji wa bitcoin.

Ikiwa hardware sahihi zitatumika katika zoezi hili la uchimbaji wa bitcoin na gharama za umeme za eneo ni rafiki kwa zoezi hili faida maradufu ni jambo la hakika kabisa,nazungumza hili kutokana na uzoefu mdogo nilio nao wa karibu mwezi hivi.

Binafsi nimejikita ktk uchimbaji na kwa uzoefu mdogo nilioupata, ninaamini uchimbaji ni njia ya kuaminika kabisa ya kupata na kunufaika na bitcoins.Nafananisha hili na umiliki binafsi wa mashine ya kuchapisha noti au sarafu itakayoingia kwenye mzunguko wa fedha.

Kwa siku 18 ambazo nimekua nikifanya zoezi hili ukiondoa mtaji yaani gharama za kununua unit moja ya uchimbaji, gharama ya umeme na internet nilizowekeza hazizidi $30 na kwa kipindi hiki kifupi ambacho nimeendelea kufanya uchimbaji ingawa si kwa masaa 24 kwa siku au mfululizo kila siku kwa sababu ya changamoto za mazingira yangu nimeweza kuchimba bitcoin 0.01627392BTC sawa na $235 kwa rate ya leo 1BTC=14,728$.Rate hii inatarajiwa kuongezeka maradufu hivyo bei ya Bitcoin kwa sasa ukilinganisha na siku zijazo bado ni rahisi,Mwezi wa nane ilikua ni $6000 hivyo alienunua Bitcoin mwezi huo wa nane anafaidi kila siku Bitcoin invyozidi kuongezeka thamani.

yapo mengi ya kusema lakini haya machache nadhani yanatosha kukushawishi msomaji kujifunza zaidi juu ya bitcoin lakini pia kukushawishi kuanza zoezi hili la uchimbaji mapema kabla hujachelewa.

Kwa watakaopenda kufanya zoezi hili la uchimbaji;

GHARAMA ZA UNIT NZIMA YA UCHIMBAJI WA BITCOIN NI KAMA ZIFUATAZO.

Antminer's S9; 13.5TH $3100@pcs (Chimbaji lenyewe hili)

PSU $150@pcs (transformer ndogo)

4000W Extension $20@pcs

4G SIM Card router $75@pcs (kwa ajili ya internet)

5 ports Splitter $14@pcs (unaweza kusema ni kama extension au multiplug ya internet)

Ikumbukwe kua gharama za Mashine hizi huathiriwa na mambo yafuatayo.

#:Thamani ya Bitcoin inayoongezeka kila kukicha.
#:Uhitaji sokoni unaoongezeka kutokana na ongezeko la thamani ya Bitcoin kila kukicha.
#:Stock ya mashine ambayo huisha mara kutokana na uhitaji mkubwa sokoni unaozidi kwa mbali kabisa utengenezwaji wa mashine hizi za kuchimba Bitcoin.Hili husababisha mashine hizi kuuzwa kwa utaratibu wa kuorder kwanza (Pre-order).

**Mashine za kuchimba sarafu nyingine za mtandaoni zaidi ya Bitcoin kama vile Litecoin, Euthereum...n.k zinapatikana pia, nicheki whatsapp +8613119592149 kwa mawasiliano zaidi.

Hivi ndivyo opareshini yangu ndogo ya uchimbaji inavyoonekana.Mashine ya pili ni ya rafiki ninayomsaidia kuhost.

7ba1618d4f57216effe09647c174232e.jpg

76d523467578a6d84d943f702a009e72.jpg

adfbd5d44e0a698849e11365a207ec6e.jpg
hii kitu zamani niliwaza kuifanya sema kwa umeme wa africa na hasa Tanesco unaweza kuishia kulipia bili tu, hizo mashine zinakula umeme hasa hiyo latest Antimimer S9 nahisi wewe unayefanya mining utakuwa haupo bongo
 
Ndio maana hasa naitaka hiyo na vile vile wamiliki wa mfumo wanajulikana hawa waheshimiwa wa Bitcoin wameamua wao wasijulikane na wala zawadi hawapokei inakuwa ngumu kujua identity yao ingawa hamna ubishi cypocurrency ndio currency ya internet.

Uzuri mwingine wa Ethereum, iko chini sasa, ukiiwahi sasa, ikipanda unapanda nayo sana tu.
 
Juzi nilikuwa nasikiliza BBC World Service kama kawaida yangu.

Kuna dogo mmoja walikuwa wanamuhoji haya mambo ya Bitcoin, yeye alianzisha exchange ya Bitcoin miaka ya mwanzo mwanzo kabisa, kuna wakati a third of all bitcoins zilikuwa zinauzwa na mtandao wake.

Yule dogo alikuja kuwa implicated kwamba kahusika kuwauzia wahalifu Bitcoin.

Sheria za Kimarekani zilivyo kali, mhalifu kashtakiwa, mpaka aliyemuuzia mhalifu Bitcoin naye kashtakiwa, dogo alikuja kufungwa.

Matthew Bannister akamuuliza kama alijua kwamba anawauzia wahalifu, nikafikiri dogo atakanusha, akasema ni kweli alijua.

Ila kamahauna exchange ya kuuza, kuwa implicated ni vigumu, kwa sababu watu wengi mostly wananunua, na hata ukiuza kama mtu mmoja tu asiye na exchange, huna liability kama mtu mwenye exchange.
 
Bitcoin is a bubble they say,halidumu litapasuka muda si mrefu,ila haki ya mungu ningekua na hata million ambayo niko tayari kuipoteza ningenunua.
 
Heshima kwenu wote wakubwa kwa wadogo! Natumai mnaendelea vyema!

Walau kwa DONDOO za hapa na pale kwa wale ambao wangependa kujua zaidi ningependa kuwashirikisha kile ambacho nimejifunza kuhusiana na Bitcoin.

Kwa uzoefu mdogo niliupata toka nimeanza kufuatilia na kupata bitcoins, zipo njia mbili za kupata bitcoins.

Njia ya kwanza ni TRADING yaani kuuza na kununua Biticoin.

Bitcoin ni aina ya sarafu kama ilivyo shilingi au dola,tofuauti yake ni kua yenyewe ni sarafu ya mtandaoni.Hivyo kama jinsi mtu anaponunua Dola kwa Shilingi kwa kutegemea exchange rate ya siku, ndivyo jinsi Bitcoin invyonunuliwa na kuuzwa kwa kutegemea exchange rate ya siku hio.

Faida kubwa ktk trading yaani kuuza na kununua Bitcoin hupatikana pale ambapo mtu ananunua bitcoin msimu ambao bei yake ni rahisi na kuiuza msimu ambapo bei yake inakua imeongezeka.

Njia ya Pili ya kupata bitcoin ni kwa operesheni iliopewa jina la Mining "Uchimbaji".

Hapa Bitcoin inachukuliwa kama jiwe la thamani mfano wa almasi au dhahabu ambazo hupatikana kwa njia ya kuchimba, tafauti ya uchimbaji wa bitcoin ni kua zoezi hili la uchimbaji linafanyika kwa kutatua milinganyo migumu ya mahesabu mtandaoni kwa kutumia computer.

Katika zoezi hili nguvu ya utatuzi wa milinganyo hii ambayo hutegemea na kupimwa na kasi ya computer husika(speed :the Number of bits of information/data that can be processed in a unit second) ndio msingi mkubwa wa uchimbaji, ndio maana computer za kawaida pekee hazitoshi kufanya zoezi hili kwa mafanikio yoyote ya kuridhisha.

Hii imepelekea wataalamu kuunda hardware ambazo ni maalum kwa ajili ya zoezi hili la uchimbaji, kwa maneno mengine hardwere zanye uwezo wa kuchakata Terahashes (T#=10^9) wakati mwingine Petahashes (P#=10^15) za data katika sekunde moja. Hardware hizi zinaitwa "Miners" hapo nadhani kwa kiswahili tutaziita chimbio au labda chimbaji...we amua!

Sababu nyingine kwa nini zoezi hili linafananishwa na uchimbaji wa madini, ni kwa sababu ya kuwepo kwa hifadhi yenye kikomo (limited reserve) ya bitcoin.

Mpaka sasa hifadhi ya bitcoin ulimwenguni mwote ni Milioni 21 tu.Kuwepo kwa hifadhi hii yenye kikomo ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa zianazo sababisha ongezeko la kasi la thamani ya Bitcoin.Chukulia kwa mfano hifadhi ya dhahabu au mafuta ulimwenguni inakaribia kuisha, kupungua wa kiwango cha dhahabu au mafuta kwa wakati wowote ule kutasababisha ongezeko kubwa la bei ya dhahabu au mafuta kwa wakati huo, vivyo hivyo kupungua kwa hifadhi ya Bitcoin.

Jambo jingine, zoezi zima la uchimbaji linahitaji na litumia nishati ya kutosha kabisa ya umeme jambo linalofanya computer za kawaida kua na ufanisi usiotosheleza katika zoezi hili la uchimbaji wa bitcoin.

Ikiwa hardware sahihi zitatumika katika zoezi hili la uchimbaji wa bitcoin na gharama za umeme za eneo ni rafiki kwa zoezi hili faida maradufu ni jambo la hakika kabisa,nazungumza hili kutokana na uzoefu mdogo nilio nao wa karibu mwezi hivi.

Binafsi nimejikita ktk uchimbaji na kwa uzoefu mdogo nilioupata, ninaamini uchimbaji ni njia ya kuaminika kabisa ya kupata na kunufaika na bitcoins.Nafananisha hili na umiliki binafsi wa mashine ya kuchapisha noti au sarafu itakayoingia kwenye mzunguko wa fedha.

Kwa siku 18 ambazo nimekua nikifanya zoezi hili ukiondoa mtaji yaani gharama za kununua unit moja ya uchimbaji, gharama ya umeme na internet nilizowekeza hazizidi $30 na kwa kipindi hiki kifupi ambacho nimeendelea kufanya uchimbaji ingawa si kwa masaa 24 kwa siku au mfululizo kila siku kwa sababu ya changamoto za mazingira yangu nimeweza kuchimba bitcoin 0.01627392BTC sawa na $235 kwa rate ya leo 1BTC=14,728$.Rate hii inatarajiwa kuongezeka maradufu hivyo bei ya Bitcoin kwa sasa ukilinganisha na siku zijazo bado ni rahisi,Mwezi wa nane ilikua ni $6000 hivyo alienunua Bitcoin mwezi huo wa nane anafaidi kila siku Bitcoin invyozidi kuongezeka thamani.

yapo mengi ya kusema lakini haya machache nadhani yanatosha kukushawishi msomaji kujifunza zaidi juu ya bitcoin lakini pia kukushawishi kuanza zoezi hili la uchimbaji mapema kabla hujachelewa.

Kwa watakaopenda kufanya zoezi hili la uchimbaji;

GHARAMA ZA UNIT NZIMA YA UCHIMBAJI WA BITCOIN NI KAMA ZIFUATAZO.

Antminer's S9; 13.5TH $3100@pcs (Chimbaji lenyewe hili)Bei hii ni ya Dec 80/017, bei hii inabadilika kutokana na mabadiliko ya thamani ya BTC.

PSU $150@pcs (transformer ndogo)

4000W Extension $20@pcs

4G SIM Card router $75@pcs (kwa ajili ya internet)

5 ports Splitter $14@pcs (unaweza kusema ni kama extension au multiplug ya internet)

Ikumbukwe kua gharama za Mashine hizi huathiriwa na mambo yafuatayo.

#:Thamani ya Bitcoin inayoongezeka kila kukicha.
#:Uhitaji sokoni unaoongezeka kutokana na ongezeko la thamani ya Bitcoin kila kukicha.
#:Stock ya mashine ambayo huisha mara kutokana na uhitaji mkubwa sokoni unaozidi kwa mbali kabisa utengenezwaji wa mashine hizi za kuchimba Bitcoin.Hili husababisha mashine hizi kuuzwa kwa utaratibu wa kuorder kwanza (Pre-order).

**Mashine za kuchimba sarafu nyingine za mtandaoni zaidi ya Bitcoin kama vile Litecoin, Euthereum...n.k zinapatikana pia, pm me kwa mawasiliano zaidi.

Hivi ndivyo opareshini yangu ndogo ya uchimbaji inavyoonekana.Mashine ya pili ni ya rafiki ninayomsaidia kuhost.

7ba1618d4f57216effe09647c174232e.jpg

76d523467578a6d84d943f702a009e72.jpg

adfbd5d44e0a698849e11365a207ec6e.jpg
mm naitaji
 
Kamari ni hatari kwa Afya yako.
Bora nibaki kwenye ulofa wangu kuliko kujiingiza kwenye mavuno yasiyo halali.
 
Ahsante mimi naomba kujua beo ya kichimbio cha Ethereum. Naiependa zaidi hiyo kwasababu ambazo kwa sasa haziko wazi ila kwa moja kubwa wamiliki wanajulikana ila hii ya Satoshi Nakamoto nitanunua kidogo kidogo. Ila nataka nifocus kwenye Ethereum.
Mkuu ulifanikiwa kumiliki Etherium?
 
kwa ujumla unaweza kufananisha hiki kichimbio na machine/kiwanda kidogo cha kuchapa sarafu, hivyo mapato yako yatategemea jinsi unavyoiruhusu mashine kufanya kazi yake na pia kuihudumia itakapohitaji maintanance, lakini pia One 13.5T# machine kwa mwezi inaweza kukuchimbia kwa wastani 0.1BTC, kazi inabaki kwako kufanya conversion kulingana na rates za siku.

Faida ipo maradufu kwa hakika.Bei ya umeme hapo nyumabani ni fursa kabisa kwa aina hii ya uwekezaji.

Soon 1BTC itafikia $30,000 by tht time sijui kama vichimbio vitakua vinashikika.
Imefika $45,900 watu wanaona ndogo sasa
 
Bitcoin milioni 21 ni pool... Ambapo kila miner fanikiwa kuverify transactions analipwa bitcoin 12.5(kwasasa) kutoka kwenye ile pool ya bitcoin 21M. Mpaka saa bitcoin 16M zimeshavunwa. (Takriban 80% ya pool nzima yaan 21M) hivyo hakuna anaemiliki bitcoin pool. Nikama tunavyosema hakuna anaemiliki madini... Yoyote atakaewekeza katika uchimbaji basi atapata madini ambayo ndio malipo yake. Hivyo naww ukiwekeza katika uchimbaji wa BTC utalipwa bitcoin kutoka kwenye pool ya 21M BTC (japo sasa zimebaki takriban 4.5M BTC kwenye pool) ikumbukwe BTC ziko fixed amount. Hakuna yoyote atakaeweza kuongeza pool capacity. Hivyo zikiisha katika pool basi BTC itakuwa ghali sana... Kwani mzunguko utakuwa mkubwa na miners wataanza kucharge gharama za transactions kutoka kwa watumiaji(kwasasa transaction ni sawa na bure) hope nimejieleza vzr... Nakaribisha maswali....
Duuuh sasa miner reward ni 6.25BTC
 
Uzuri mwingine wa Ethereum, iko chini sasa, ukiiwahi sasa, ikipanda unapanda nayo sana tu.
Daaah mkuu,kuna watu pia watakuja kuikuta ADA ipo USD 300,TRON ipo $ 10 ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom