Pata bitcoin kwa njia ya uchimbaji

Pata bitcoin kwa njia ya uchimbaji

Bitcoin milioni 21 ni pool... Ambapo kila miner fanikiwa kuverify transactions analipwa bitcoin 12.5(kwasasa) kutoka kwenye ile pool ya bitcoin 21M. Mpaka saa bitcoin 16M zimeshavunwa. (Takriban 80% ya pool nzima yaan 21M) hivyo hakuna anaemiliki bitcoin pool. Nikama tunavyosema hakuna anaemiliki madini... Yoyote atakaewekeza katika uchimbaji basi atapata madini ambayo ndio malipo yake. Hivyo naww ukiwekeza katika uchimbaji wa BTC utalipwa bitcoin kutoka kwenye pool ya 21M BTC (japo sasa zimebaki takriban 4.5M BTC kwenye pool) ikumbukwe BTC ziko fixed amount. Hakuna yoyote atakaeweza kuongeza pool capacity. Hivyo zikiisha katika pool basi BTC itakuwa ghali sana... Kwani mzunguko utakuwa mkubwa na miners wataanza kucharge gharama za transactions kutoka kwa watumiaji(kwasasa transaction ni sawa na bure) hope nimejieleza vzr... Nakaribisha maswali....
Duh, aisee,
Nadhani hapa shule inahitajika zaidi, maana naona kama ndio nazidi kutoelewa kuliko kuelewa.
Hizo BTC 21Mil alizi-set nani sasa??
And why 21Mil only??
The way alivyoweka hizo 21Mil za mwanzo why asiziongeze zaidi kama zimeshavunwa 80% na anajua zikiisha italeta shida?
Na ni nani huyo mtu??
 
Duh, aisee,
Nadhani hapa shule inahitajika zaidi, maana naona kama ndio nazidi kutoelewa kuliko kuelewa.
Hizo BTC 21Mil alizi-set nani sasa??
And why 21Mil only??
The way alivyoweka hizo 21Mil za mwanzo why asiziongeze zaidi kama zimeshavunwa 80% na anajua zikiisha italeta shida?
Na ni nani huyo mtu??
Okay, kuna maelezo marefu kdg pamoja na mahesabu ndani yake. Kwa kifupi, kila baada ya saa moja block 6 huvumbuliwa kwenye bitcoin. Zidisha mara saa 24 za siku, zidisha mara siku 365 za mwaka alafu zidisha mara miaka minne ya blocl reward. (*block reward ni kiasi cha malipo in BTC ambazo miner wanalipwa. Hivyo kila baada ya miaka minne (4) block reward inapungua kwa asilimia 50. So ilianza kwa malipo ya BTC 50 kwa kila transaction mwaka 2008, ikapungua kuwa 25BTC mwaka 2012, ikapungua kuwa 12.5 mwaka 2016, itapungua kuwa 6.25, mwaka 2020 nk) hivyo kufanya jumla ya kuwa 210240. (Yaan 6x24x365x4)

Ukijimlisha hizo reward yaan 50+25+12.5+.... Mpka ziishe utapata jumla ya 100. So 210240x100 utapata 21,024,000.
 
Mtoa Mada nauliza kati ya blockchain na localbitcoin ipo iko poa sana?
Unaweza kua na account katika zote mbili, Lakini Lacalbitcoin ndio imepenyeza zaidi kuliko blockchain, siisomi blockchain kipande hii ila localbitcoin inasomeka vzr tuu
 
Kama Idadi ya Bitcoins iko limited (21mil), je hizi zote 21mil ziko kiwa watu/taasisi??
Mimi nikianza kuzichimba napewa Bitcoins za nani??
Kanuni ya Kihasibu inasema kwenye any Debit transaction, there must be a correspondent Credit side for the same amount (Double Entry system), sasa mimi nikichimba nikapata nani atakua anapungua??
Mfumo wa kiteknolojia umejengwa ambao wenyewe unarespond to the stronger computational power;the computational power inturn is determined by time and electricity kwa maneno mengine Fedha; Bitcoin as a reward is that response; niufananishe huu mfumo na electronic games, the score depends on whether someone plays or not; a score is a result of playing the game.

Games zinatengenezwa kua na kiwango fulani cha mwisho cha score, lakini score inapatikana tuu pale mtu anapocheza. Vivyo hivyo na system ya bitcoin no one has all the bitcoins,hata mvumbuzi mwenyewe, Mvumbuzi/wavumbuzi wamefanya kazi ya kujenga mfumo tuu peke yake.BTC mpya kwenye mzunguko hutengenezwa tuu mtu anapofanya hili zoezi la uchimbaji, otherwise wavumbuzi kumiliki BTC's would destort the whole purpose of bitcoin i.e decentralization of currency.

Hivyo ni mfumo ambao umejengwa kwa namna ambavyo Matokeo/score /reward inatolewa pale tuu mtu anaposhiriki katika zoezi hili la uchimbaji. Hivi ndivyo uchimbaji unavyofanya kazi mkuu.

Nadhani hili suala la limit ya hizi BTC's hata kichumi inaleta maana hasa ukizingatia historia ya fedha...tatizo kubwa la uchumi tulilo nalo sasa hapa duniani ni kuongezwa kwa noti kwenye mzunguko wa fedha zisizo na Back up yoyote ya thamani/dhahabu.Nadhani hii ni fani yako kutokana maandiko yako hivyo nadhani unaelewa zaidi...wanapozungumzia financial bubble, mimi hua nafikiri kama sio pekee hii ni mojawapo ya sababu za hicho kitu kinachoitwa financial bubble, fedha zisizo na back up ya thamani.

Swali lako la pili Uchimbaji sio transaction, Mining ni kitendo cha kurecord bitcoin transactions katika kitabu cha historia ya trasactions zinazofanyika kwa kutumia bitcoins. Kitabu hiki ambacho kila mtu mwenye computer anaweza kuandika (kwa sasa uandishi wenye faida ukiwa umejiunga na wengine wanaofanya huo uandishi~a pool) tofauti yake na mfumo wa sasa wa kibank kitabu hiki ni cha kadamnasi/ public, mfumo wa kiteknolojia/ Protocols zimejengwa ndani ya mfumo huo, (mojawapo ndio kama hio ya ulazima wa kutumia Umeme na Muda=fedha) zinazowezesha uandishi kukubalika au kutokubalika...hili ni kwa lengo la kudhibiti conterfeiting kutokana na kwamba kila mtu na sio benki peke yake ana fursa ya kuandika kitabu hiki cha historia ya transactions.

Undishi wa historia hio ya transactions unapothibitishwa kufanyika ktk protocol zilizojengwa ndani ya mfumo huu uchimbaji/uandishi unazawadiwa BTC's.

Ukishachimba unaweza kufanya transactions yoyote upendayo.Tokea Hapa sasa naamini kanuni zote ya fedha na mabadilishano ya thamani zinafuatwa kama kawaida kabisa.

Kwa maelezo haya hope atleast unausoma mchezo kwa namna fulani.

Kumradhi kwa kuchanganya lugha.
 
Hii ilikuwa Nov 29, 2017
 

Attachments

  • IMG_20171129_194219.jpg
    IMG_20171129_194219.jpg
    61 KB · Views: 48
Loo leo nimeingiza kitu muhmu sana maishan mwangu hili somo nilkuwa nafuatilia sana lkn ckuwa nmelielewa vema leo nimefumbuka pakubwa asante sana mkuu
 
Sasa hpo mkuu nmepiga maheaabu hasa hyo miner bei ghal sana $3100 du parefu balaa
 
Heshima kwenu wote wakubwa kwa wadogo! Natumai mnaendelea vyema!

Walau kwa DONDOO za hapa na pale kwa wale ambao wangependa kujua zaidi ningependa kuwashirikisha kile ambacho nimejifunza kuhusiana na Bitcoin.

Kwa uzoefu mdogo niliupata toka nimeanza kufuatilia na kupata bitcoins, zipo njia mbili za kupata bitcoins.

Njia ya kwanza ni TRADING yaani kuuza na kununua Biticoin.

Bitcoin ni aina ya sarafu kama ilivyo shilingi au dola,tofuauti yake ni kua yenyewe ni sarafu ya mtandaoni.Hivyo kama jinsi mtu anaponunua Dola kwa Shilingi kwa kutegemea exchange rate ya siku, ndivyo jinsi Bitcoin invyonunuliwa na kuuzwa kwa kutegemea exchange rate ya siku hio.

Faida kubwa ktk trading yaani kuuza na kununua Bitcoin hupatikana pale ambapo mtu ananunua bitcoin msimu ambao bei yake ni rahisi na kuiuza msimu ambapo bei yake inakua imeongezeka.

Njia ya Pili ya kupata bitcoin ni kwa operesheni iliopewa jina la Mining "Uchimbaji".

Hapa Bitcoin inachukuliwa kama jiwe la thamani mfano wa almasi au dhahabu ambazo hupatikana kwa njia ya kuchimba, tafauti ya uchimbaji wa bitcoin ni kua zoezi hili la uchimbaji linafanyika kwa kutatua milinganyo migumu ya mahesabu mtandaoni kwa kutumia computer.

Katika zoezi hili nguvu ya utatuzi wa milinganyo hii ambayo hutegemea na kupimwa na kasi ya computer husika(speed :the Number of bits of information/data that can be processed in a unit second) ndio msingi mkubwa wa uchimbaji, ndio maana computer za kawaida pekee hazitoshi kufanya zoezi hili kwa mafanikio yoyote ya kuridhisha.

Hii imepelekea wataalamu kuunda hardware ambazo ni maalum kwa ajili ya zoezi hili la uchimbaji, kwa maneno mengine hardwere zanye uwezo wa kuchakata Terahashes (T#=10^9) wakati mwingine Petahashes (P#=10^12) za data katika sekunde moja. Hardware hizi zinaitwa "Miners" hapo nadhani kwa kiswahili tutaziita chimbio au labda chimbaji...we amua!

Sababu nyingine kwa nini zoezi hili linafananishwa na uchimbaji wa madini, ni kwa sababu ya kuwepo kwa hifadhi yenye kikomo (limited reserve) ya bitcoin.

Mpaka sasa hifadhi ya bitcoin ulimwenguni mwote ni Milioni 21 tu.Kuwepo kwa hifadhi hii yenye kikomo ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa zianazo sababisha ongezeko la kasi la thamani ya Bitcoin.Chukulia kwa mfano hifadhi ya dhahabu au mafuta ulimwenguni inakaribia kuisha, kupungua wa kiwango cha dhahabu au mafuta kwa wakati wowote ule kutasababisha ongezeko kubwa la bei ya dhahabu au mafuta kwa wakati huo, vivyo hivyo kupungua kwa hifadhi ya Bitcoin.

Jambo jingine, zoezi zima la uchimbaji linahitaji na litumia nishati ya kutosha kabisa ya umeme jambo linalofanya computer za kawaida kua na ufanisi usiotosheleza katika zoezi hili la uchimbaji wa bitcoin.

Ikiwa hardware sahihi zitatumika katika zoezi hili la uchimbaji wa bitcoin na gharama za umeme za eneo ni rafiki kwa zoezi hili faida maradufu ni jambo la hakika kabisa,nazungumza hili kutokana na uzoefu mdogo nilio nao wa karibu mwezi hivi.

Binafsi nimejikita ktk uchimbaji na kwa uzoefu mdogo nilioupata, ninaamini uchimbaji ni njia ya kuaminika kabisa ya kupata na kunufaika na bitcoins.Nafananisha hili na umiliki binafsi wa mashine ya kuchapisha noti au sarafu itakayoingia kwenye mzunguko wa fedha.

Kwa siku 18 ambazo nimekua nikifanya zoezi hili ukiondoa mtaji yaani gharama za kununua unit moja ya uchimbaji, gharama ya umeme na internet nilizowekeza hazizidi $30 na kwa kipindi hiki kifupi ambacho nimeendelea kufanya uchimbaji ingawa si kwa masaa 24 kwa siku au mfululizo kila siku kwa sababu ya changamoto za mazingira yangu nimeweza kuchimba bitcoin 0.01627392BTC sawa na $235 kwa rate ya leo 1BTC=14,728$.Rate hii inatarajiwa kuongezeka maradufu hivyo bei ya Bitcoin kwa sasa ukilinganisha na siku zijazo bado ni rahisi,Mwezi wa nane ilikua ni $6000 hivyo alienunua Bitcoin mwezi huo wa nane anafaidi kila siku Bitcoin invyozidi kuongezeka thamani.

yapo mengi ya kusema lakini haya machache nadhani yanatosha kukushawishi msomaji kujifunza zaidi juu ya bitcoin lakini pia kukushawishi kuanza zoezi hili la uchimbaji mapema kabla hujachelewa.

Kwa watakaopenda kufanya zoezi hili la uchimbaji;

GHARAMA ZA UNIT NZIMA YA UCHIMBAJI WA BITCOIN NI KAMA ZIFUATAZO.

Antminer's S9; 13.5TH $3100@pcs (Chimbaji lenyewe hili)

PSU $150@pcs (transformer ndogo)

4000W Extension $20@pcs

4G SIM Card router $75@pcs (kwa ajili ya internet)

5 ports Splitter $14@pcs (unaweza kusema ni kama extension au multiplug ya internet)

Ikumbukwe kua gharama za Mashine hizi huathiriwa na mambo yafuatayo.

#:Thamani ya Bitcoin inayoongezeka kila kukicha.
#:Uhitaji sokoni unaoongezeka kutokana na ongezeko la thamani ya Bitcoin kila kukicha.
#:Stock ya mashine ambayo huisha mara kutokana na uhitaji mkubwa sokoni unaozidi kwa mbali kabisa utengenezwaji wa mashine hizi za kuchimba Bitcoin.Hili husababisha mashine hizi kuuzwa kwa utaratibu wa kuorder kwanza (Pre-order).

**Mashine za kuchimba sarafu nyingine za mtandaoni zaidi ya Bitcoin kama vile Litecoin, Euthereum...n.k zinapatikana pia, nicheki whatsapp +8613119592149 kwa mawasiliano zaidi.

Hivi ndivyo opareshini yangu ndogo ya uchimbaji inavyoonekana.Mashine ya pili ni ya rafiki ninayomsaidia kuhost.

7ba1618d4f57216effe09647c174232e.jpg


76d523467578a6d84d943f702a009e72.jpg


adfbd5d44e0a698849e11365a207ec6e.jpg
Na vip mtu akihitaji anapataje na atawezaje kuvitumia
 
Ahsante mimi naomba kujua beo ya kichimbio cha Ethereum. Naiependa zaidi hiyo kwasababu ambazo kwa sasa haziko wazi ila kwa moja kubwa wamiliki wanajulikana ila hii ya Satoshi Nakamoto nitanunua kidogo kidogo. Ila nataka nifocus kwenye Ethereum.
Uzuri mwingine wa Ethereum, iko chini sasa, ukiiwahi sasa, ikipanda unapanda nayo sana tu.
 
Sasa hpo mkuu nmepiga maheaabu hasa hyo miner bei ghal sana $3100 du parefu balaa
Sasa mkuu kakwambia katika muda mfupi tu karudisha karibu 10% ya hiyo miner, tena si kwa ku mine 24/7.

Kulikuwa na wakati mining ilikuwa haina deal (mgano bitcoin ilipokuwa under $600) ila bei inavyopanda ndivyo mining inavyokuwa deal.
 
Sasa hpo mkuu nmepiga maheaabu hasa hyo miner bei ghal sana $3100 du parefu balaa
Duuh asee ndugu hii bei ni outdated tunapozungumza sasa. Bei imeshafika $3,650 sasa.
 
Back
Top Bottom