Pata bitcoin kwa njia ya uchimbaji

Pata bitcoin kwa njia ya uchimbaji

Tanzaone

Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
70
Reaction score
53
Heshima kwenu wote wakubwa kwa wadogo! Natumai mnaendelea vyema!

Walau kwa DONDOO za hapa na pale kwa wale ambao wangependa kujua zaidi ningependa kuwashirikisha kile ambacho nimejifunza kuhusiana na Bitcoin.

Kwa uzoefu mdogo niliupata toka nimeanza kufuatilia na kupata bitcoins, zipo njia mbili za kupata bitcoins.

Njia ya kwanza ni TRADING yaani kuuza na kununua Biticoin.

Bitcoin ni aina ya sarafu kama ilivyo shilingi au dola,tofuauti yake ni kua yenyewe ni sarafu ya mtandaoni.Hivyo kama jinsi mtu anaponunua Dola kwa Shilingi kwa kutegemea exchange rate ya siku, ndivyo jinsi Bitcoin invyonunuliwa na kuuzwa kwa kutegemea exchange rate ya siku hio.

Faida kubwa ktk trading yaani kuuza na kununua Bitcoin hupatikana pale ambapo mtu ananunua bitcoin msimu ambao bei yake ni rahisi na kuiuza msimu ambapo bei yake inakua imeongezeka.

Njia ya Pili ya kupata bitcoin ni kwa operesheni iliopewa jina la Mining "Uchimbaji".

Hapa Bitcoin inachukuliwa kama jiwe la thamani mfano wa almasi au dhahabu ambazo hupatikana kwa njia ya kuchimba, tafauti ya uchimbaji wa bitcoin ni kua zoezi hili la uchimbaji linafanyika kwa kutatua milinganyo migumu ya mahesabu mtandaoni kwa kutumia computer.

Katika zoezi hili nguvu ya utatuzi wa milinganyo hii ambayo hutegemea na kupimwa na kasi ya computer husika(speed :the Number of bits of information/data that can be processed in a unit second) ndio msingi mkubwa wa uchimbaji, ndio maana computer za kawaida pekee hazitoshi kufanya zoezi hili kwa mafanikio yoyote ya kuridhisha.

Hii imepelekea wataalamu kuunda hardware ambazo ni maalum kwa ajili ya zoezi hili la uchimbaji, kwa maneno mengine hardwere zanye uwezo wa kuchakata Terahashes (T#=10^9) wakati mwingine Petahashes (P#=10^15) za data katika sekunde moja. Hardware hizi zinaitwa "Miners" hapo nadhani kwa kiswahili tutaziita chimbio au labda chimbaji...we amua!

Sababu nyingine kwa nini zoezi hili linafananishwa na uchimbaji wa madini, ni kwa sababu ya kuwepo kwa hifadhi yenye kikomo (limited reserve) ya bitcoin.

Mpaka sasa hifadhi ya bitcoin ulimwenguni mwote ni Milioni 21 tu.Kuwepo kwa hifadhi hii yenye kikomo ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa zianazo sababisha ongezeko la kasi la thamani ya Bitcoin.Chukulia kwa mfano hifadhi ya dhahabu au mafuta ulimwenguni inakaribia kuisha, kupungua wa kiwango cha dhahabu au mafuta kwa wakati wowote ule kutasababisha ongezeko kubwa la bei ya dhahabu au mafuta kwa wakati huo, vivyo hivyo kupungua kwa hifadhi ya Bitcoin.

Jambo jingine, zoezi zima la uchimbaji linahitaji na litumia nishati ya kutosha kabisa ya umeme jambo linalofanya computer za kawaida kua na ufanisi usiotosheleza katika zoezi hili la uchimbaji wa bitcoin.

Ikiwa hardware sahihi zitatumika katika zoezi hili la uchimbaji wa bitcoin na gharama za umeme za eneo ni rafiki kwa zoezi hili faida maradufu ni jambo la hakika kabisa,nazungumza hili kutokana na uzoefu mdogo nilio nao wa karibu mwezi hivi.

Binafsi nimejikita ktk uchimbaji na kwa uzoefu mdogo nilioupata, ninaamini uchimbaji ni njia ya kuaminika kabisa ya kupata na kunufaika na bitcoins.Nafananisha hili na umiliki binafsi wa mashine ya kuchapisha noti au sarafu itakayoingia kwenye mzunguko wa fedha.

Kwa siku 18 ambazo nimekua nikifanya zoezi hili ukiondoa mtaji yaani gharama za kununua unit moja ya uchimbaji, gharama ya umeme na internet nilizowekeza hazizidi $30 na kwa kipindi hiki kifupi ambacho nimeendelea kufanya uchimbaji ingawa si kwa masaa 24 kwa siku au mfululizo kila siku kwa sababu ya changamoto za mazingira yangu nimeweza kuchimba bitcoin 0.01627392BTC sawa na $235 kwa rate ya leo 1BTC=14,728$.Rate hii inatarajiwa kuongezeka maradufu hivyo bei ya Bitcoin kwa sasa ukilinganisha na siku zijazo bado ni rahisi,Mwezi wa nane ilikua ni $6000 hivyo alienunua Bitcoin mwezi huo wa nane anafaidi kila siku Bitcoin invyozidi kuongezeka thamani.

yapo mengi ya kusema lakini haya machache nadhani yanatosha kukushawishi msomaji kujifunza zaidi juu ya bitcoin lakini pia kukushawishi kuanza zoezi hili la uchimbaji mapema kabla hujachelewa.

Kwa watakaopenda kufanya zoezi hili la uchimbaji;

GHARAMA ZA UNIT NZIMA YA UCHIMBAJI WA BITCOIN NI KAMA ZIFUATAZO.

Antminer's S9; 13.5TH $3100@pcs (Chimbaji lenyewe hili)Bei hii ni ya Dec 80/017, bei hii inabadilika kutokana na mabadiliko ya thamani ya BTC.

PSU $150@pcs (transformer ndogo)

4000W Extension $20@pcs

4G SIM Card router $75@pcs (kwa ajili ya internet)

5 ports Splitter $14@pcs (unaweza kusema ni kama extension au multiplug ya internet)

Ikumbukwe kua gharama za Mashine hizi huathiriwa na mambo yafuatayo.

#:Thamani ya Bitcoin inayoongezeka kila kukicha.
#:Uhitaji sokoni unaoongezeka kutokana na ongezeko la thamani ya Bitcoin kila kukicha.
#:Stock ya mashine ambayo huisha mara kutokana na uhitaji mkubwa sokoni unaozidi kwa mbali kabisa utengenezwaji wa mashine hizi za kuchimba Bitcoin.Hili husababisha mashine hizi kuuzwa kwa utaratibu wa kuorder kwanza (Pre-order).

**Mashine za kuchimba sarafu nyingine za mtandaoni zaidi ya Bitcoin kama vile Litecoin, Euthereum...n.k zinapatikana pia, pm me kwa mawasiliano zaidi.

Hivi ndivyo opareshini yangu ndogo ya uchimbaji inavyoonekana.Mashine ya pili ni ya rafiki ninayomsaidia kuhost.

7ba1618d4f57216effe09647c174232e.jpg


76d523467578a6d84d943f702a009e72.jpg


adfbd5d44e0a698849e11365a207ec6e.jpg
 
Ahsante mimi naomba kujua beo ya kichimbio cha Ethereum. Naiependa zaidi hiyo kwasababu ambazo kwa sasa haziko wazi ila kwa moja kubwa wamiliki wanajulikana ila hii ya Satoshi Nakamoto nitanunua kidogo kidogo. Ila nataka nifocus kwenye Ethereum.
 
Nikafikiri kuna Migodi kama ya Buzwagi na Tanzanite ambako watu wanachimba Bitcoin
 
No one is regulating Bitcoin, hichi ndicho kinachontia shaka. Wala hizo bitcoin wallets hazina dhamana, wakiamua kuzichukua coin zako huna pa kulia. Wacha niendelee na pesa za karatasi tu
 
Ahsante mimi naomba kujua beo ya kichimbio cha Ethereum. Naiependa zaidi hiyo kwasababu ambazo kwa sasa haziko wazi ila kwa moja kubwa wamiliki wanajulikana ila hii ya Satoshi Nakamoto nitanunua kidogo kidogo. Ila nataka nifocus kwenye Ethereum.
Samahani mkuu kwa sasa sina hii connection, Labda baada muda fulani hivi ila kwa kwa sasa vichimbio vya Litecoin na Bitoin vinaweza kupatikana.
 
Mkuu kwa Bei hizo naweza nikatoa Bitcoin ngapi?
kwa ujumla unaweza kufananisha hiki kichimbio na machine/kiwanda kidogo cha kuchapa sarafu, hivyo mapato yako yatategemea jinsi unavyoiruhusu mashine kufanya kazi yake na pia kuihudumia itakapohitaji maintanance, lakini pia One 13.5T# machine kwa mwezi inaweza kukuchimbia kwa wastani 0.1BTC, kazi inabaki kwako kufanya conversion kulingana na rates za siku.

Faida ipo maradufu kwa hakika.Bei ya umeme hapo nyumabani ni fursa kabisa kwa aina hii ya uwekezaji.

Soon 1BTC itafikia $30,000 by tht time sijui kama vichimbio vitakua vinashikika.
 
No one is regulating Bitcoin, hichi ndicho kinachontia shaka. Wala hizo bitcoin wallets hazina dhamana, wakiamua kuzichukua coin zako huna pa kulia. Wacha niendelee na pesa za karatasi tu
Suala la security ya investment kama hii ni jukumu la mmiliki wa wallet....zipo njia mbili za kusecure ur BTC wallet...moja ni Chaguo la wallet analofanya muhusika, wallet inayopendekezwa sana inaitwa Blockchain wallet (hii wanaitumia zaidi wamarekani)....kwa kufanya backing up mtumiaji peke yake anakua na control ya kufunga na kufungua wallet yake at will, hii ni feature muhimu kwa ajili ya kuilinda wallet ya mtumiaji, zipo wallet zenye feature hii na zipo zisizo na hii feature.

Njia ya pili na salama zaidi ni kuhifadhi mapato ya account yako kwenye hardware inayoonekana kama USB inaitwa ledger, unaweza kutumia njia mojawapo kati ya hizi ya pili ikiwa na usalama wa hakika zaidi.Njia hii inapendekezwa hasa zaidi kwa watumiaji wa wallets zisizo na feature hii ya kuback up ur wallet, mfano Xapo (ambayo ni maarufu nje ya marekani, binafsi hadi sasa natumia Xapo).

Suala la kumjua au kutokumjua ni nani anae control BTC hili kwa kweli sijui linachoathiri kwa sababu wataalam wa teknolojia wanasema itachukua mamilioni ya miaka kuhack Blockchain technology ambayo ndio teknolojia inayoibeba BTC....ndio maana mvumbuzi wa teknolojia hii aidha mtu mmoja au kundi la watu hawajafahamika mpaka sasa.

Kukosekana kwa usalama sana sana itakua ni kwenye makampuni yanayofanyabiashara hii ya BTC kwa maana ya wallets na makampuni yanayowezesha transactions mbali mbali, na usalama ni kama nilivyo eleza hapo juu.
 
...
...
Mpaka sasa hifadhi ya bitcoin ulimwenguni mwote ni Milioni 21 tu.Kuwepo kwa hifadhi hii yenye kikomo ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa zianazo sababisha ongezeko la kasi la thamani ya Bitcoin.Chukulia kwa mfano hifadhi ya dhahabu au mafuta ulimwenguni inakaribia kuisha, kupungua wa kiwango cha dhahabu au mafuta kwa wakati wowote ule kutasababisha ongezeko kubwa la bei ya dhahabu au mafuta kwa wakati huo, vivyo hivyo kupungua kwa hifadhi ya Bitcoin.
...
...
Kama Idadi ya Bitcoins iko limited (21mil), je hizi zote 21mil ziko kiwa watu/taasisi??
Mimi nikianza kuzichimba napewa Bitcoins za nani??
Kanuni ya Kihasibu inasema kwenye any Debit transaction, there must be a correspondent Credit side for the same amount (Double Entry system), sasa mimi nikichimba nikapata nani atakua anapungua??
 
Maswali kwa mleta maada??

Naomba nichanganulie bei za machine hizo na aina yake na tofauti zake na je ipi ni bora ukiipata..

Je? Nikipata hiyo machine vitu vipi nahitaji kuwa navyo zaidi ya bitcoin account??

Na uingizaji wa pesa upoje kulingana na maelezo ni lazima uweke pesa kwanza ndo uanze kutumia??

Bei zake niwekee kwa tsh
 
Kama Idadi ya Bitcoins iko limited (21mil), je hizi zote 21mil ziko kiwa watu/taasisi??
Mimi nikianza kuzichimba napewa Bitcoins za nani??
Kanuni ya Kihasibu inasema kwenye any Debit transaction, there must be a correspondent Credit side for the same amount (Double Entry system), sasa mimi nikichimba nikapata nani atakua anapungua??
Bitcoin milioni 21 ni pool... Ambapo kila miner fanikiwa kuverify transactions analipwa bitcoin 12.5(kwasasa) kutoka kwenye ile pool ya bitcoin 21M. Mpaka saa bitcoin 16M zimeshavunwa. (Takriban 80% ya pool nzima yaan 21M) hivyo hakuna anaemiliki bitcoin pool. Nikama tunavyosema hakuna anaemiliki madini... Yoyote atakaewekeza katika uchimbaji basi atapata madini ambayo ndio malipo yake. Hivyo naww ukiwekeza katika uchimbaji wa BTC utalipwa bitcoin kutoka kwenye pool ya 21M BTC (japo sasa zimebaki takriban 4.5M BTC kwenye pool) ikumbukwe BTC ziko fixed amount. Hakuna yoyote atakaeweza kuongeza pool capacity. Hivyo zikiisha katika pool basi BTC itakuwa ghali sana... Kwani mzunguko utakuwa mkubwa na miners wataanza kucharge gharama za transactions kutoka kwa watumiaji(kwasasa transaction ni sawa na bure) hope nimejieleza vzr... Nakaribisha maswali....
 
Kama Idadi ya Bitcoins iko limited (21mil), je hizi zote 21mil ziko kiwa watu/taasisi??
Mimi nikianza kuzichimba napewa Bitcoins za nani??
Kanuni ya Kihasibu inasema kwenye any Debit transaction, there must be a correspondent Credit side for the same amount (Double Entry system), sasa mimi nikichimba nikapata nani atakua anapungua??
Swali la msingi kabisa, tunahitaji majibu hapa mleta mada.

Bitcoin is real, but bitcoin mining doesn't make much sense.

Bitcoin ni biashara ambayo ili upate bitcoins lazima kue na mtu anaeuza bitcoins just like stocks and forex.

Umesema kiasi cha bitcoins kiko fixed (21 mil), Sasa hizi unazochimba zinatoka kwa nani?

Hebu tupe darasa mkuu!
 
Back
Top Bottom