Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Passport zaidi ya 600 zipo makao makuu ya uhamiaji Kurasini na hazijachukuliwa na wenyewe.
Pasi hizo pamoja na zile za Afrika Mashariki nyingi ziliombwa kati ya mwaka 2005 na mwaka 2015.
Katika siku za hivi karibuni idara ya uhamiaji imetisitsha zoezi la utoaji pasi hadi hii "backlog" ya hizi zilizo tayari ziweze kuhakikiwa na kujulikana nani ni wamiliki wake.
Hivyo kama una mtu unamfahamu au ndugu, jamaa au rafiki , basi unaweza kumjulisha utakapoona jina lake katika orodha iliyo katika link hii- http://immigration.go.tz/PASIPOTI DSM.pdf
Pia ipo orodha ya passport 17 za waombaji wa kutoka mkoa wa Mbeya ambazo inapatikana hapa: http://immigration.go.tz/ORODHA YA PASIPOTI MBEYA.pdf