Wasalaam, mwandishi na mwanasheria pascal mayalla aliwahi kuandika makala 'je bunge letu linajipendekeza'? Hii ilikua mwaka jana 2018. Baada ya makala hii kama kawaida mh spika job ndugai alifoka na kusema bwana mayalla amelidhalilisha bunge hivyo aliitwa kujieleza.
Yanayotokea leo kwa prof assad ni yaleyale yaliomtukea bwana mayalla, tofauti ni moja tu kwamba prof assad amelikashifu bunge akiwa nje ya nchi ila bwana mayalla alifanya hivyo akiwa ndani ya nchi.
Ni vema kutafakari swala la msingi(fact inissue) , je alichokisema prof assad akiwa nje ya nchi kwamba "bunge la Tanzania ni dhaifu"je ni uongo? au ni ukweli? Nani hasa anaonewa hapa, ni spika, bunge, au prof assad? Binafsi naamini kwenye ukweli uongo hujitenga hivyo navuta subra.