Pascal mayalla: je bunge linajipendekeza?

Pascal mayalla: je bunge linajipendekeza?

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
4,523
Reaction score
4,722
Wasalaam, mwandishi na mwanasheria pascal mayalla aliwahi kuandika makala 'je bunge letu linajipendekeza'? Hii ilikua mwaka jana 2018. Baada ya makala hii kama kawaida mh spika job ndugai alifoka na kusema bwana mayalla amelidhalilisha bunge hivyo aliitwa kujieleza.

Yanayotokea leo kwa prof assad ni yaleyale yaliomtukea bwana mayalla, tofauti ni moja tu kwamba prof assad amelikashifu bunge akiwa nje ya nchi ila bwana mayalla alifanya hivyo akiwa ndani ya nchi.

Ni vema kutafakari swala la msingi(fact inissue) , je alichokisema prof assad akiwa nje ya nchi kwamba "bunge la Tanzania ni dhaifu"je ni uongo? au ni ukweli? Nani hasa anaonewa hapa, ni spika, bunge, au prof assad? Binafsi naamini kwenye ukweli uongo hujitenga hivyo navuta subra.
 
Ndugai alisema wanaokosoa bunge ni wengi na wengine kama kina pascal waliitwa kufafanua tuhuma zao.Hata Pascal ana kinga ya kikatiba ya kitoa maoni kama yeye binafsi au mwandishi lakini alihojiwa kufafanua kauli yake.
 
pascal mayalla sio hitimisho na yeye yupo mlimani city samaki samaki anakula bisi akiangila kombe la mapinduzi kati ya CAG vs Spika wa bunge
 
Wasalaam, mwandishi na mwanasheria pascal mayalla aliwahi kuandika makala 'je bunge letu linajipendekeza'? Hii ilikua mwaka jana 2018. Baada ya makala hii kama kawaida mh spika job ndugai alifoka na kusema bwana mayalla amelidhalilisha bunge hivyo aliitwa kujieleza.
Mkuu Subira the princess, kiukweli jf ni kubwa!, huwezi amini, hili bandiko ndio nikutana nalo leo!.
Thanks, ubarikiwe.
P
 
Back
Top Bottom