Pasaka: Asili, umuhimu wake na tamaduni zetu

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
PASAKA NI NINI?

Pasaka ilianza lini na nani?, Inamaanisha nini?

Kutoka 12:1
BWANA akanena na Musa, na Haruni katika nchi ya Misri akawaambia, Mezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.

Kumbukumbu la Torati 16:1 Na ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki;

Tangu wakati wa kuanzishwa kwa Sheria za Musa, utaratibu wa kuhesa miezi uliojulikana kwa Wayahudi ulikuwa ni ule wa Miandanmo ya Mwezi lakini ilihusiana na mwelekeo wa machweo ya jua. Utaratibu wa mzunguko hadi kufikia siku za maadhimisho ya sikukuu za kidini ilitegemea sana na miandamo ya mwezi. Mwaka wa kidini ulianza katika kipindi kinachokaribiana na kile cha usiku na mchana kuwa na muda sawa katika mzunguko wa jua linapopita katikati ya mstari wa Ikweta, yapata kama tarehe 21 Marchi.

Utaratibu wa kuhesabu mwanzo wa mwezi ulianzia na mwandamo wa mwezi mpya. Kwa maneno mengine ni kwamba ulianzia katika maadhimisho ya mwandamo wa mwezi mpya kwa maneno mengine ni kwamba, mwaka ulianzia katika muandamo wa mwezi mpya uliofuatia mwanzo wa majira ya baridi.

Kuna mambo ya kupendeza kuyajua kuhusiana na hali hii. Inaonekana kwamba dunia iliumbwa katika kipindi hiki cha majira ya baridi wakati wa kipindi kile cha Uumbaji.

Pia baada ya gharika kuu, Nuhu alifungua mlango wa Safina na kutoka kuanza maisha mapya kwenye Ulimwengu Mpya katika kipindi hiki cha baridi cha mwaka ule. Wana wa Israeli pia walitoka kutoka nchi ya utumwa ya Misri katika kipindi hiki hiki cha majira ya baridi. Kipindi hiki cha majira ya baridi ni cha kufanywa tena kwa mambo yote katika asili zake, ni ishara ya uumbaji mpya wa Mungu wa maisha mapya. Mwezi huu wa Abibu hatimaye ulijulikana kama mwezi wa Nisani.

Kutoka 12: 3: Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana kondoo kwa watu wa nyumba moja;
4 na ikiwa watu wa nyumbani niwachache kwa mwana kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na atwae mwana kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana kondoo.
5 Mwana kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.
6 Nanyi mtamweka katika siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni

Kuanzia mwanzoni kabisa mwa uumbaji Mungu alitupa ishara ili kutufanya sisi tuitambue zawadi yake ya upatanisho ambayo ni huyu Mwana wake wa pekee Yesu Kristo. Katika uumbaji wake aliiumba mianga mikuu miwili ambyo ni Jua na Mwezi, ambavyo vinawakilisha Kristo na Kanisa. Aliviumba siku ya nne ya juma la uumbaji (2 Petro 3:8 inasema .). Pia kwenye Pasaka yule Mwana Kondoo alitunzwa na kuhifadhiwa kwa muda wa siku nne. Katika siku ya miaka-elfu nne, Kristo na kanisa walizaliwa.

Kutoka 12: 7 8
Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla. Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu
Huu ni mfano wa mana ambayo kwayo Kristo alikufa. Taji la miiba na misumari aliyopigiliwa mikononi mwake, yote iluimchoma mwili wake na alkufa msalabani. Damu ilipakwa kwenye miimo ya milango kwenye hali sawa na ile damu iliyomwagika msalabani.

Uchungu
Uchungu ni dalili ya mateso, kutendewa ukatili na utumwa kama tusomavyo Kutoka 1:14, Warumi 1:20 na Yeremia 9:15. Pasaka iliambatana na kula "mboga za uchungu", Kutoka 12:8, Hesabu 9:11. Hii mboga iliyoliwa hapa haijulikani ilikuwa ni ya aina gini. Huenda ilikuwa ni aina yoyote ya mboga chungu iliyopatikana mahali pale walipokuwa na iliyopatikana kipindi ambacho Pasaka ilikuwa inaadhimishwa. Mboga hii iliwakilisha taswira ya uchungu wa utumwa ambapo watu walitaabishwa kwao; na inachukuliwa pia kuwa ni taswira ya mateso ya Kristo.

Kutoka 12:9 25
Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani. Wala msisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya BWANA. Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu, nitakapoingia nchi ya Misri. Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo, mkamchinje pasaka. Nanyi twaeni tawi la hisopo, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini, na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele. Itakuwa, hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, BWANA atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu
[Tunapaswa kuwa na meza iliyoandaliwa vizuri na sahani, bakuli na kikombe. Katikati ya meza tunakuwa na sahani ya nyama iliyopambwa kwa saladi Maridadi na figili zikiizunguka ile sahani lakini kukiwa tupu bila kuwepo nyama ndani yake. (Kama tungeweka nyama kwenye hii sahani, basi tungehukumiwa kwa kumsulibisha Kristo katika mwili kwa sababu yeye alikuwa ni ile sadaka kamilifu iliyokomesha aina zote za dhabihu). Tunaanza kwanza kwa kula zile mboga zenye uchungu (mchunga, ama aina yoyote ya mboga zenge uchungu za majani lakini zisizo na madhara zikiliwa) zichovywe kwenye maji ya chumvi huku tuliuliza maswali yafuatayo].

Maswali ya Pasaka ni Yapi?

1. Je, ni kwanini usiku huu ni wa tofauti na nyingine zote?

Kutoka 12: 26 - 27
Kisha itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, Nnini maana yake utumishi huu kwenu? Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia

2. Je, ni kwanini tunakula chakula hiki kisicho cha kawaida?

Kutoka 1:13 14
Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; wakafanya maisha yao kuwa machungu kwa kazi nguvu; kazi ya chokaa nay a matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba kwa kazi zao zote walizotumikishwa kwa ukali.

3. Je, ni kwanini tunachovya mboga hizi yenye uchungu kwenye maji machungu?

Kutoka 1:14
Ili kuyakumbuka machungu yaliyotokana na mateso ya utumwa ya Misri na jinsi walivyookolewa kwa kupitia Bahari ya Shamu; wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa nay a matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.
4. Je, yuko wapi Mwana kondoo wa Pasaka? Kwa kuwa sahani iko wazi. Mwana Kondoo wa Dhabihu amekwisha chinjwa tayari pale msalabani kwa hiyo teno la kuleta dhabihu kwenye sahani lingemaanisha ni kumsulibisha Kristo kwa upya.

1 Wakoritho 5:7 8
Basi, jisafisheni, mkate ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo mahkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

Waebrania 10:12 14
Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
(Hatuli nyama kwenye ibada hii kwa sababu baada ya Kristo kusulibiwa ambaye ni "Ddhabihu Kamilifu", basi tutakosea kama tutamchinja mnyama tena. Hivyo basi tendo la sahani kuwa wazi inamaanisha kwamba Kristo ndiye Mwana Kondoo wetu wa Pasaka).

Kutoka 12:26 39
Kisha itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, Nnini maana yake utumishi huu kwenu? Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia. Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawapiga wazaliwa wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu. Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, mkamtumikie BWANA kama mlivyosema. Twaeni kondoo zenu na ngombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia. Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote. Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabagani. Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. Na kundi kubwa la watu waliochangamana nao wakakwea pamoja nao; na kondoo na ngombe, wanyama wengi sana. Nao wakaoka mikate isiyochachwa ya ule unga waliochukua walipotoka Misri, maana, haukutiwa chachu, kwa sababu walitolewa watoke Misri, wasiweze kukawia, nao walikuwa hawajajifanyia tayari chakula.

Tunauvunja na kuula mkate usiotiwa chachu huku tukinywa juisi ya zabibu. (Ni lazima iwe juisi ambayo haikutiwa aina yoyote ya amira au iliyochachishwa kwa kuwa chachu inawakilisha dhambi.) Wana wa Israeli waliamriwa kuondoa aina zote za chachu majumbani mwao kipindi hiki.
Kristo ambaye ndiye mfano wetu pia aliitunza sikukuu hii ya Pasaka.

Luka 22:7 20
Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka. Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie Pasaka tupate kuila. Wakamwambia, Wataka tuandae wapi? Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingine katika nyumba atakayoingia yeye. Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba wageni, nipate kula Pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu? Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo. Wakaenda, wakaona kama walioambiwa, wakaiandaa pasaka. Hata saa ilipofika, aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. Akawaambia, Nimetamani sana kuila Pasaka hii Pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja. Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Kikombe nacho baada ya kula; akasema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu,
Usiku wa Pasaka ulitolewa kwa Waisraeli miaka mingi sana kabla ya Kristo, lakini ilionyesha kikamilifu usahihi wa mwezi na siku ambayo Kristo alipaswa kufa msalabani. Ilionyesha kwamba yeye alipaswa kuwa ndiye Mwana Kondoo wa Mungu asiye na dhambi wala waa lolote. Hii ni moja kati ya sikukuu ambazo tumeamriwa kuzitunza na kuziadhimisha milele.

Siku nyingine muhimu zimeorodheshwa kawenye vitabu vifuatavyo:

Kutoka 20:8 11
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa

Lakini Sabato ni lini?

Sio Jumamosi kama wengine wanavyodhania. Pia sio Jumapili kama wengine wanavyoadhimisha. Lakini katika mwaka huu imetokea tu kwamba inaangukia siku ya Jumapili.Kwa mujibu wa mpango wa Mungu, mwezi wa kwanza unaanzia katika mwezi wa Abibu. Mwezi huu wa Abibu unaandama kwenye kipindi kilicho karibu na siku ambayo jua linapita katikati ya dunia kwenye mstari wa Ikweta, siku inayolingana masaa ya usiku na mchana (mwanzoni mwa majira ya baridi). Kwa mujibu wa utaratibu wa Mungu, huanza tarehe 18 Marchi, saa 12:00 jioni na huishia Marchi 19 jioni. Siku saba baada ya Marchi 25 inakuwa ni siku ya saba ya au Sabato. Hii hubadilika mwaka mmoja hadi mwingine kwa kuwa kalenda yetu haifuati utaratibu wa Mwandamo wa Mwezi.

Mwanzo 1:14
Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;

Warumi 14:5 - 6
Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa ni sawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.

Soma pia > Zifahamu siri 7 zilizofichika kuhusu sikukuu ya Pasaka
 
Napenda kujua hii pasaka husherehekewa kwa ajili ya jambo gani.

I'm curios. ⏰
 
Mnataka nayo muishikie bango au kuiga (ila kuiga hamuwezi kwani mitume wengine hawakufufuka!)? Christmas, Yesu alizaliwa, jamaa wakatafuta usawa, wakaita Maulid ya Mtume, matokeo yake wanapingana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanasema si halali kusherehekea maulid (bida'a), wengine wanasema ni halali (hasa wanaopenda kuiga vitu vya upande mwingine). Sasa naona hapa unataka ujue Pasaka ni nini ili uipendekeze huko, lakini bahati mbaya jamaa yenu hakufufuka!
 
Mnataka nayo muishikie bango au kuiga (ila kuiga hamuwezi kwani mitume wengine hawakufufuka!)? Christmas, Yesu alizaliwa, jamaa wakatafuta usawa, wakaita Maulid ya Mtume, matokeo yake wanapingana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanasema si halali kusherehekea maulid (bida'a), wengine wanasema ni halali (hasa wanaopenda kuiga vitu vya upande mwingine). Sasa naona hapa unataka ujue Pasaka ni nini ili uipendekeze huko, lakini bahati mbaya jamaa yenu hakufufuka!

teh teh teh!unafujo ww!
 
Pasaka ni aina ya chakula kilichokuwa kinaandaliwa maalum kwa kutumia kondo na wana wa Israel kama kumbukumbu ya wao kutoka utumwani Misri! Kulikuwa na taratibu zake za kula! Mojawapo ni kula ukiwa umesimama! Mgeni hakuruhusiwa kula nk. Hivyo pasaka ni CHAKULA!
Katika agano jipya kondoo wa pasaka ni YESU KRISTO! tunakula mwili wake na kuinywa damu yake katika kukumbuka tulivyotoka katika agano la kale ambalo lilituweka chini ya sheria!
 
Duh! Kumbe ni kumbukumbu za kufa kwa Mungu,
Haaaa haaaa kuna watu akili zao ni funza tupu hata ukielimisha Mungu hafi hawaelewi.
 
Duh! Kumbe ni kumbukumbu za kufa kwa Mungu,
Haaaa haaaa kuna watu akili zao ni funza tupu hata ukielimisha Mungu hakuzaliwa, halali,hasinzii,hafi,wala hana mfano na kitu chochote yameng'ang'ana tu hawaelewi.
 
Yesu, mungu pamoja nasi, masiha, anafufuka katika wafu na kupalizwa mbinguni
 
Napenda kujua hii pasaka husherehekewa kwa ajili ya jambo gani.

I'm curios. ⏰

PASAKA NI NINI NA MAANA YAKE
************************************************
Pasaka ni sikuku iliyoamriwa na Mungu tangu siku za kale kwa wayahudi kuifanya katika mwezi wa Abibu au Nisani katika "kalenda ya kiebrania" yaani mwezi wa 3 au 4 katika kalenda ya kirumi, kwa lengo la kumbuka njisi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani Misri; Twasoma: "Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako. Nawe umchinjie pasaka BWANA, Mungu wako katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake." (Kumbukumbu 16:1-2) Soma pia: (Kutoka 12:14) Kama tulivyoona katika pasaka wayahudi waliamriwa kuchinja mnyama mmoja katika kundi, lakini tunapoendela kusoma tunaona jinsia Mungu alivyoamuru mnyama huyo aokwe na kuliwa; Twasoma:


"Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoa nchi ya Misri, siku zote za maisha yako. Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote usiku kucha hata asubuhi. Usimchinje pasaka ndani ya malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako; ila mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako apakalishe jina lake, ndipo mtakapomchinjia pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri." (Kumbukumbu 16:3-6); Soma pia: (Kut 12:3-13) Katika mwezi huo wa abibu ambao Mungu aliufanya kuwa mwezi wa kwanza kwako, Wayahudi walifanya karamu ya Pasaka kuwa kumbukumbu la jinsi Mungu alivyowaokoa kutoka Misri (Kutoka 12:1-51; Walawi. 23:5).


Pasaka maana yake ni "kupita Juu", maana Mungu alipita juu ya nyumba zao asiwaangamize wazaliwa wao wa kwanza; Twasoma: "Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazo kuwapo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri." (Kutoka 12:13); Soma pia:(Kutoka 12:27)


JE WAKRISTO TUNA PASAKA LEO?
Ni kweli wakristo tuna pasaka leo, walakini si katika utaratibu ule Uliotumika katika siku za waisraeli, kama tulivyoshuudia maandiko yaneleza wazi ya kuwa sikukuu hizo zilikomeshwa; Basi hebu tuone utaratibu wa Pasaka ya wakristo leo ni upi;


Zingatia: Kama tulivyoona hapo juu, waisraeli waliokolewa na damu ya mnyama walio ipaka katika miimo na miisho ya milango yao na ndipo malaika wa Bwana alipotambua na kupita juu; Soma tena: (Kutoka 12:13, 27); lakini wakristo tunaambiwa pasaka wetu ni Yesu mwenyewe aliyetuokoa kwa damu yake; Twasoma:

"Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:29); Soma pia: (Yohana 1:36) "Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa milioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo." (1 Petro 1-18-19) "Basi jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mapate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;" (1 Wakoritho 5:7) Basi kama tulivyoona Neno la Mungu linatuthibitishia ya kuwa kwa sasa wakristo tunaokolewa na damu ya Yesu ambaye ndiye Pasaka wetu na si kwa damu ya mnyama aliyekuwa Pasaka wa kale. Basi kiwa hivyo ndivyo, ni dhahiri hata utratibu wa kusherehekea pasaka kwa wakristo ni tofauti, Basi hebu tuone wakristo tunasherehekeaje pasaka yetu leo.


Yesu alipokuwa akila Pasaka ya mwisho pamoja na wanafunzi wake, aligeuza Pasaka. Aliwaambia kwamba, kuanza siku ile, watakapokula mikate wangekumbuka mwili wake uliotolewa kwa ajili yao badala ya kukumbuka kuokolewa kutoka utumwani nchini Misri; Twasoma: "Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega akawapa wanafunzi wake, akisema, Twaeni mle; huu ndio mwili wangu Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi." (Mathayo 26:26-28) "Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi, ya kuwa usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, na ye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kwa kila mywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo." (1 Wakorintho 11:23-26).


JE WANAOSHEREHEKEA PASAKA YA KALE WAMEPOTEA?
Ni kweli karibu ulimwengu mzima unasherehekea pasaka kama walivyokuwa wakisherehekea wayahidi nyakati zile, wakidhani ndivyo ilivyo agizwa, basi na tuzingatie maneno yafuatayo; Twasoma: "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti" (Mithali 14:12) "Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa. Waacheni hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili." (Mathayo 15:13-14) "Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu." (Mathayo 7:21-23) "Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe." (1 Wakorintho 4:6) Basi kama tulivyoona, upotofu uliopo katika sikukuu hii ya pasaka na jinsi Mungu anavyo tuonya kuwa makini na mafundisho ya uongo, ni dhahiri tunawajibu wa kujifunza neno la Mungu kwa bidii ili tupate kujua yaliyo mapenzi yake tukayafanye; Soma: (Yakobo 1:22-25)
 
Mnataka nayo muishikie bango au kuiga (ila kuiga hamuwezi kwani mitume wengine hawakufufuka!)? Christmas, Yesu alizaliwa, jamaa wakatafuta usawa, wakaita Maulid ya Mtume, matokeo yake wanapingana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanasema si halali kusherehekea maulid (bida'a), wengine wanasema ni halali (hasa wanaopenda kuiga vitu vya upande mwingine). Sasa naona hapa unataka ujue Pasaka ni nini ili uipendekeze huko, lakini bahati mbaya jamaa yenu hakufufuka!

Jibu swali ....kuzi wewe.....
 
Mnataka nayo muishikie bango au kuiga (ila kuiga hamuwezi kwani mitume wengine hawakufufuka!)? Christmas, Yesu alizaliwa, jamaa wakatafuta usawa, wakaita Maulid ya Mtume, matokeo yake wanapingana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanasema si halali kusherehekea maulid (bida'a), wengine wanasema ni halali (hasa wanaopenda kuiga vitu vya upande mwingine). Sasa naona hapa unataka ujue Pasaka ni nini ili uipendekeze huko, lakini bahati mbaya jamaa yenu hakufufuka!

Doooh!
 
Back
Top Bottom