Pasaka imenipotezea rafiki yangu kipenzi

Pasaka imenipotezea rafiki yangu kipenzi

Nyela maveembo[emoji21][emoji21][emoji21][emoji29][emoji29][emoji29]
 
Ni wiki moja tu imepita, Tulichati kwa whatsap.Tulikuwa tukicheka madakika yakapita.Sikujua Kama Ulikuwa waniaga, Umeondoka mkuu.Pumzika kwa Aman Kaka Fred,Mungu akupokee. Mpaka Sasa sielewi na pia siamini Kama kweli umetutoka, nawaza na kujifariji labda kesho utaamka.Taarifa za kifo chako, zinatatiza ni ngumu kuelewa.Pumzika kwa Aman Kaka Fred, Mungu akupokee. Taarifa zinaeleza ulikuwa watoka kijijini Kilolo, mara Izraeli akakupata,ghafla bila kujua Pumzika kwa Aman Kaka,hiyo ni njia yetu sote. Utakumbukwa Sana mitamdaoni,fb mpaka jf.Fb ulijulikana na ukurasa wako wa vichekesho,Tabasamu na Fuledi,wengi walikuelewa,na walipenda vichekesho vyako.Pumzika kwa Aman Kaka,Mungu akupokee.Ajali ya gari imekatisha uhai wako, Tena siku ya Pasaka,kweli kifo ni fumbo,nakosa hata wa kunisimulia ilikuwaje,kila mtu anasema juu juu tu,Pumzika kwa Aman broo Mungu akupokee.😭
Pole sana ndugu, wema hawadumu, wanaonyanyasa wenzao kwa madaraka ndio wanadunda na mavichwa yao kama kambale mumi.
 
Kidrive kuna raha yake but kuna hitaji
1. Umakini
2. Sharp decision
3.Kuvumilia makosa ya wengine na kuresolve ili kuepusha madhara.
Hii hoja namba tatu wengi sana tunaisahau, ndiyo tunajikuta tukisababisha ajali ambazo zingeweza kuepukika
 
Wanaoongoza kwa kudrive hovyo ni madereva wa mabasi.
Ambao wanajitahd kuwa fare ni madereva wa malori.
 
Hii hoja namba tatu wengi sana tunaisahau, ndiyo tunajikuta tukisababisha ajali ambazo zingeweza kuepukika
Head to head collision nyingi huwa zinasababishwa na point namba tatu. Ata kama unahaki unapomuona mwenzako amekosea mvumilie punguza mwendo, mpe nafasi ya kujirekebisha, madereva wa mabasi huwa hawana huo muda ukijichanganya anakuletea..ata yy akijichanganya hana muda wa kujiuliza mara mbili.
 
Kichwa cha habari kina utata kidogo “Pasaka imenipotezea Rafiki yangu......”inaleta maana tofauti,anyway RIP Fred !km itakupendeza mtoa post naomba utukumbishe post zake alizozitoa ndg yetu huyu (maana majina yetu JF ni ya bandia )ila na sisi tushiriki msiba huu kwa Feeling.
Inaonesha aligonga mvinyo akawa ana drive... Maana pasaka haiwezi ondoka na mtu hivi hivi....
 
Road kuna mengi..otherwise labda kama hujawah toka nje ya mkoa ukidrive
 
Unafanya masikhara na kifo. Izraeli akampata maana yake nini?unaandika kitu hukijui.kwa masikhara wakat unajidai ni jamaa yako.
 
Pumzika kwa Amani FRED. Pole sana mkuu na kwa familia yake yote
 
Death is the destination we all share, No one has ever escaped it and that is as it should be

Because Death is very likely the single best invention of life, our life

Pole Mkuu
 
ooh jamani pole sana. Bwana ametoa na Bwana ametwaa
 
Back
Top Bottom