Pasaka imenipotezea rafiki yangu kipenzi

Pasaka imenipotezea rafiki yangu kipenzi

MR.NOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
339
Reaction score
512
Ni wiki moja tu imepita, Tulichati kwa whatsap.Tulikuwa tukicheka madakika yakapita.Sikujua Kama Ulikuwa waniaga, Umeondoka mkuu.Pumzika kwa Aman Kaka Fred,Mungu akupokee. Mpaka Sasa sielewi na pia siamini Kama kweli umetutoka, nawaza na kujifariji labda kesho utaamka.Taarifa za kifo chako, zinatatiza ni ngumu kuelewa.Pumzika kwa Aman Kaka Fred, Mungu akupokee. Taarifa zinaeleza ulikuwa watoka kijijini Kilolo, mara Izraeli akakupata,ghafla bila kujua Pumzika kwa Aman Kaka,hiyo ni njia yetu sote. Utakumbukwa Sana mitamdaoni,fb mpaka jf.Fb ulijulikana na ukurasa wako wa vichekesho,Tabasamu na Fuledi,wengi walikuelewa,na walipenda vichekesho vyako.Pumzika kwa Aman Kaka,Mungu akupokee.Ajali ya gari imekatisha uhai wako, Tena siku ya Pasaka,kweli kifo ni fumbo,nakosa hata wa kunisimulia ilikuwaje,kila mtu anasema juu juu tu,Pumzika kwa Aman broo Mungu akupokee.😭
 
Nilipo ona sehem umeandika kwamba alikua member wa humu jf, hapo ndipo hasa nimejikuta natamani kujua zaidi kuhusu marehemu.
R.i.P jf member....[emoji22][emoji22]
 
Mnaweza kupata picha alikua ni mtu wa aina gani. Rip bro
FB_IMG_1555966762519.jpeg
FB_IMG_1555966728574.jpeg
FB_IMG_1555966631752.jpeg
 
Njia yetu sote

Ni ahadi Mungu aliahidi wote tutapita hapo

Mbele yake nyuma yetu,Mungu amuweke panapo stahikhi.
 
R.I.p kaka [emoji22],tulikiwa nae Njombe jamaa wakati huooo,mcheshi sana,haishi vituko,dah!pumzka kwa amani bro,sote njia yetu ni moja!
 
Kichwa cha habari kina utata kidogo “Pasaka imenipotezea Rafiki yangu......”inaleta maana tofauti,anyway RIP Fred !km itakupendeza mtoa post naomba utukumbishe post zake alizozitoa ndg yetu huyu (maana majina yetu JF ni ya bandia )ila na sisi tushiriki msiba huu kwa Feeling.
 
Back
Top Bottom