Parking System Arusha mnanyanyasa wananchi

Parking System Arusha mnanyanyasa wananchi

hjayhals

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
768
Reaction score
559
Habari wana JF
Naleta mbele yenu suala hili naamini linaweza kufika panapohusika na likafanyiwa kazi mara moja, kumekuwa na unyanyasaji mkubwa sana wa wananchi wamiliki/madereva wa magari Arusha kuhusiana na suala zima wanaloita "wrong parking". Inasikitisha kwamba maeneo mengi mistari ya njano imefutika kwa hiyo inakuwa vigumu kwa wananchi kuona na wanapopaki wanakuja jamaa na cheni wanafunga gari yako na faini inakuhusu, tatizo watu wanaripoti hadi kwa mkuu wao (Ngare) kuwa mistari haionekani bila msaada wowote, huku vijana wake wakijitapa kwamba wakichora mistari serikali itapata vipi mapato?

Wameweka kambi zaidi eneo la samunge (sikh temple union building), pale kuna parving zilizowekwa na wale jamaa wenye jengo lao, wakatofautisha parving nyekundu kama alama zao za parking, sasa hivi kutokana na uchafu zile parving hazionekani kabisa tofauti zake zote zinafanana (nimeambatanisha picha) na ukienda na gari pale kamwe huwezi kuona kama kuna paving za tofauti, wanakuja wanakuambia umekanyaga mstari (parving nyekundu) na wanakushinikiza ulipe faini.

Kama hili suala litafanyiwa kazi mistari ikachorwa mjini watu wakaiona itakuwa vyema sana kuliko namna ambavyo watu wanavyodhulumiwa.

Nawasilisha.
samunge sikh temple.jpg
 
Aisee mimi na hasira nao nimepiga picha hadi vitambulisho vyao,iko siku wataingia 18 zangu watajuta. Wamechimba mitaro mistari haionekani halafu wanasema wrong parking. Mistari imefutika haionekani.
 
me kabla ya kushuka kwenye gari wakati wa kupaki namwita yule dada parking aangalie ka niko sawa...nikirudii nikikuta nyororo zao ama zangu ama zao wahuni wale...hiyo ni.baada ya kutifuana nao sana huko nyuma...
 
Back
Top Bottom