GE2025 Paresso: Samia ameondoa hofu kwa wafanyabiashara

GE2025 Paresso: Samia ameondoa hofu kwa wafanyabiashara

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Aliyekuwa mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso, amewataka wananchi wa Kilimanjaro kumpa kura za kishindo mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ifikapo Oktoba 29, akisema ameweka mazingira bora kwa wafanyabiashara nchini.

Akizungumza jana Jumatatu, Septemba 8, 2025, katika uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika Kata ya Pasua, Manispaa ya Moshi, Paresso amesema kabla ya Samia kuingia madarakani wafanyabiashara walikuwa na hofu kubwa, kiasi cha baadhi yao kuhamisha mitaji nje ya nchi.

“ Samia alipoingia madarakani aliboresha mahusiano na wafanyabiashara, hasa kwenye mifumo ya kodi. Leo hii mazingira yamebadilika na wafanyabiashara wanafanya shughuli zao bila hofu,” amesema Paresso.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho pamoja na wananchi. Mgombea ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Ibrahim Shayo maarufu Ibra Line, aliyeahidi kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa stendi ya mabasi, miundombinu ya barabara na ukusanyaji wa taka ngumu

Soma pia


Chanzo: Mwananchi_official
 
Walikuwa na Hofu ya Nini...??. Hakuna kitu kinanipa Amani Moyoni kama Mm nikiwa Dukani Halafu Kila Kitu nimelipia Sina Deni na Mtu wala utawala Wowote..

Maana Kila Vielelezo vipo na Wakija Wala Huna Wasiwasi.. Ukiwa na Hofu Ujue Kuna MADUDU umefanya.
 
Back
Top Bottom