GE2025 Paresso: CCM ndiyo Chama kinachoweza kuongoza nchi hii

GE2025 Paresso: CCM ndiyo Chama kinachoweza kuongoza nchi hii

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Cecilia Paresso amesema kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo uliofanywa na CCM, chama hicho kinakuwa chama pekee kinachofaa kuendelea kuongoza nchi

Paresso ambaye alikuwa mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha na kwa muda mrefu kada wa CHADEMA kabla ya kuhamia CCM, amesema Dkt. Samia anastahili kupewa kura kwani kaonesha uwezo wake kiuongozi kwa kipindi cha miaka minne aliyokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

"hiki chama ambacho kimetuongoza kwa kipindi chote ndiyo chama pekee ambacho kinaweza kutuongoza tena sisi tuliopo leo, watoto wetu na vizazi vijavyo"

Paresso amesema katika kuonyesha uwezo wa kiuongozi, CCM imefanikiwa kuilinda amani ya nchi yetu jambo ambalo ametahadharisha kuwa vyama vingine havitaweza kufanya endapo vikipewa mamlaka

Haya ameyasema Septemba 23, 2025 akiwa katika mwendelezo wa vikao vya kutafuta ushindi wa Dkt Samia, Mgombea ubunge wa jimbo la Muhambwe Dkt Samizi pamoja na madiwani wa jimbo hilo

Akiwa jimbo la Muhambwe Paresso ameshiriki vikao pamoja na kamati za siasa za matawi, kamati za utekelezaji za jumuiya na mabalozi katika matawi ya Nyabitaka, Nyarugusu , Kasana na Kumshwabure


 
Kweli njaa haina adabu. Kamanda ameamua na yeye kujitoa ufahamu ili maisha yaende mbele.
 
Back
Top Bottom