Parapanda lylics

Parapanda lylics

kapesly

Senior Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
163
Reaction score
108
🎵🎤🎼🎶🎵🎤🎼🎶🎼🎶🎼
👤 for Roma na
🙊 for Stamina
👤Karibu mzee kingunge kwenye makazi ya milele Mimi huku ninamji wangu tayari unaitwa nyerere ,nimeshtuka kukuona huku nini chanzo cha msiba..h,
🙊 nimipango ya mungu na nimekumisi swaibah
👤vipi nchi yangu Mtawala ni chama gani❕❗❓
🙊Bado ni C C M,Ingawa kuna Upinzani...
👤unamaana gani!? Kwaiyoo Raisi ni NANi!?
🙊Raisi ni JOHN ndo anaongoza usukani..
👤 John Malechelaaah
🙊Nooh Magufuli,ulimuacha ni mbunge wa Chato,Sijui unamkumbuka vizuri..
👤 Hahaa..ngoja kwanza unajua haya mambo haya minilizani alipotoka Mkapa angefata Jakaya!.
🙊 Jakaya alitawala akaja akaritaya(retire) nimeacha mengi yaani mambo ni moto mambo ni fayah
👤 Aaha mbona nasikia mambo haiko sawa na kina nani hawa ambao wanajiita UKAWA
🙊 ni wapinzani waliungana lakini hawakumshinda MAGU wengine chama walihama na bado wakapata TABU <Sanaaa,>
Kakomesha ufisadi.<Kodi> Kaongeza ukusanyaji Hakika wamepata mkombozi atayewafikisha nchi ya ahadi
👤Nilisikia siku hizi bunge halionyeshwi kwenye inamaana hoja za viongozi wanachi haziwafikii na mitandao ya kijamii je vipi haiwasaidii!?
🙊Kuna Dada anaitwa Mange pliizi..(laxima...)
🎶🎶🎼🎼🎶🎼🎶🎼🎶🎼🎶
👤je! Vipi kabuli langu tayari walilijengea na vipi kuhusu mke wangu maria wanamtembeleah!?
🙊Kuhusu kumtembelea hilo toa shaka wanamjali na kumlea tena kwa heshima na mamlakah..
👤Na nimemwona shemeji yangu h amakweli mnapendana mmefatana penzi la kweli kufa na kuzikana vipi mwanangu makongolo Mali zangu anazichungah!.
🙊 an'ghaa Bora wakwako mwenzie bize na TUNDAH.. Mm.mh..hivi Julius ulikua simba au yanga!!
👤kiukweli niliipenda Yanga ila simba ni kisangah.
🙊enhehee..mwalimu unajua hadi kisanga!?
👤hata hilo nasikia mengi kibamia hadi kudangah..nimemwona komba huku nyimbo za chama anatunga nani!?
🙊Mi nasikia wanaisoma namba Ila sijui ameitunga nani!?
👤Sijakuelewa kwani anaesimamia sanaa ni nani!?
🙊mmh..lipo baraza ila wasanii wanaishi uani..

🎼🎶🎵🎶🎤🎼🎵🎶🎼🎵
👤Kuhusu mungano bado upo ama umechujah!?
🙊 mpemba anauza kariakoo na mzalamo anaduka ungujah!
👤Ujinga Maradhi na Umasikini bado maadui nipe taarifah.
🙊ujinga angarau ao wengine janga la taifa..
👤na kuhusu barabara..!
🙊zipo
👤madaraja
🙊yapo
👤 Kama ndivyo inamaana uchumi unapanda enhee..
🙊mmmh..wanadai cherehani mbili ukiwanazo unakiwanda vyuma viko still na kuna hospitali hazina vitandah
👤Bado nina maswali mengi vipi mwenendo wa katiba.!
🙊mchakato ulisitishwa inasemekana walimpigah.!
👤walimpiga nani na kina nani na nini alifanyah..!?
🙊Mwalimu sijui ila ni watu WASIOJULIKANA..
👤waliompiga risasi lissu
🙊ni watu WASIOJULIKANA..
👤kina nani walimteka Roma?
🙊ni watu WASIOJULIKANA..
👤na wanaoteka waandishi wa habari?
🙊eenhe sijui ni watu WASIOJULIKANA..

🎼🎶🎤🎶🎼🎵🎶🎼🎶🎵🎼
 
Duh mie mshamba kusoma heading tu nikaanza kuimba parapanda italia parapanda ooh malaika watakua wamekwisha kumjia kweeenda kumlaki
Hahahaha Numbisa nmecheka khaaa
Ila upo kama mm nlivyosikia Parapanda nami nikaanza kuimba kama ww
 
Bonge LA ngoma aisee.....haitafungiwa ile I bet
 
Niliposoma heading nikajua muhimbili mambo yakuwa sio mambo.
Dah!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom