Miss MariaAntonia tatizo lipo kwenye wewe kulazimisha makosa yawepo iwapo utayakosa. Just be careful. . .'DON'T LOOK FOR TROUBLE WHERE THERE ISN'T ANY, BECAUSE IF YOU DON'T FIND IT, YOU'LL MAKE IT.Just believe in someone.'
ni ngumu kumeza 'DONT LOOK'
mimi naona LOOK kimyakimya bila mwenzio kujua unalook, ukijiachia sana utajashtukia kuna mafuriko pindi UTAKAPOSHINDWA KUPUMUA maji yamekuzingira kitanda wewe ukiwa usingizini
Paranoia ni ugonjwa wa akili kama yalivyo magonjwa mengine ya akili, mtu mwenye tatizo hili anahitaji msaada wa haraka wa tiba, maana itakuwa ni vigumu kwake si kujenga tu uhusiano imara na mwenzi wake bali pia hata jamii iliyomzunguka.
Naamini sio vibaya kumwambia mtu mwenye tabia hizo kuwa yu mgonjwa, na anahitaji tiba ya haraka, kwani huo utakuw ani msaada mkubwa sana kwake. wengi wetu hapa kuna watu waliotuzunguka, wanaweza kuwa ni wenzi wetu, marafiki zetu, wafanyakazi wenzetu au jamaa zetu wanaokabiliwa na tatizo hili, lakini tunaona haya kuwaambia ukweli kuwa ni wagonjwa. Hata kama wakitukasirikia, lakini tutakuwa tumewasaidia sana katika maisha yao ya kimahusiano.
Ahsante sana Lizzy kwa kulizungumzia hili. kwani wengi tumekuwa tulileta mada humu za watu wenye tatizo hili lakini tumekuwa tukizunguuuka wakati ukweli ndio huu.
Hayo ni maradhi ya kimalezi,yanatibika kwa ushauri,tatizo mtu mwenye maradhi haya hajui kama anayo mpaka akutane na mtaalamu wa saikolojia!So ushauri kwa hawa ni kuwakutanisha na madaktari hawa wa saikolojia!
Samahani sana ndugu,
Kwani huo ugonjwa una level moja tu? Hakuna wale ambao hali yao ni mild na wale ambao ni serious?
Babu DC,nakusalimu!Nijuavyo mimi haya ni maradhi yanayotokana na malezi kwa kias kikubwa,so inafikia ugonjwa unaonekana ni mtu anaingia kwenye ndoa so ni ukubwani,muda unakua umepita,hivyo lazima anakua tayari ni siriaz,kuepusha hali ya kuwa siriaz ni kumuwahi mtu akiwa kwenye familia kwa kubadili malezi!
Nakubaliana na wewe Babu DC
Ndo maana nikasema paranoia nayo inategemea ni kiasi gani
Kama ni kupima in % unaweza kuta mtu ana 10% lakini haijaanza kuleta madhara makubwa
Na mwingine unakuta ni 90% ambayo haivumiliki
But to some extent, watu wengi ni paranoia kwa level fulani
Ndo maana ukimkuta mpenzi wako anatoka guest
Lazima uulize ni nini kinendelea hapo hasa kama hakukuambia atapita huko
Lakini je kukutwa unatokea mlango wa guest ni kwamba unacheat?