Paradox ya CCM - "Britanicca"

Paradox ya CCM - "Britanicca"

sure kuwa mwana ccm haimaanishi ni lazima ujitoe akili ,tuna wana ccm kama askofu gwajima ,mzee warioba..hata mimi ni ccm
 

Attachments

  • images - 2026-08-13T004504.144.jpeg
    images - 2026-08-13T004504.144.jpeg
    49.7 KB · Views: 1
Unayo haki na uhuru wa maoni, hakuna ibara wala kifungu cha sheria kinachosema kuwa mfuasi wa chama fulani kunakuondolea haki yako ya kikatiba na hata hile inayotambuliwa kisheria.

Chukua hatua ya kuwasilisha maoni yako upendavyo mladi tu hauvunji sheria.

chanzo: www.katibampya.com
 
Marehemu Mustafa Sabodo alikuwa mfanyabiashara mkubwa na kada wa muda mrefu wa CCM aliyewahi kutoa michango ya fedha na kuunga mkono CHADEMA ili kuimarisha demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania.Sababu na Msimamo wa SabodoKukuza Demokrasia: Aliamini kuwa upinzani wenye nguvu unasaidia kuisimamia serikali na kuleta maendeleo.Ushirikiano Huru: Licha ya kuwa kada wa CCM, alitoa misaada ya mamilioni ya fedha kwa CHADEMA katika vipindi tofauti vya uchaguzi na mikutano yao mikuu.Mtazamo wa CCM: Chama cha CCM kilieleza kuwa kila mtanzania ana uhuru wa kutumia rasilimali zake na kutoa msaada kwa chama chochote apendacho.

huyu mwana ccm wakati wa uhai wake alikuwa anatoa michango yake ya fedha kusapoti chadema ,je kwa leo mwanachama wa ccm tena mfanyabiashara mkubwa anaweza kwenda kupeleka mchango wa pesa zake chadema na kuwapongeza chadema huku yeye ni mwana ccm?? inawezekana leo??
Kuna tofauti kati ya mzalendo na mwanasiasa (nationalist vs politician).
Kwa sasa hatuna wazalendo, wapo wanasiasa wanaowaza faida yao binafsi au zaidi sana ndugu na marafiki.
Wazalendo watafikiria taifa kwa ujumla.
Changamoto tuliyonayo kwa nyakati hizi, katika utumishi wa uma, na jamii kwa ujuma, wazalendo ni wachache sana. Wapo vibaraka, chawa, mafisadi, majuha na majinga. Hili ni janga la kitaifa.
Tunahitaji majasiri wazalendo kwenye madaraka waanze kutoa upya elimu ya uzalendo kwa vitendo.
 
1/ Kuna kitu kinashangaza wengi kwenye forum yetu.
Mwanachama wa CCM anayeitwa BRITANICCA amekuwa gumzo.

2/ BRITANICCA ni mwanachama wa chama tawala CCM. Lakini kazi yake kubwa ni kukosoa mienendo ya chama chake mwenyewe kila siku.

3/ Cha kushangaza zaidi...
Anamkubali na kumsifu zaidi Mwenyekiti wa CHADEMA kuliko Mwenyekiti wake mwenyewe wa CCM.

4/ Sio tu hivyo.
Amegeuka kuwa mfuasi kindakindaki wa LISSU. Anamfuata na kumsapoti kuliko hata anavyomfuata Mwenyekiti wake Samia.

5/ Hii inatuambia nini?
Kwamba hata ndani ya chama tawala kuna sauti zinazopinga, kuna watu wamechoka, kuna watu wanaona kinyume kinaendelea.

6/ Swali ni: Hii ni ujasiri wa kutoa maoni au ni ishara ya mgawanyiko ndani?
Maoni yenu? 👇


Britanicca
Ni maoni ndani ya Ccm.
Endelea mutoa maoni mkuu.

Sisi waafudhina tunataman sana chama chetu kibadili sana aina ya siasa zake.

Watu wanataka maendeleo , Matokeo, na Furaha .

Nalog-off
 
Ila wakati wa Mkapa na alivyoua watu kule Zenji ulikuwa poa
Wakati Kikwete ukaibuka na gozigozi
Alivyokuja Magu ukatulia
Na sasa umeibuka tena
Hii inaitwa Pattern Recognition
 
Udini hauna nafasi,akitawala mtawala wa dini yako unafaidika nini?haya sasa unafaidika nini,ama ushabiki kama simba na yanga,..nvhi ikiwekewa vikwazo ama petroli ikipanda bei, wananchi wote bila kujali dini zao wata athirika na mfumuko wa bei ,n hali ya manadiliko ya kiuchumi.

watu wakiumizwa yale ya O29 kwani ni watu wa dini moja tu ndio walioathirika??

Hata mkichagua viongozi wengi wa dini moja mkawarundika serikalini wamesaidia nini ?wameleta faida gani?

NA PROPAGANDA ZA KUWAGAWA WATU KWA UDINI zilianzishwa lakini ZIKAFELI na hazitafanikiwa.
 
Mi ni CCm kitambo dogo, Tatizo mnadhan CCM lazima kila mtu awe muimba mapambio

Britanicca
Na ndiyo shida kubwa iliyopo hivi sasa, mimi naamini wapo wana CCM wenye akili na wanajua mambo yanayoendelea hivi sasa mengi ni hovyo lakini hawawezi kutoka angalau anonymously kusema ukweli.

Inataka uwe mtu wa misimamo haswa kukosoa chama chako pindi unapoona mambo hayaendi inavyopaswa. Nakubaliana na mdau hapo juu, you're principled.
 
Na ndiyo shida kubwa iliyopo hivi sasa, mimi naamini wapo wana CCM wenye akili na wanajua mambo yanayoendelea hivi sasa mengi ni hovyo lakini hawawezi kutoka angalau anonymously kusema ukweli.

Inataka uwe mtu wa misimamo haswa kukosoa chama chako pindi unapoona mambo hayaendi inavyopaswa. Nakubaliana na mdau hapo juu, you're principled.
Hata Lissu akikosea akitokea Lema amemkosoa ni vita.


Mwanasiasa apendi ukweli.


Kila mwanasiasa upenda kushabikiwa hata yale ya uongo
 
Back
Top Bottom