Papo kwa papo

Papo kwa papo

Azizi J Hamad

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2020
Posts
442
Reaction score
230
Ilani ya CCM, Sura ya 10, Ibara ya 251,(e), Uk.299. Hatua nyingine muhimu kwa Chama katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ni kuhakikisha kuwa, Chama kinatenga siku maalum kila wiki ili kusikiliza kero za wananchi na kuzifikisha serikalini kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

Chama Cha Mapinduzi kimeamua kutumia uwanja wa Papo Kwa Papo, kuwa ni njia mojawapo ya sehemu ya kukutanisha viongozi na wananchi wote, ili kufikisha changamoto na kero zao, kisha ziweze kupata ufumbuzi.

Mimi nimeamua kuwa mubashara kila siku ya Jumamosi kufuatilia kipindi hiki cha Papo kwa Papo, na sitaki kufanya ajizi kukushauri ewe mtanzania mwenzangu kuungana na mimi na watanzania wote kufuatilia kipindi hiki kila siku ya Jumamosi saa3:00-5:00 usiku kupitia channel 10, Uhuru fm redio, mitandao ya kijamii ya Chama Cha Mapinduzi, pamoja na ile ya Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Ndg.Humphrey Polepole. {Youtube, Facebook na Twitter}
#PapoKwaPapo
 

Attachments

  • PapoKwaPapo.m4v
    11.1 MB
Kwani wewe ni mbunge wa Jimbo gani?
 
Naona unapiga promo ukitarajia hicho kipindi kipate mvuto. Hicho wanaangalia wanaccm na watu waliopoteza ramani.
 
Back
Top Bottom