Papa kujadili ndoa na talaka kanisani

Papa kujadili ndoa na talaka kanisani

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,109
Reaction score
53,630
10541911_860985067253493_4725128045075662751_n.jpg

141005160700_vatican_synod_512x288_bbc_nocredit.jpg

Viongozi wa kanisa watajadili maswala kama ndoa, talaka na uzazi wa mpango wa kisasa

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis amefungua rasmi mkutano wa viongozi wakuu wa kanisa hilo kujadili maswala kama vile uzazi wa mpango, talaka na ndoa za jinsia moja.

Wanaojadili maswala haya ni viongozi wa kanisa hilo na wanatarajiwa kufanya hivyo kwa uwazi bila uoga wowote.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya Vatican, David Willey anasema kuwa Papa alifungua mkutano huo na kuwataka viongozi hao kuongea bila uoga wowote kwa kipindi cha wiki moja.

Papa alianzisha mjadala wa baadhi ya mambo ambayo ni mwiko kwa wengi wa viongozi wa kanisa na kuwataka kuyajadili bila uoga.

Aliwaambia zaidi ya viongozi 200 wa kanisa hilo pamoja na wataalamu kuongea bila hofu ya kumuudhi,kuongea ukweli na kwa uwazi na kusikiliza kwa umakini.

Mkutano huu ni wa kipekee kwani mikutano ya Vatican kwa kawaida huwa na kimya kingi.

Lugha ambayo hutumika kwa kwaida huwa imejaa maneno yanayoambatana tu na mafunzo ya kanisa.

Papa Francis alifungua rasmi mkutano huo na kuwataka viongozi wengine kuongea kwa uwazi.

Papa amekuwa akitaka gumzo katika kanisa kuhusiana na maswala ya ngono na pengo lililopo katika mafunzo ya dini na masuala kuhusu familia na ambavyo familia za kikatoliki zinaishi maisha yao.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala kuhusu ikiwa ni sawa kuruhusu wakatoliki wanaotalakiana na kisha kuona tena kukubaliwa kupokea sacramenti.

Papa Francis anataka kanisa kuwaonea huruma watu waliotalakiwa bila ya kulegeza msimamo kuhusu maswala ya ndoa.

Chanzo
: BBC Swahili

Papa kujadili ndoa na talaka kanisani - BBC Swahili
 
10541911_860985067253493_4725128045075662751_n.jpg

10628287_860985490586784_8153498639473749430_n.jpg

141005160700_vatican_synod_512x288_bbc_nocredit.jpg

Viongozi wa kanisa watajadili maswala kama ndoa, talaka na uzazi wa mpango wa kisasa

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis amefungua rasmi mkutano wa viongozi wakuu wa kanisa hilo kujadili maswala kama vile uzazi wa mpango, talaka na ndoa za jinsia moja.

Wanaojadili maswala haya ni viongozi wa kanisa hilo na wanatarajiwa kufanya hivyo kwa uwazi bila uoga wowote.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya Vatican, David Willey anasema kuwa Papa alifungua mkutano huo na kuwataka viongozi hao kuongea bila uoga wowote kwa kipindi cha wiki moja.
Papa alianzisha mjadala wa baadhi ya mambo ambayo ni mwiko kwa wengi wa viongozi wa kanisa na kuwataka kuyajadili bila uoga.
Aliwaambia zaidi ya viongozi 200 wa kanisa hilo pamoja na wataalamu kuongea bila hofu ya kumuudhi , kuongea ukweli na kwa uwazi na kusikiliza kwa umakini. Mkutano huu ni wa kipekee kwani mikutano ya Vatican kwa kawaida huwa na kimya kingi.
Lugha ambayo hutumika kwa kwaida huwa imejaa maneno yanayoambatana tu na mafunzo ya kanisa.
Papa Francis alifungua rasmi mkutano huo na kuwataka viongozi wengine kuongea kwa uwazi. Papa amekuwa akitaka gumzo katika kanisa kuhusiana na maswala ya ngono na pengo lililopo katika mafunzo ya dini na masuala kuhusu familia na ambavyo familia za kikatoliki zinaishi maisha yao.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala kuhusu ikiwa ni sawa kuruhusu wakatoliki wanaotalakiana na kisha kuona tena kukubaliwa kupokea sacramenti.
Papa Francis anataka kanisa kuwaonea huruma watu waliotalakiwa bila ya kulegeza msimamo kuhusu maswala ya ndoa.chanzo.
Papa kujadili ndoa na talaka kanisani - BBC Swahili
 
Dini zinazoenda na wakati!
Possibly Mungu nae anaenda na wakati eee...
 
Wakristo wanacheza na NATURE jambo ambalo haliwezekani.

Mwenyezi Mungu kaumba wanawake na wanaume ili waowane, ili watende tendo la ndoa (sex) kisha Wakristo wanapinga hicho kitu yaani wanashindana na Mungu.

Ingawa kufanya kwa siri lakini inaonesha bora kutoka hadharani.
 
Hii habari jana Radio Tumaini waliiyeyusha wakaiminya ghafla walipokuwa wanapitia magazeti asubuhi saa 2.
 
Back
Top Bottom