Papa Francis: Nitakufa baada ya miaka miwili au mitatu

Papa Francis: Nitakufa baada ya miaka miwili au mitatu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
papa+px.png

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Fransis.PICHA|MAKTABA


KWA UFUPI
Utamaduni wa kuachia madaraka ndani ya kanisa hilo linalotajwa kuwa na waumini wengi duniani uliasisiwa upya mwaka jana na mtangulizi wake, Papa Benedict XVI aliyeng'atuka kutokana na
matatizo ya kiafya.


Vatican, Italia
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kwa mara ya kwanza ametabiri hatima ya maisha yake duniani akisema kuwa anaamini Mungu anaweza kumpa muda wa miaka miwili au mitatu ya kuishi.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akitoka ziarani Korea Kusini kurejea Vatican, Papa Francis alisema suala la kuendelea kuishi ni neema ya Mungu.

"Suala hili naliona kama neema tu ya Mungu kwa watu wake. Najaribu kutafakari kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua kwa sababu hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu nitakuwa nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba," alisema.

Papa Francis (77), pia alizungumzia uwezekano wa kustaafu endapo atahisi kwamba afya yake hairuhusu kuendelea na kazi.

Utamaduni wa kuachia madaraka ndani ya kanisa hilo linalotajwa kuwa na waumini wengi duniani uliasisiwa upya mwaka jana na mtangulizi wake, Papa Benedict XVI aliyeng'atuka kutokana na matatizo ya kiafya.

Pamoja na kwamba Papa Francis hajawahi kuzungumza hadharani kuhusu ni lini pengine anaweza kufariki dunia, lakini baadhi ya vyanzo vya habari kutoka Vatican vinasema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwaambia watu wake wa karibu kuhusu siku zake chache zilizosalia duniani.

Wachambuzi wa masuala ya kiimani kwa nyakati tofauti walisema huenda kiongozi huyo ana tatizo la kiafya ambalo halijawekwa wazi.

Wakati hayo yakiendelea taarifa za ndani zinabainisha kwamba kiongozi huyo aliwahi kutolewa pafu moja baada ya kuathirika wakati akiwa kijana nchini Argentina.

CHANZO: Mwananchi


 
Akiona Mwaka wa Tatu umefika hajafa si anajiua tu kutimiza usemi wake
 
Sina hakika kama maana yake aliyokusudia ni hiyo, philosophers wana namna yao ya kuongea kwa lugha iliyofichika!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom