Papa Francis kuchangia wahanga Msumbiji

TEAM 666

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
4,330
8,421
Hello JF

Papa Francis ametoa msaada wa kiasi cha dola 121,000 (£90,000) kusaidia wahanga wa mashambulio ya kigaidi yaliyotokea Kaskazini mwa Msumbiji katika jimbo la Cabo Delgado.

cq5dam.thumbnail.cropped.1500.844-600x338.jpg


Msaada huo umetolewa baada ya askofu wa Pemba, Luis Fernando Lisboa, kuomba msaada kwa ajili ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia za wanamgambo wa kiislamu.

Kumekuwa na mashambulio kadhaa katika maeneo ya utajiri wa gesi tangu mwaka 2017. Watu wapatao 430,000 wameachwa bila makazi kutokana na vurugu hizo.

Askofu Lisboa akiongoza kampeni inayofahamika kama “Together for Cabo Delgado” yaani Pamoja kwa ajili ya Cabo Delgado.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa papa ametuma mchango wake ambao utatumika kujenga hospitali na makazi ya watu ambao wanaishi katika kambi haswa katika eneo la Montepuez na Chiure.

Maombi hayo ya askofu yalitaka suluhisho la kiusalama na msaada kwa watu waliopoteza makazi yao.
 
Back
Top Bottom