Papa agoma kuishi Ikulu: KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ameendelea kuwa kiongozi wa matukio yanayopingana na watangulizi wake, ambapo sasa amekataa kuhamia katika makazi ya kifahari ya Papa
Makasiri ya Vatican yale huingii hivi hivi tu mjomba, lazima lazima yapigwe fathiha ya nguvu (waweza ita upako au kisomo ukipenda🙂 . Vinginevyo hivyo vimbwanga utakavyokumbana navyo humo ndani nasikia ni balaa. Kumbuka yamekuwa makazi ya Ma pope karibia 270 na kila mmoja alikuwa ameacha makarama na spirit yake kwenye yale makasiri.
Lakini Papa Francis isitoshe yeye ni mjamaa na anaishi kijamaa fulani kwani hata msosi wake anajipikia na alichodai kupewa apartment ndogo tu haoni haja ya mtu mmoja kuwa '000's of sq fts na big number of staffs (watwana na vijakazi🙂 wanaopishana na kupigana vikumbo kwenye corridor kwenye jumba saa zote na kubakia kuitikia wenyewe hata hawajaitwa na mtu🙂
Ndio maana unaambia kiongozi makini ni yule 'anayeongoza kwa mfano' na yeye ameamua bila shaka wengine waliochini wataona haya. Kumbuka katika kanisa katoliki wako watumishi wanaishi 'very lavish life' na magenge ya ki mafia na ufisadi wa kutisha wakiwemo ma priests na Ma Bishop hata baadahi ya viongozi waandamizi huko Vatican kwenyewe. Hivyo nafikiri anajaribu kuleta mageuzi ya kimitazamo ili kanisa lipate kuchukua mwelekeo mpya wenye matumaini kwa waumini.