Panya road wafanya uporaji Yombo Buza

Hawa watoto walikuwa wanawezana na walimu, walimu hutoa adhabu kulingana na tabia pamoja na kosa la Mtoto.
Mfano mtoto ambaye ni panya road hawezi kutii mwalimu, hivyo walimu hupambana naye mpaka baadae ananyooka Mwenyewe.

Lakini walimu wakipambana nao mnasema walimu wakatili sana, sasa watoto kama hawa na umeambiwa wengine ni wanafunzi wakikutana na walimu wakaleta ubabe walimu wawaangalie tu?

Kutokana na lawama za wazazi walimu wameweka watoto kwenye makundi, kuna wengine hata wafanye nini hawapewi adhabu.

Adhabu hizi tutakuuja kufidia sisi wazazi watoto hao wakiingia mtaani,

Safi sana walimu upole wenu tunauona,
Acha wazazi waendelee kuwatete baadae wataanza kuwabaka wazazi na Kuwa***ti wazazi hao hao. Walimu Fudisheni tu msitoe adhabu.
 
Mkuu nilimaanisha hivi;

Mtoto akiwa nyumbani ni jukumu la mzazi,akiwa Shuleni kwa kawaida anakua chini ya uangalizi wa Shule "Walimu" akiwa mitaani ni jukumu la kila raia kumkanya au kumuongoza anapoona anafanya jambo lolote baya,

Watoto ndio taifa la kesho, na bila kutengeneza kizazi kijacho kua na maadili mazuri nadhani itakua ni tatizo kubwa huko mbeleni,

Huu ni ushauri tu,najua ni ngumu kiasi but we have no choice kama tunataka amani na kua na taifa bora.

Mkuu hivi unawafahamu wazazi wa kizazi kiki?.
Mzazi ukimuonya mtoto wake anakuja na mapovu na matusi lukuki, ukimwelewesha anakuambia mtoto ni wake mwache usimguse wala kumkemea . Tofauti na wakati tunakua sisi.
Kama mzazi mwenyewe anatembea nusu uchi, baba chapombe unategemea nini hapo?. Niwimbi la hiyo mitoto. Dawa Muishio dar nanyi muwe na kundi lenu la paka rodi, Yaani jino kwa jino. Akitishia unatenga shingo uone kama wataendelea wajinga hao.
 
Nadhani hapa pia kuna tatizo kubwa la Malezi,


Mtoto anatoka usiku mnene kama huo mzazi unakua wapi? Wazazi wengi wamekua "Bize" sana na mambo ya kimaisha na kusahau kua na muda wa malezi wa kumfuatilia mwanae hasa vitendo vyake na marafiki anaozunguka nao, kujua marafiki wa mwanao ni jambo la msingi mno ili kuona mwanao ana muelekeo gani,

Pia kuna hili suala la kubeti,hii ni kama kucheza Kamari, mtoto akikosa hela za kubet basi atajaribu kuzitafuta kwa njia yeyote ile ili tu akabeti coz amesha kua addicted na mchezo huo,

Wazazi tujitafakari na malezi ya vijana wetu kabla ya kuvitupia lawama vyombo vya ulinzi,

Malezi ni jukumu la kila mzazi na kila mwalimu na wananchi kwa ujumla.

Punguzeni kutia mimba wanawake halafu mnakimbia majukumu, matokeo yake kunakuwa na watoto mwitu wenye hasira, waliokosa upendo wala ubinadamu.
 
Back
Top Bottom