bora mim
JF-Expert Member
- Aug 6, 2014
- 552
- 735
Tunaomba mtuache walimu, waleeni wenyew watoto Wenu.Nadhani hapa pia kuna tatizo kubwa la Malezi,
Mtoto anatoka usiku mnene kama huo mzazi unakua wapi? Wazazi wengi wamekua "Bize" sana na mambo ya kimaisha na kusahau kua na muda wa malezi wa kumfuatilia mwanae hasa vitendo vyake na marafiki anaozunguka nao, kujua marafiki wa mwanao ni jambo la msingi mno ili kuona mwanao ana muelekeo gani,
Pia kuna hili suala la kubeti,hii ni kama kucheza Kamari, mtoto akikosa hela za kubet basi atajaribu kuzitafuta kwa njia yeyote ile ili tu akabeti coz amesha kua addicted na mchezo huo,
Wazazi tujitafakari na malezi ya vijana wetu kabla ya kuvitupia lawama vyombo vya ulinzi,
Malezi ni jukumu la kila mzazi na kila mwalimu na wananchi kwa ujumla.