Panga pangua serikalini

Panga pangua serikalini

Agama_Agama

Senior Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
141
Reaction score
135
Ikiwa imepita zaidi ya miaka mitatu toka awamu ya tano kuingia madarakani, tumeshuhudia panga pangua ya safu za uongozi kila kukicha. Hii ilianza mapema tu baada ya awamu mpya kushika nchi.

Nimejaribu kufikiri kwa akili chache tu kwamba haya mabadiliko ya viongozi kila siku yana faida zaidi ya hasara au la.

Hii haimanishi kuwa napinga mabadiliko yenye kulenga maboresho kwenye serikali. Fikra zinazonijia zinanitatiza maana nakosa kuelewa shida ipo wapi. Je, ni wateuliwa kutokufaa kwa nafasi husika? Au mteuzi kutokujua nani anafaa wapi?

Nimezungumzia suala la muda nikitafakari kuwa awamu ina miaka mitano. Nusu ya kwanza ya awamu hii imekwisha na sasa tunashambulia nusu ya pili.

Kwa uelewa wangu nadhani muda wa kutengeneza mifumo ya utawala ilikuwa mwaka wa kwanza. Kama nchi inakuwa na vision na mission basi zinatekelezwa kwa muda uliobaki. Ili kuwezesha hili lifanikiwe tunahitaji stability kwenye uongozi. Sasa zoezi la hamisha, tumbua, tengua, teua na yanayofanana nayo linaleta ukakasi kwenye kufikia azma hii.

Kila mtu anahitaji adaptation ili kuweza kuleta tija hususan kwenye uongozi. Sasa haya mabadiliko ya kila kukicha yananipa mashaka kama Kweli tunaweza kufikia maono ya mtawala ambayo wateuliwa wanatakiwa kuyafikia.

Mwaka huu utaisha tukiwa bado tunateua watendaji na uchaguzi mwingine utafika tukiwa hatujaona mwelekeo kama nchi.

[emoji2986]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja yako ni ya msingi kwamba tunaktakiwa kutengeneza mfumo wa utawala, kwa mantiki kuwa kwa sababu Tanzania haijapata uhuru leo, mfumo huu tulitakiwa tuwe tumeshautengeneza tangu huko nyuma, lakini nadhani tulishindwa. Kwa hali hiyo basi, sasa hivi tunatakiwa kuwa kwenye operation ya mageuzi ya uchumi, mfumo utakuja kujipa wenyewe huko mbele ya safari by the way. Tumwacheni Rais afanye kazi hata akianza na Mawaziri 30 mwanzoni mwa awamu halafu akaja akamalizia na wengine 30 mwishoni mwa awamu ambao ni tofauti na alionza nao, bado kwetu sisi inafaa, na hasa ndiyo kitu kinachotufaa zaidi kwa kipindi hiki. Tuko kwenye operation ya mabadiliko ya uchumi na huku tukionyesha namna discipline ya watumishi wa umma inavyotakiwa kuwa, kwa maana kwamba hata hiyo discipline hatuna isipokuwa tunajaribu kuitafuta alongwith issue ya ujenzi wa uchumi.
 
Mkuu una point. Lakini naona tunafanya kitu inaitwa trial and error kila siku. Unadhani huu mfumo utakuja kupatikana kwa hii style?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu una point. Lakini naona tunafanya kitu inaitwa trial and error kila siku. Unadhani huu mfumo utakuja kupatikana kwa hii style?

Sent using Jamii Forums mobile app

Nadhani hatutakiwi kuutengeneza, ila utajiset wenyewe tukishajenga discipline ya kazi na kukomesha ufisadi. In as much as kama ambavyo huwezi kumwongezea kimo mtoto wako kwa kumunyumbulisha viungo ili akue na kuongezeka kimo, bali kwa kumpa lishe nzuri na inayotakiwa, vivyo hivyo mfumo huu hatutakiwi kujikita katika kuujenga kwa staili hiyo, tunatakiwa tuchape kazi, tujenge discipline ya kazi na tuachane na mambo ya ufisadi. Tukishetekeleza yote haya, mfumo utajiset wenyewe automatically , believe me!
 
Back
Top Bottom