Panga la JPM sasa lanyemelea balozi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,814
34,195
pic+panga.jpg

Rais John Magufuli.
Dar es Salaam. Baada ya kukamilisha uteuzi wa baraza la mawaziri na makatibu wakuu ulioingiza sura nyingi mpya, pangapangua hiyo sasa inawanyemelea mabalozi na maofisa wao wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.

Baada ya kuingia Ikulu, Rais John Magufuli alianza kupunguza gharama za uendeshaji Serikali kwa kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma isipokuwa kwa kibali cha Ikulu, akitaka shughuli hizo zifanywe na kusimamiwa na mabalozi.

Magufuli pia aliamua siku ya Uhuru isherehekewe kwa kufanya usafi na fedha ambazo zingetumika kwenye sherehe hizo zielekezwe sehemu nyingine, na pia kupunguza gharama za sherehe za kupongeza wabunge na kiasi kilichobaki kilitumika kununulia vifaa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Kasi hiyo ya kupunguza gharama za uendeshaji Serikali, sasa inaelekea kuangaza kwenye balozi za Tanzania nje, ambako mbali na kupunguza watumishi na kubadilisha mabalozi, Serikali pia itataka kuwaondoa wale waliomaliza muda wao.

Kuna taarifa kuwa mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania watapewa amri kurejea nyumbani wakisubiri uteuzi mpya, huku wengi wao wakistaafishwa.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga alisema Rais Magufuli hajatoa maelekezo yoyote kuhusu suala la mabalozi japo wakati ukifika atafanya hivyo kulingana na mahitaji ya nchi. Alisema lengo la Serikali ni kuongeza ufanisi katika utendaji wake wa kazi kitaifa na kimataifa hivyo kuwapo kwa mabadiliko hakutaweza kuzuilika.

“Tunatakiwa kujipanga upya ili kuhakikisha kila mmoja anafanya kazi kwa bidii na kwa weledi kwenye nafasi aliyopewa. Nadhani tusubiri kwa sababu wakati ukifika Rais atatuelekeza nani anaenda wapi, anabaki au anastaafu, kinachoangaliwa zaidi ni kuongeza ufanisi,” alisema Balozi Mahiga.

Wasomi walonga

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa (UoI), Jimson Sanga alisema mabalozi walioshindwa kuiwakilisha Tanzania ipasavyo lazima matumbo yao yapate joto wakihofia kustaafishwa kwa lazima.

“Natarajia kuziona sura nyingi mpya kwa kwa sababu kazi ya balozi siyo tu kukaa huko nje, ni kuiwakilisha nchi kwa kufanya kazi zote zinazowahusu, hasa za kidiplomasia. Kwa wale walioshindwa kutumiza wajibu wao lazima waugue kwa sababu wanajua Serikali iliyopo madarakani siyo ya kubebana, uwezo wa kazi ndiyo sifa pekee,” alisema Sanga na kuongeza: “Ukizungumzia balozi maana yake ni mtu anaeweza kuizungumzia nchi yake kule anakoiwakilisha. Kwa kifupi anakuwa pale kama nembo ya Taifa, bila shaka elimu ya kidiplomasia ndiyo inayotakiwa kuwa sifa moja wapo wakati wa uteuzi.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Dk Richard Mbunda alisema ilifika hatua balozi anakosa kazi ya kufanya, kama kuingia makubaliano yoyote kwa niaba ya nchi yake, kutokana na wanaohusika na sekta hiyo kuamua kwenda wenyewe.

“Balozi wa nchi ni kama Rais kule anakoiwakilisha nchi yake. Ndiye msemaji na mtendaji mkuu kwa niaba ya Serikali iliyompeleka hivyo natarajia kuona mabalozi watakaopelekwa na Serikali hii, kuwa ni wale wenye weledi na uwezo mkubwa wa kuiwakilisha nchi yao,” alisema Dk Mbunda.

Mhadhiri mwingine wa UDSM, Patrick Myovela alisema anatarajia kuona sura nyingi mpya kwenye uteuzi wa mabalozi, kutokana na kazi nzito ya uwakilishi wa nchi iliyo mbele yao.

“Kama kuna ambaye hakutimiza wajibu wake, panga haliwezi kumuacha. Kinachotakiwa ni uwezo wa kusimamia maslahi ya Taifa hasa kupitia sera ya uchumi,” alisema. Myovela alisema uwakilishi mzuri wa balozi, unaweza kuongeza wawekezaji ndani ya nchi na hivyo kusaidia katika kukuzwa uchumi. chanzo.Panga la JPM sasa lanyemelea balozi


KWA HILO JAMBO ATAKALO FANYA RAIS MAGUFULI KUWASTAAFISHA MABALOZI

WALIOKUWEPO NCHI ZA NJE

NINAMUUNGA MKONO RAIS WETU MAGUFULI ONA HII HABARI CHINI JINSI UBALOZI WA ITALY

WALIVYO TUNYIMA NA KUTUZUNGUSHA KUHUSU MAOMBI YETU YA PASSPORT MIAKA YA NYUMA.



Malalamiko Ubalozi wa TZ Italy.jpg
Malalamiko Ubalozi wa TZ Italy.jpg
 
Waraka wa Wakereketwa kuhusu "Ubaya wa Ubalozi wetu wa Italy"
Info Post
Subi Nukta
10/02/2014 09:06:00 PM
No Comment

UBAYA WA UBALOZI WETU WA ITALY

Tunaomba uitangaze habari hii bila kuificha na wala usipunguze hata herufi moja!!!

Kila aliyewahi kuomba huduma toka ubalozi wetu wa Rome ana malalamiko yake. Ima atakuwa amecheleweshwa mno kupatiwa huduma hiyo au hakupatiwa kabisa.Muda mrefu tumenyamaza kimya tukitegemea kuwa hali ingebadilika, lakini kila siku zinavyokwenda mambo ndivyo yanavyozidi kuwa magumu na kuharibika hasa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kutozingatiwa matatizo yetu limekuwa ni jambo la kawaida mno kiasi cha kutufanya tujiulize mara mbili.. Sisi kweli ni raia wa Tanzania wenye haki ya kupatiwa msaada toka ubalozini kwetu?

Mara zote msaada tunaokuwa tukiuhitaji SI PESA, kiasi cha kwamba Mh. Balozi aseme kuwa nchi yetu haina uwezo wa kipesa kusaidia raia wake. Msaada tunaoomba ni KUPATIWA VYETI HUSIKA ILI NASI TUWEZE KUKAMILISHA HATI ZA UHALALI WA UKAAZI WETU.

Matatizo yetu yana sehemu tatu kuu zifuatazo:

  1. Hivi sasa watu wengi pasi zetu zinaisha 2015 na tumeshamuomba Mh.Balozi amtume Afisa wa pasi-japo kwa gharama zetu - aje kututatulia tatizo hilo HAJAFANYA LOLOTE. Mh.huyo katuimbisha kuwa angemtuma Afisa wa pasi August au September, kuja kuonana nasi na miezi hiyo imeshapita na hatuoni dalili zozote za kusaidiwa. Kuna hatari kubwa ya wengi kutokuwa na valid passports ifikapo 2015, Je tutawalaumu watu watapotumia njia za kienyeji na za vichochoroni kutatua tatizo lao?
  2. Kuna watu wameomba pasi imeshapita sasa miaka miwili na stakabadhi za malipo wanazo na wala hakuna jibu lolote la maana wanalopewa.
  3. Tuna watoto wetu waliozaliwa huku hawana pasi wanashindwa kusafiri na wazazi wao kuja Tanzania. Ubalozi unashindwa vipi kutoa huduma japo mara moja kwa mwaka?
Tunaamini udhalilishaji huu unatokana na filosofia ya Mh Balozi ya kutojali watu anaowaongoza maana inajulikana hata huko mikoani alipokuwa (Dodoma & Mwanza) wananchi hakuwa akiwajali. Tunahofia asije akawa anataka kuendeleza mfumo huo hata huku ughaibuni. Mbona Mheshimiwa Rais Kikwete yupo very simple? Anajali na huwatembelea raia wake mara kwa mara? Hata misiba ya raia wa kawaida huwa anahudhuria, sasa huyu Balozi yeye ni nani? Je yeye anajiona ni bora kuliko Rais wetu?

Tumelazimika kueleza yote haya si kwa sababu tunataka tu kulalamika LA HASHA, bali tumeona tukiendelea kuficha, kilio kitatuhusu. Yes KI - TA - TU - HU - SU.

Tunaviomba vyombo vyote vya habari vifikishe udhalilishaji huu kwenye idara husika hasa Bungeni na kwa Mheshimiwa Rais ili waelewe kuwa UBALOZI WETU WA ITALY HAUJALI WATANZANIA. UNAJALI MASLAHI YAO YA KIBINAFSI.

LABDA TAARIFA HII ITAZIAMSHA BALOZI NYINGINE ZIWEZE KUWAJALI RAIA WA TANZANIA. SISI TUNAJIVUNIA URAIA WETU HATA KAMA BALOZI HATUJALI NA TUNAIPENDA NCHI YETU NA TUTAENDELEA KUIPENDA NA KUITUKUZA. TUTAFURAHI KUONA NA MABALOZI WETU WANAELEWA UMUHIMU WA KUWAJALI WATANZANIA KULIKO MASLAHI YAO YA KIBINAFSI.

Imeandikwa na :
(WAKEREKETWA WA UTURUKI, UGIRIKI, NA ITALY)

chanzo.Waraka wa Wakereketwa kuhusu "Ubaya wa Ubalozi wetu wa Italy" - wavuti
 
Wahusika Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje Tumbuwa hayo majipu. Ukishindwa Mkabidhi Mheshimiwa Rais Magufuli ayatumbuwe hayo Majipu yanatusumbuwa sana tunashindwa hata kurudi nyumbani kuwatembelea Wazazi wetu kwa kukosa Passport za kuasafiria. Tumechoka kuteswa kwa haki zetu wenyewe.
 
Wahusika Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje Tumbuwa hayo majipu. Ukishindwa Mkabidhi Mheshimiwa Rais Magufuli ayatumbuwe hayo Majipu yanatusumbuwa sana tunashindwa hata kurudi nyumbani kuwatembelea Wazazi wetu kwa kukosa Passport za kuasafiria. Tumechoka kuteswa kwa haki zetu wenyewe.
Mheshimiwa balozi ni mhandisi aliebobea mwenye mambo ya umeme.

Inawezekana kabisa kurudi nyumbani kusaidia Tanesco maana amewahi kufanya kazi hadi kwenye shirika la umeme nchini Sweden.

Au itabidi arudi kufundisha vyuoni maana kwa taaluma huyu mzee wetu sio mwanadiplomasia na ndio maana alikuwa akionekana hivyo alivyo.
 
Mheshimiwa balozi ni mhandisi aliebobea mwenye mambo ya umeme.

Inawezekana kabisa kurudi nyumbani kusaidia Tanesco maana amewahi kufanya kazi hadi kwenye shirika la umeme nchini Sweden.

Au itabidi arudi kufundisha vyuoni maana kwa taaluma huyu mzee wetu sio mwanadiplomasia na ndio maana alikuwa akionekana hivyo alivyo.
Ufumbuzi mzuri Rais Magufuli awastafishe hao Maofisa wa ubalozi waliko nchi za nje aweke Mabalozi wapya hawafai hawa Maofisa wa Ubalozi wa zamani hata kidogo kutuongoza sisi Raia tuliopo nchi za nje wanatutesa sana.
 
Ufumbuzi mzuri Rais Magufuli awastafishe hao Maofisa wa ubalozi waliko nchi za nje aweke Mabalozi wapya hawafai hawa Maofisa wa Ubalozi wa zamani hata kidogo kutuongoza sisi Raia tuliopo nchi za nje wanatutesa sana.

Balozi kama yule wa UK ni mwanadiplomasia na anaonekana hata kwenye mikusanyiko ya kawaida ya watanzania.

Inawezekana kabisa wakateuliwa mabalozi wapya kutoka wizarani na wengine kuhamishwa.

Tumsubiri raisi na mipango yake.
 
HIYO BENDERA NDIO OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA ULIOPO MJINI ISTANBUL NCHINI TURKEY. NI MTURUKI MFANYA BIASHARA MMOJA AMEJITOLEA KUWEKA HUO UBALOZI WA TANZANIA NCHINI TURKEY SERIKALI YA TANZANIA HAINA OFISI YA UBALOZI NCHINI TURKEY NI JAMBO LA AIBU SANA.WAKATI WATURUKI WANAO OFISI YA UBALOZI HAPO KWETU TANZANIA MJINI DARES-SALAAM.
Ubalozi wa Tanzania nchini Turkey..jpg
 
Huyo wa mabo ya nje ni mzeeeeeeeee kwanza kishajichokea sidhan kama bado IQ yake inatunza kumbukumbu; mpaka sasa tangu ateuliwe wala hatujamskia akisema chchte utadhani wizara yake haina daily activities; sjui jpm hakupa watu wenye umri wa wastani ktk hii wizara!! ngoja tuone naye atakavyoibuka. Pengine, labda tuvute subira tumpe @least a year; vinginevyo watu wenye umri kama huu hawapaswi kuwa tena wateule sehemu za uwazir.
 
Back
Top Bottom