Panga la JPM lachinja vichwa 152

Panga la JPM lachinja vichwa 152

haiw

haiwezekani wewe ukawa mwana ukawa. huwezi mtaja mzee wa Richmond hivihivi. nani kakwambia umtaje? ? yeye mbona Mbowe alishamsafisha
e
Kiukweli mimi ni mwana ukawa tena kindakindaki lakini Kitendo cha Lowasa kuja huku kiukweli tuache unafki tulikosea sana
Ila hilo haijawi kunifanya niwaamini ccm
Haiwezi ikatokea
Kwa sababu najua ccm ni ile ile ooh ni ile ile
 
Kufukuza watu ni moja ya hatua za kushughulikia ufisadi lakini ndogo sana hasa ukizingatia jinsi nchi yetu ilivyokuwa ikiendeshwa toka juu (Ikulu) kwa mfumo wa kifisadi. Kuna watumishi wengi tu waliolazimika "kufanikisha" ufisadi wa wakubwa wao ili wadumu kazini au wapandishwe vyeo. Wapo waliofukuzwa kazi kwa kujifanya "wanoko" sana.

Kazi kubwa sana inayotakiwa kufanywa kwa haraka ni kuminya mianya kadhaa iliyotegwa huko nyuma inayoliibia taifa kiasi kikubwa cha fedha za umma. Kwa mfano mkataba wa (IPTL) ni janga la taifa usipositishwa mapema. Mingine kama ya Symbion/Richmond, gesi, madini nayo ichunguzwe na kuwekwa sawa asap. Kwa bahati mbaya waliohusika kuandaa mikataba yenye ufisadi mkubwa unaoibana serikali ni kama vile hawagusiki (the untouchables)!

Kuziba mianya hiyo kukiambatana na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wakuu (mafisadi papa) ndipo tutakapoanza kupata mabadiliko ya kweli tunayotarajia. Kutimua watendaji wa umma kumesaidia kutoa ujumbe kwamba Ikulu ya safari hii ni nyingine lakini bila mianya kudhibitiwa ni suala la muda tu tutarudi kulekule. Halafu inawezekana pia kuna wahanga wengi waliotimuliwa wakitekeleza matakwa ya mabosi wao kwa jinsi navyoifahamu serikali.

La muhimu zaidi ni kukamilisha Katiba itakayoondoa fursa za kifisadi na kusimamia haki za wananchi wote.
 
Magufuli hawez kuwa rais bora hata robo.. Hana hiyo karba.. dhambi ya kwanza ni kwasababu yy hakushinda taasisi ya Urais
 
Yani kila cku wanafukuza mwishoe wataanza kujifukuzisha wenyewe. Wanaona kiongoz bora ni Yule anayefukuza wafanyakazi . Wamesahau kiongoz anatakiwa kuwa na busara .hekima,akili, na maarifa.
***************************************
HUONI TIJA "TRA" HII NI TIJA AMBAYO IMEPATIKANA BAADA KUUONDOA MTANDAO WA UCHAFU,
"MTANDAO WA UCHAFU"
Ni kikundi cha mnyororo wa waovu ambao huwa ni hatari sana/
mtandao / chains ni watu wengi!!
DAWA YAKE KUONDOA WOTE.
 
Yani kila cku wanafukuza mwishoe wataanza kujifukuzisha wenyewe. Wanaona kiongoz bora ni Yule anayefukuza wafanyakazi . Wamesahau kiongoz anatakiwa kuwa na busara .hekima,akili, na maarifa.
Jamani kumbe falsafa ya kutumbua majipu haikueleweka. labda la muhimu wataje walioondolewa kwa kuonewa.
 
Yani kila cku wanafukuza mwishoe wataanza kujifukuzisha wenyewe. Wanaona kiongoz bora ni Yule anayefukuza wafanyakazi . Wamesahau kiongoz anatakiwa kuwa na busara .hekima,akili, na maarifa.
Kiongozi mwenye busara, hekima, akili na maarifa watz kwa wingi wetu tulimpiga chini kupitia sanduku la kura.

Tulimbaini kuwa sifa ulizozitaja(ambazo mnadhani anazo) hana, ni danganya toto. Ana shahada ya sanaa, sijui maigizo.......... chungaaa...,

Tumemchagua huyu fukuza fukuza, haijalishi utampa sifa gani ilimradi atutoe hapa tulipofikia- taifa la wezi na wasiowajibika.

Kaeni pembeni, mwanamume apige kazi, mtaelewa mbele ya safari. Anasema hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom