Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,868
- 730,469
Tanzania chini ya mchonga pekee ndio ilikuwa
Tanzania ya maono
Tanzania ya mikakati
Tanzania ya utawala wa sheria nani afanye nini kwenye nini
Tanzania yenye mwelekeo sasa
Tanzania yenye dira ya tulikotoka tulipo na tuendako ....matokeo yalionekana wazi hasa kwenye viwanda vyetu wenyewe hasa kwenye nyanja za michezo viwanda na kilimo
Nyerere akang'atuka mwaka 1984/85...akiwa anaamini ana vijana aliowapika vema! Mapando aliyoamini ameyamea vema na kuyapa samadi bora ya afya elimu na hata uzalendo kwa nchi Kama taifa na Afrika kwa ujumla wake
Akachukua mzee Mwinyi na kuleta uchumi wa soko huria na bila maono ya mbali wala maandalizi ya kutosha
Unapofungua dirisha kupitisha hewa safi hata vichafu hupitia hapo hapo.... Tukayumba mno lakini miaka kumi ikapita salama
Akaingia mzee Ben mtemi jeuri lakini mwenye hekima akaja naye na sera zake tofauti kabisa na mzee Mwinyi ,kidogo heshima ya nchi ikarudi lakini naye akiwa kafanya yake yasiyovutia.. Akamaliza miaka yake kumi salama na sasa anakula bata
Kijiti cha Mkapa kikapokelewa na Jemadari kikwete... Yeye akalegeza kidogo wananchi wakamfurahia sana lakini akasau kukaza pale alipolegeza hivyo pakalegea kabisa, ikaja kuthibitika kuwa yeye si mtu wa maamuzi magumu na hupenda kumridhisha kila mtu.. Ameondoka akiitwa Mr dhaifu
Wananchi wakiwa wamechoshwa mno na hali ya mambo ilivyo wakaamua kukipumzisha chama tawala kupitia box la kura, lakini kikwete hakukubali hili litokee... Ikafanyika rafu ya wazi kabisa na matokeo yanajulikana wazi
Haya Mapando matatu baada ya mchonga yamefanya crossbreeding mbaya kiasi kwamba matokeo yake imetokea mmea mpya ambao badala ya matunda hata kwenye hatua za awali kabisa maua yake yanaonyesha wazi kabisa kuwa matunda yake hayatakuwa tufaa wala embedodo bali miba za michongoma itakayomchoma kila mmoja wetu bila kujali
Pando la mwisho limetumia mbolea ya viwandani yenye sumu na kemikali nyingi zenye kudhuru mwili.....
Lawama hizi je zinamtahili mchonga?