Kinachoendelea katika taifa letu kwasasa nakifananisha na sarafu kuwa na pande mbili zenye muonekano tofauti.
Wakati wa utawala wa shujaa wetu habari zilizokuwa zinasikika zilikuwa zinahusu mazuri ya Shujaa wetu na serikali yake tu. Ulikuwa huwezi kusikia mabaya yake au ya serikali yake kwenye chombo chote cha habari, vijiweni, na hata kwenye nyumba za ibada.Tbc wao walianzisha mpaka kipindi walikiita kishindo cha awamu ya tano, kipindi hicho kilikuwa kina kazi moja tu kusifia awamu ya tano.
Wachache waliojaribu kukosoa na kuelezea makosa walikiona cha mtema kuni.
Kutokana na uhuru wa kukosoa wa vyombo vya habari, wanasiasa na wanaharakati kuminywa na badala yake tbc, na baadhi ya magazeti yaliyoamua kujisalimisha, na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini walioamua kujifungamanisha na uongozi wa serikali kuanza kusifia tu bila kukemea ubaya hata pale ulipokuwa dhahiri, wananchi wengi nao waliingia imani kwamba serikali yetu chini ya shujaa ilikuwa takatifu kama Malaika.
Baada ya kutokea kilichotokea, sasa kuna ripoti ya CAG imejaribu kuanika udhaifu na mapungufu mengi ya utawala wa shujaa. Yaani kutuonyesha upande wa pili wa sarafu.
Watu wengi hasa wale walioaminishwa kwamba utawala uliopita ulikuwa ni wa watakatifu wamepigwa na butwaa, hawaamini walichokisikia au kukisoma kwenye ripoti ya CAG.
Wengine wamefikia kusema ripoti hii imetolewa makusudi kwa nia ya kumchafua shujaa. (wanahoji kwamba ripoti kama hiyo mbona haikuwahi kutolewa enzi zake?)
Bahati mbaya wamesahau kilichomkuta CAG aliyetangulia alipojaribu kuonyesha udhaifu wa serikali kwenye ripoti zake ikiwemo upotevu wa 1.5 trillion.
Vile vile wamesahau onyo alilopewa huyu CAG alipoteuliwa kwamba wewe ni CAG usiende kujifanya na wewe ni mhimili mwingine wa serikali. Mihimili inajulikana ni mitatu na viongozi wa mihimili hiyo wanajulikana. Sasa katika mazingira kama hayo unadhani huyo CAG alikuwa na ujasiri gani wa kuanika udhaifu wa serikali?
Lakini juzi tulimsikia mama akisisitiza ripoti ya CAG iwe wazi zaidi bila kufichaficha mambo. Hicho ndo kilichofanyika na ndio maana watu wengi wamepigwa na butwaa maama hawakuzoea kusikia ripoti kama hiyo enzi hizo.
Walizoea kuona upande mmoja wa shilingi wa mazuri ya awamu ya tano wanashituka kuona udhaifu huo wanadhani ni njama za kumchafua shujaa.
Uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa vyama siasa na wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wakosoaji unapokosekana si rahisi kujua udhaifu wa serikali.
Ni vizuri sasa tuelewe kwamba sarafu siku zote inakuwa na pande mbili zenye picha tofauti.