Pamoja nasi au kinyume nasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja nasi au kinyume nasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BABA JUICE, Feb 26, 2011.

 1. BABA JUICE

  BABA JUICE JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Demokrasia ni nini hasa katika nchi za kiafrika! Toka huu mwaka uanze tumeshuhudia viongozi wakiondolewa madarakani ,mapinduzi hayo yalianzia Tunisia yakaelekea Misri na sasa Libya. Tukirudi nyuma unakumbuka baada ya world trading center kulipuliwa, jaribu kukumbuka statement ya Bush “EITHER YOU ARE WITH US OR AGAINST US”Kilichofuata ni uvamizi Iraq na Afghanistan na sheria ya ugaidi kulazimishwa katika nchi za kiafrika. Hivi ndivyo jinsi mmarekani anavyosambaza demokrasia yake. Tukirudi katika mada kuu,hawa viongozi ambao wananchi hawawataki wamekaa muda mrefu kweli madarakani na ukiangalia kwa upana zaidi muda wote waliokaa madarakani bado hawajawapa wananchi unafuu wowote wa maisha, kipindi chote hicho nchi za ulaya na marekani zilikuwepo na hazikusema chochote kwasababu walikuwa wanalinda maslai yao leo hii wao ndio wa kwanza kukosoa utawala wa hawa viongozi na kutoa siri zao, huoni kama huu ni unafiki kwa haya mataifa yanayojifanya yanaitakia demokrasia nchi za kiafrika. Ukiangalia kwa nchi kama ya Libya kiongozi wao amejitaidi kwa kiasi kikubwa kuleta unafuu kwa wananchi wake lakini kwa upande mwingine amewanyima wananchi wake uhuru wa kutoa mawazo na kuvibana vyombo vya habari lakini Libya ni nchi amboyo imepiga hatua ukilinganisha na Tanzania, muda mwingine nimesikia watu wakisema hii nchi inaitaji kiongozi ambaye ni dictator kwani wananchi wamechoshwa na hawa viongozi wanaojali maslai yao na wasio kuwa na msimamo. Kweli Africa inaitaji democrasia kweli na nini hasa ni democrasia kwa nchi zetu,ukimuangalia Robert Mugabe(Africa Leader) kachaguliwa kidemocrasia kama hao western countries wanavyotaka lakini juzi tu chokochoko zimeanza kwenye media kwamba nae Mugabe aondoke!jamani huyu mtu si kachaguliwa kidemocrasia kabisa na kuna serikali ya umoja, kwa mtazamo waqngu hizi nchi za ulaya zinataka kuitawa afrika kwa njia nyingine ukiachia ukoloni, ni democrasia ya aina gani wanataka katika nchi zetu?unajua wananchi wa Tunisia,Libya au misri sio kwamba wanataka democrasia hapana angalia kiundani kwa mfano hapa kwetu Tanzania tunaiji democrasia kweli au tunaka umeme wa uwakika,ajira,uduma bora ya afya, miundombinu na makazi bora na uchumi wa uwakika vitu hivi vyote wanachi ndio tunataka, lakini hakuna kiongozi wa kutupa pamoja na demokrasia yetu hii. Itafika siku na sisi tutachoshwa na demokrasia ya mmarekani na kuleta democrasia yetu sisi, ukiangalia kiundani umasikini ndio unazidi kuongezeka kwasababu viongozi wetu hawana kauli wanongozwa na hao waliowaletea democrasia.
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  usitegemee demokrasia itakuja kwa kuziachia nchi za ulaya na marekani, maana kila taifa lina masirahi kwa nchi za afrika hivyo hata hili vunguvungu la mapinduzi unaweza kuona lina sababishwa na wao hasa pale wanapotunyonya kupitia viongozui wetu vishoka, vilazi, na wenye uchu na utajiri kama rais wa misri, wanawatumia sana ili wa chote malighafi zetu. lakini mwisho wake wanawangeuka nakuwafungulia mashidaka au hata kuwaua. tuna mifano mingi tu ,Charles teira, osama, sadam wote wametumiwa sana na marekani lakini mwisho wake tumeuona na bado tunao hao viongozi wanaojipendekeza kila siku utazani kama wameolewa na Marekani kila kukicha wanaenda kuomba misaada je unategemea watavuna nini kama sio ujinga na kuendeleza wimbi la kuiba malighafi zetu?
   
Loading...