Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Ndugu yangu; kazi ya kiongozi ni kuwasaidia wengine kwa namna yoyote iwezekanayo na naamini uliipigania nafasi hiyo kwa lengo la kuwasaidia vijana kwa vile utakavyoweza.
Comrade mwenyekiti; tukuombe jambo moja ambalo kwa sasa pengine ndio changamoto kubwa zaidi inayowakabili vijana na kwa bahati mbaya si vijana wenyewe wala wazee wetu ambao wameweza kuishughulikia na kuipatia suluhu kikamilifu licha ya jitihada mbali mbali zinazofanyika.Tunaamini wengi wanaliona hili na wangependa litatuliwe lakini mjadala unaweza kuwa juu ya njia bora zaidi ya ku address changamoto hii.
Mkuu; wewe pamoja na timu yako, itapendeza kama mtakaa na kuandaa mkakati mzuri juu ya kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini kwani vijana wengi sana wanashindwa kufikia ndoto zao kutokana na changamoto hii.
Mkuu suala hili ni gumu lakini linaweza kushughulikiwa na serikali ya Ccm kama ikitia nia, nanyi mkawaongoza vijana wengine kuweka input za maana katika hilo .
Hata hivyo ni vyema vijana wenyewe wakafanya uchambuzi wa changamoto hii na kuwashauri viongozi wa nchi namna ya kukabiliana zaidi na changamoto hii ambayo inazidi kuongezeka kila Siku. Kimsingi, Wewe na timu yako kama mtaona inafaa na ikiwapendezeni, mnayo nafasi nzuri ya kuwaongoza wengine katika hili.
Kuhusu mahali pakuanzia; mambo mawili yaneweza kuzingatiwa ikionekana inafaa.
Kwanza, mnaweza kuratibu matamasha ambayo mnaweza kuwakutanisha vijana na watu ambao wanaweza kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa kuanzisha miradi yao wenyewe kidogo kidogo, kuweza kuwa " inspire" , kuwa "coach" na kuwa "motivate" ili wapate momentum ya kuanza. Jambo hili nimuhimu sana kwani wengi wana saikolojia ya kushindwa na hili ni tatizo kubwa.
Pili, hii ilishashauriwa huko nyuma kuwa muweze kutengeneza vizuri wazo lililotolewa kwamba, badala ya vijana wote kupatiwa mikopo wakasome chuo kikuu , kisha baada ya hapo zaidi ya 90% wakose ajira ya walichosomea, basi mikopo igawanywe mafungu mawili. Moja wapewe wanaopenda sana kuwa na degree na nyingine wakopeshwe wenye ndoto za kuwa na miradi na makampuni yao. Wazo hili limefafanuliwa vyema humu Jf na litazidi kufafanuliwa kwenye Uzi huu na
Tatu, kutengeneza plan yoyote mtakayoona inafaa kusaidia kukabili changamoto hii.
Mkuu, kama mkifanikiwa kulifanyia kazi jambo hili na likafanikiwa, mtakuwa mumewasadia vijana wenzenu wengi na hakika watawashukuruni. Kadhalika mtaacha alama katika uongozi wenu duniani na kwa Mungu mtakuwa na malipo pia. Ni nini basi mnaweza kufanya na kiwaka na faida kwa vijana kuzidi hili? Kama mkiona jambo hili ni jema basi fanyeni na hakuna atakayejutia. Nawatia moyo kuwa mkiamua mnaweza kufanya jambo kubwa ambalo halikutegemewa.